CCM inalia ngome zake zimemomonyolewa na M4C

mwanakidagu

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
208
78
CCM imechoka,inahitaji kuji reform upya,nguvu hiyo haina,ni kama mnazi uliofikia kikomo kuendelea kujizaa,imebaki na mlingoti uliosimama,bila ya matunda,hakuna tena uwezekano wa kuifanya iweze kuzaa matunda mema kwa watanzania,wala hakuna nabii anayeweza kuitabiria uhai wake,kwa kuwa yenyewe imefitinika tangu mizizi ,shina hata matawi,kama mjusi afavyo anavyo banwa na mlango huku akitazama,ndivyo amabavyo vuguvugu la mabadiliko lilo anzishwa na CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA(M4C),kote nchini kimesababisha kukiweka uchi chama hiki mbele ya wananchi waliodanganywa miaka nenda miaka rudi tangu uhuru.

CCM inalia,hakuna wa kuiunga mkono tena.nitafafanua,kwa sasa maisha ya watanzania ni magumu sana,hasa upatikanaji wa mahitaji muhimu, CCM haiana majibu kuhusu hilo,
haiungwi mkono tena na raia maskini,wakaao vijijini,ambao daima walikipenda chama hiki kwa mbwembwe zake.yenyewe imeamua yote liwalo na liwe,imeamua kutafuta mbeleko,ya kuibeba,kwa kutumia mbeleko hiyo imeamua kutisha,kubambikiza makosa,kuumiza raia wake ambao hawaiungi mkono( daudi MWANGOSI ALIULIWA KATIKATI YA KUNDI LA WANA USALAMA NA KAMANDA KAMUHANDA AKISHUHUDIA,MMOJA PEKEE NDIYE ALIYE FIKISHWA MBELE YAO,ILI WAJIHUKUMU WAO,HAO WENGINE KAMA HAWAFIKISHWI MBELE YAO,BASI IPO SIKU WATAENDA HAGUEKWA BI BENSOUDA) .haya yanayo jiri sasa hakuna tofauti na yale yaliyotendeka enzi za utawala wa makaburu wa africa ya kusini,mzee mandela alikuwa mtu asiyetakiwa kuishi,aliswekwa korokoroni kwa muda mrefu bila hatia,watu wake wengine walipotea bila kujulikana walipo,wengine waliuliwa kinyama,hiyo ni historia tu niliyoisoma wakati huo,basi ukishaona dalili kama hizi katika taifa lolote ujue mambo si sHwari.
nauliza,KILA KUKICHA,CHADEMA,CHADEMA,CHADEMA,CHADEMA,MITAANI CHADEMA.LUMUMBA CHADEMA,MASOKONI CHADEMA,VILABUNI CHADEMA,JEEE,MBONA KUNA VYAMA VINGI,CCM ACHENI USTAWI WA VYAMA VINGI UMEE NCHINI KWANI HII NCHI NI YETU WOTE,.mbona chama hiki kinaandamwa wakati ni cha msimu?.hofu yenu ni ipi kwa kuwa mlidai hakiwanyimi usingizi.?
kwa ufupi CCM ina hofu ya kuondoka madarakani,mara zote nimemsikia mwenyekiti wa CHADEMA akisema VYOMBO VYA DOLA,MTUACHE TUPAMBANE NA CCM PEKE YAKE,JE VYOMBO VYA DOLA NDIYO MBELEKO YA CCM? KARIBUNI KWA KUCHANGIA.
 
Mpaka Katiba mpya itakapotenganisha majukumu ya madola katika nchi, kamwe ccm haitaacha kutegemea mbeleko ya maguvu, maana majeshi yote, mahakama na bunge vyote viko chini ya utawala wa ccm kwa sasa na mkuu wake ni Mwenye kigoda wa ccm na rais wa nchi. Akikohoa tu, mate yakiruka hutofautishi ni ya ccm au rais au jemadari wa majeshi au mkuu wa vyombo vya dola. Tofauti wanazotuambia ni misemo ya kwenye jukwaa kumfunika mtoto alale usingizi.
 
Magamba wapo hoi,licha ya kutuita Magaidi CHADEMA imeongeza wafuasi kutokana na huruma ya wananchi juu ya Uonevu.
 
tunataka mtuhakikishie usalama wetu. mmekuwa ni chama cha matukio na pale yanapopungua mnafikia hata hatua ya kucreat matukio kama la kuwateka watu ili muendeleze agenda zenu. kwa taarifa yako mwisho wa ubaya ni aibu. na tayari imeshaanza kuwapata. na huu ni mwanzo tu.
 
Back
Top Bottom