CCM inakwenda arijojo - Mtei | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM inakwenda arijojo - Mtei

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fredrick Sanga, Apr 22, 2011.

 1. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Friday, 22 April 2011
  Fidelis Butahe


  MWASISI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema siku za CCM kukaa madarakani zinahesabika kwa kuwa chama hicho kimekosa usimamizi bora na hivyo kuiyumbisha nchi.

  Akijibu maswali mbalimbali ya Mwananchi jana, Mtei alisema chama hicho kimeshindwa kutatua matatizo yanayowakabili Watanzania, suala ambalo litaifanya kupotea katika ramani ya utawala wa nchi.


  "Siku za CCM kukaa madarakani zinahesabika, yaani natamani hata uchaguzi ufanyike kabla ya 2015,"alisema Mtei.


  Mtei ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kukaririwa akisema kwamba, hatua inayofuata katika vita ya ufisadi ndani ya CCM, ni kwa viongozi wa Serikali wa ngazi zote ambao wamekuwa wakikisaliti chama hicho kwa kujifanya miungu watu.


  Kwa mujibu wa Mtei, Chadema ndio chama kitakachochukua nchi baada ya CCM, kwani chama hicho tawala, kinakosa viongozi waadilifu na wanaojali matatizo ya Watanzania.


  Mtei ambaye aliwahi kuwa gavana wa kwanza mzalendo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) nchini, alisema chama imara ni kile chenye sera za kutatua matatizo ya nchi na watu wake na sio "kujivua gamba".


  Alisema kuwa Chadema ni chama imara kwa kuwa kina viongozi waadilifu ambao wako tayari kubuni mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.


  Mtei alisema kitendo cha CCM kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi ikiwa ni pamoja na kuwapa siku 90 wanaweza kutimkia vyama vya siasa huku akisisitiza kuwa Chadema haitakuwa tayari kuwapokea.


  "Chadema hakiwezi kukubali watuhumiwa wa ufisadi, yaani Watanzania wanataka wahukumiwe kwa ufisadi wao leo hii Chadema tuwapokee, hakuna kitu kama hicho, Watanzania wako wengi sana na wanaoingia Chadema wapo pia ila kwa watuhumiwa wa ufisadi hapana, haiwezekani,"alisisitiza
   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hiyo!! We need actually to create our own rules and define our direction siyo kufuata fuata tu kila tunachoambiwa na wabaka rasilimali zetu. Its very sad watu wako busy kujivua gamba badala ya kubuni mikakati kusaidia watu.

  CCM haitakiwi kuwepo madarakani, watz tumevumilia mno hadi sasa na hii inatokana na nidhani yetu ya uoga, umimi na kujiona suala la mageuzi ni la watu fulani fulani. Uzalendo ulishaisha tena, na waliouua ni CCM kwa vitendo vyao ya kutaka kuendelea kutawala kwa nguvu.
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimekusoma mkuu. Ujinga na Uoga unatuponza.:spy:
   
 4. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Saa ya ukombozi imewadia
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  arijojooo afu wao wanajifanya marijalii
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CCM Wana kama hii

  Falsafa ya Chama CDM
  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.

  2.
  Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.


  3.
  Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.

  4.
  Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.


  5.
  CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.

  6.
  CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.

  7.
  Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.

  8.
  Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
   
 7. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  well said, inaelekea, imekuwa ikielekea na itaendelea kuelekea milele na milele amina.
   
 8. z

  zamlock JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ccm mwwisho wao umekaribia tena kama mzee mtei alivyo sema na mimi naunga mkono na mawazo yake kuwa ingekuwa ni vyema uchaguzi ufanyike kabla ya mwaka 2015 ili taifa likombolewe
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndio safari ya Arijojo ya CCM. But be careful with the kick of the dying horse:lalala:
   
 10. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  mtei mmiliki wa kampuni ya chadema wala sio mwanzilishi.

  alipokuwa waziri wa fedha nchi ilifilisika. alishindwa kutekeleza siasa ya ujamaa na kujitegemea.

  ataka kabidhi tanzania mkwe wake mbowe ambaye hata kuongoza familia kumemshinda kichekesho!
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ushauri wa Mtei ulikataliwa akajuzulu na nchi ikaangamia, sasa hapa sijakusoma:frusty:
   
Loading...