CCM Ina Sababu za Kumhofia Lema

CCM Ina Sababu za Kumhofia Lema

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,298
Reaction score
3,060
Initially Lema was not my bread and butter. But he has earned and now he's won my admiration.

What stands out most is his attitude. Lema is very daring, he's also aggressive (which suits the current war) and of coz he loves his voters. It seems there's a bond with his people which defies the political norms.

CCM wana kila sababu ya kumwogopa Lema, maana hakuna jambo baya ambalo hawajajaribu kumtendea:-

1) Walijaribu kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa ubunge 2010 (hali iliyopelekea kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo na kusababisha taharuki ambayo kama RPC Basilio Matei hakuingilia huenda maafa makubwa yangetokea)
2) Mchakato mzima wa uchaguzi wa Meya wa Arusha na mauaji yaliyofutia
3) Vurugu, dhuluma na hujuma ili kumsababisha asitekeleze majukumu yake ya kibunge jimboni kwake
4) Katika kupinga dhuluma na uonevu dhidi yake na hasa kwa wapiga kura wake Lema "alijotlea" kukaa magereza kwa siku 14. Juhudi za kumsihi atoke gerezani zilfanikiwa kabla ya kipindi hicho kutimia.
5) Lema alibaini na kusimama kidete kupinga hila na njama za madiwani watano walioisaliti CHADEMA na wananchi wao.
6) CCM kupitia Jaji mchumia tumbo wakamvua ubunge ktk mazingira tata na ya aibu
7) Alitumia muda na fursa hiyo kukitumikia chama na hasa vuguvugu la M4C. Kila alikokwenda ameisambratisha CCM na hivyo kumwongezea kujiamini na mbinu zaidi za kisiasa na kiutendaji.
8) Ingawa Lema hakutaka kukata rufaa, alishauriwa na kukubali ushauri wa kukata rufaa na hatimaye tarehe 21 Disemba 2012 alitangazwa kuwa Mbunge halali wa Arusha na Mahakama ya Rufaa.

Hivyo kwa hayo machache Lema haihofii wala kutishwa na CCM kwa lolote, ila kinyume chake ni CCM wanaomhofia Lema. Afanye kazi kwa kipindi kilichobaki maana mchango na uongozi wake unahitajika sana jimboni kwake kwa sasa.

May G-D bless Godbless J. Lema
 
Ni kweli kabisa mkuu Lema ni mpigania ukombozi wa kweli kama ilivyokuwa kwa Nelson Mandela na Steve Bicco. Ni jasiri sana. Long live CHADEMA. Long live Lema
 
Ronal ama kweli umenena kwa kweli you are talented to define people big up!!! Lema kaka kaza buti safari iliyobaki ni fupi mno. Nenda kwanza huko bungeni ututetee sisi wanyonge ambao serikali imetuzalilisha kwa kutuuza pamoja na rasili mali zetu. Uje jimboni kwako uone ufisadi unaofanywa na ccm kwa kuuza ardhi kiholela eti wawekezaji come bro waiting for you!!!
 
kamanda lema kwa sasa ndo kaiva hasa kwa ajili ya mapambano. wanaarusha wote mpeni ushirikiano wa hali ya juu ili atekeleze majukumu yake ya kibunge ili arusha ipate maendeleo zaidi.
 
Mkuu ulikuwa Arusha? au ulifatilia vyombo vya habari...
Umenena kweli mkuu. Hakika mapokezi ya jana ya kamanda Lema amedhibitisha kuwa ni kipenzi cha wana Arusha. Mapokezi yale sijawahi kuyashuhudia kwa kingozi yoyote wa kiasasa tangu nipevuke akili.
 
Kweli Mkuu,
Unajua ingawa niliyamiss mapokezi kiduchu (kwani flight yangu toka Arusha ilikuwa 6am) Ila jamaa anapendwa.
Watanzania wameiva (ripe) kwa ukombozi, CHADEMA wasonge mbele kwa mbele tu
 
Ronal ama kweli umenena kwa kweli you are talented to define people big up!!! Lema kaka kaza buti safari iliyobaki ni fupi mno. Nenda kwanza huko bungeni ututetee sisi wanyonge ambao serikali imetuzalilisha kwa kutuuza pamoja na rasili mali zetu. Uje jimboni kwako uone ufisadi unaofanywa na ccm kwa kuuza ardhi kiholela eti wawekezaji come bro waiting for you!!!

Pamoja mkuu. Kila mtu ana mchango ktk ukombozi wa Tanzania. Kwa hiyo tumia talanta yako mkuu
 
Wanchi kweli tuumpe kamanda ushirikiano wa hali na mali ili aweze kuwafichua hawa mafisadi, ila la zaidi sio kwa wana Arusha tuu tunamwihitaji kote Tz tafadhali awatete watu wote maana ukombozi ni kwa watu wote. Ukiangali taharuki ilikuwa Tz kote kwa watz wote walioko nje na ndani ya nchi. Mimi nilikuwa kazini hapa kwenye nchi za watu ila nilipigiwa simu na mtz mwenzangu, na tuliamua kufunga kazi na kuanza kujiburudisha na watz wenzangu hapa kwa kweli ilikuwa siku ya furaha kama vile tuko nyumbani.
 
Na kuhakikisha hilo leo yuko Mererani kilichotokea huko hakijawahi kutokea...

Niliwahi kukosoa mfumo wa siasa za Lema. Na niliweka bayana kutomfagilia Lema. Lakini kwa jinsi alivyozidi kujipambanua kama Mpiganaji wa kweli, nimejikuta namzimikia na kumfagilia. Hongera zake na namtakia mafanikio katika utumishi wake.
 
Ukweli ni ukweli, Lema ni kiboko.

Natamani sana CCM yangu nayo ingekuwa na mtu kama Lema, kwa sasa imejaa vilaza tu kama Nape na Mwigulu.
 
patamu sana hapo.CCM Lumumba waliingia kichwa kichwa sana A town.A-towners wakaendelea na mambo yao.Mrema ambaye CCM walimboa vibaya anamjua Lema vyema sana.Hawa wajinga wajinga wajinga wengine watasikia sana maneno ya hovyo toka kwa hao madalali wa uwaziri wanaojiiita "wapelelezi" watapiga changa la macho kama akinda ndolanga na issue za kuuza wachezaji nje. Bahti mbaya sana CCM walibugia sana glass kadhaa za mvingo wa Lema sasa ndio pombe inapanda kichwani wakai ikiwa tumboni tele.Wakijihisi inapanda basi wajue itaendelea mpaka ifikie pale mchale ulipasa fika.
 
kuna wanasiasa wasomi sana wanashangaa iweje Lema apendwe kiasi hiki?
 
Initially Lema was not my bread and butter. But he has earned and now he's won my admiration.

What stands out most is his attitude. Lema is very daring, he's also aggressive (which suits the current war) and of coz he loves his voters. It seems there's a bond with his people which defies the political norms.

CCM wana kila sababu ya kumwogopa Lema, maana hakuna jambo baya ambalo hawajajaribu kumtendea:-

1) Walijaribu kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa ubunge 2010 (hali iliyopelekea kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo na kusababisha taharuki ambayo kama RPC Basilio Matei hakuingilia huenda maafa makubwa yangetokea)
2) Mchakato mzima wa uchaguzi wa Meya wa Arusha na mauaji yaliyofutia
3) Vurugu, dhuluma na hujuma ili kumsababisha asitekeleze majukumu yake ya kibunge jimboni kwake
4) Katika kupinga dhuluma na uonevu dhidi yake na hasa kwa wapiga kura wake Lema "alijotlea" kukaa magereza kwa siku 14. Juhudi za kumsihi atoke gerezani zilfanikiwa kabla ya kipindi hicho kutimia.
5) Lema alibaini na kusimama kidete kupinga hila na njama za madiwani watano walioisaliti CHADEMA na wananchi wao.
6) CCM kupitia Jaji mchumia tumbo wakamvua ubunge ktk mazingira tata na ya aibu
7) Alitumia muda na fursa hiyo kukitumikia chama na hasa vuguvugu la M4C. Kila alikokwenda ameisambratisha CCM na hivyo kumwongezea kujiamini na mbinu zaidi za kisiasa na kiutendaji.
8) Ingawa Lema hakutaka kukata rufaa, alishauriwa na kukubali ushauri wa kukata rufaa na hatimaye tarehe 21 Disemba 2012 alitangazwa kuwa Mbunge halali wa Arusha na Mahakama ya Rufaa.

Hivyo kwa hayo machache Lema haihofii wala kutishwa na CCM kwa lolote, ila kinyume chake ni CCM wanaomhofia Lema. Afanye kazi kwa kipindi kilichobaki maana mchango na uongozi wake unahitajika sana jimboni kwake kwa sasa.

May G-D bless Godbless J. Lema
Jamani mbona mnampandisha Zitto blood pressure. Katika watu ambao anaomba waanguke kisiasa ni Lema. Ndio maana alijitahidi sana kwenye ule mgogoro wa madiwani ili amwangushe. Tatizo Zitto ni mtu mwenye wivu sana sana sana na hataki aone mwanasiasa mwingine wa Chadema anasifiwa. Anataka yeye tu ndio aonekane. Hivyo anapoona kina Dr Slaa, Mnyika, Lema nk wakipanda chati roho yake huugulia sana...
 
Umenena kweli mkuu. Hakika mapokezi ya jana ya kamanda Lema amedhibitisha kuwa ni kipenzi cha wana Arusha. Mapokezi yale sijawahi kuyashuhudia kwa kingozi yoyote wa kiasasa tangu nipevuke akili.
wenyeji waliokuwepo wanasema alipokaribia phillips umati ulikuwa mkubwa ghafla .Wanasema ni clinton tuu aliwahi vuta watu kiasi kile. Akina mama waunza mboga mboga waliomtukana batilda na kumrushia nyanya hawakuamini macho yao, nasikia waliselebuka mbaya kwa vile walijua jamaa ambaye anaowaweza migambo na askari koko wanaojihudumia vitu vy akina mama na kuwadhalilisha kijinsia keshakuja.Wameona mji katika taswira ya ushindi wa FREEDOM.
 
Back
Top Bottom