CCM ina wenyewe Mwita Mwikabe Waitara

CCM ina wenyewe Mwita Mwikabe Waitara

Hivi unaweza kuwa Mwenyekiti Chadema??
Kwa kuwa chadema wanae mwenyekiti, jibu ni ndio unaweza kuwa mwenyekiti ndio maana wanae. Labda ungeuliza utaratibu wakupata hiyo nafasi ningekwambia hata ungejaza fomu ya uenyekiti ccm (kama ipo) ungeruhusiwa kugombea uenyekiti chadema.
 
Vijana wa sasa wana uroho wa madaraka na tamaa sana za kupata mali kwa haraka. Imefikia sasa mtu yupo tayari hata kuua mwenzie ili tuu apate chochote kama vile yeye ataishi milele.

Kinacho sikitisha zaidi mambo haya yanafanywa na vijana wasomi ambao tulitegemea wangekuwa chachu ya Mabadiliko kwa kizazi hiki.

Chukulia mfano wa huyu jamaa Mwita Waitara. Aliaminiwa na watu wa Ukonga kupitia Chadema akapata Ubunge. Lakini akaachia ngazi na kisha akaomba tena kugombea jimbo lile lile alilo liacha kupitia CCM. Jambo hilo limeondoa kitu inaitwa Credibility yake kwa jamii. Na sasa ameanza kutapatapa akitafuta wapi atagombea mpka akaropoka kuwa anataka kugombea Tarime vijijini akapambane na John Heche wa Chadema.

Dhamira yangu ilikuwa kumuonesha Waitara CCM ina wenyewe. Mara baada bwana Waitara kutangaza nia Chama cha Mapinduzi Mkoani Mara wamesema watamuita ktk kamati ya Maadili kwa kukiuka maadili ya Chama kwa kutangaza kugombea kabla ya muda.

Wakati Waitara anaitwa Kuna kibibi fulani Betina kiko bize kinazurula na Misaraba huko Mbeya na hakuna wa kumghasi. Kile kibibi kinakusanya mpaka Wasanii na kuharibu hadi miundo mbinu ya CCM inayo waingizia pesa uwanja wa Sokoine.

Hakuna wa kumuita ktk kamati ya Maadili bnaa zaidi sana alisikika kiongozi mmoja akilalamika tuu kuwa tumekosa mapato na Mechi ya Yanga na Prison imepelekwa Iringa kutokana na uwanja kuharibiwa tunasikitika sana.

Wanasikitika hawana cha kufanya kwa kibibi kizee kile. Ila kwa Waitara wanaweza tena wamemuita ktk kamati ya Maadili. Hii ndio maana halisi ya CCM ina wenyewe. Vijana Makapuku acheni urofa ninyi CCM inawenyewe ninyi endeleeni kuwashangilia tuu wakipita na Ving'ora vyao eti na wewe unajiita Mwana ccm Damu.

Maendeleo hayana Vyamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mara nyingi ccm wanakuwa na mitego ya aina hii. Wanaanzisha zogo kama mtego na kweli wapinzani wake wanaingia nakuanza kushabikia migogoro yakutengeneza kumbe ccm inaendelea na ratiba zake. Acha wapelekane kamati za maadili hata mahakamani wakipenda hilo ni lao, wasiwaondoe watu katika mstari.
 
Back
Top Bottom