CCM ina rekodi ya utekelezaji 2005 - 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ina rekodi ya utekelezaji 2005 - 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pundamilia07, Sep 22, 2010.

 1. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Yafuatayo ni machache kati ya mengi ambayo CCM na serikali yake iliahidi 2005 kwa wananchi na imetimiza.

  AHADI: KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA

  Ujenzi wa miradi 15 ya barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa
  Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010 huku ujenzi ambao
  unaendelea ukiwa ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4

  AHADI: KUONGEZA BAJETI YA KILIMO NA KUKUZA SEKTA YA VIWANDA

  Bajeti ya sekta ya kilimo imeongezeka kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005
  hadi asilimia 7.9 mwaka 2010 huku ukuaji wa sekta ya viwanda ukiongezeka kutoka asilimia 8.4 mwaka 2005 hadi asilimia 9.9 mwaka 2008.

  Idadi ya wakulima wanaopata mbolea ya ruzuku imeongezeka kutoka wakulima 750,000 mwaka 2005/2006 hadi 2,076,710 mwaka 2009/2010 huku bajeti ya ruzuku ya pembejeo ikiongezeka kutoka bilioni 7.5 hadi bilioni 101.4 katika kipindi hicho cha miaka mitano.

  Idadi ya wataalamu wa ugani walioajiriwa katika halmashauri imeongezeka kutoka wataalamu 3,379 mwaka 2007/2008 hadi 4,439 mwaka 2009/2010.

  AHADI: KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

  Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini Tanzania waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000mwaka 2009/2010.

  Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo vikuu 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo 31 mwaka 2010.

  Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kina wanafunzi 17,282

  Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 493,636 hadi 999,070 huku idadi ya wanafunzi wanaogharamiwa na serikali toka familia zenye kipato duni ikiongezeka toka 16,345 hadi 58,843. Ongezeko hili ni kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2009.

  Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 hadi wanafunzi 889,363.


  AHADI: KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

  Kutoka mwaka 2005 hadi 2009,jumla ya zahanati 464,vituo vya afya 98 na nyumba za waganga 394 zilijengwa. Zahanati 1,037 vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.

  Vifo vya watoto wachanga vimepungua hadi kufikia 58 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai mwaka 2009/2010.

  AHADI: KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA ZA MAJI

  Huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa vijijini hapa nchini imeongezeka kutoka asilimia 58.7 mwaka 2005 hadi asilimia 60.1 mwaka 2009.

  Fedha katika Mifuko ya maji zimeongezeka kutoka Sh bilioni 1.4 mwaka 2005 /2006 hadi bilioni 1.8 mwaka 2009/2010.

  AHADI: KUBORESHA MASUALA YA KIJINSIA

  Nafasi za wanawake katika ngazi ya maamuzi zimeongezeka kutoka asilimia 26 mwaka 2005 hadi 31 mwaka 2010.

  Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko! CCM inapanda mbegu ya maendeleo, amani na utulivu.
   
 2. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa, sisiemu imefanya mambo mengi sana kutekeleza ahadi zake. Kwa takwimu zaidi, unaweza kupitia katika kiungo hiki hapa.

  Kidumu Chama cha Mapinduzi
   
 3. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  KIONGOZI BWM Vs JK

  MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009
  Unga 460 Vs 1000 = 217%
  Mchele 600 Vs 1200 = 200%
  Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
  Mkate 250 Vs 700 = 280%
  Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
  Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
  Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
  Nazi 100 Vs 550 = 550%
  Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%
   
 4. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata hivyo: Chagua DR. SLAA,

  SISIEM inakumbatia ufisadi. JK anamlambalamba Lowasa leo hii!! hivi wewe uliyeleta hii thred inaingia hii kichwani mwako?

  :A S 100:tunakwenda wapi?

  Hatuwezi kuwa tunaendelea kuongozwa na "WASANII" wanaotuchezea kama vile sisi ni vitoto vidogo!
   
 5. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Unaweza kuwa na rekodi ya utekelezaji ndio lakini unatakiwa ujiulize vile vile

  1. Ni kwa kasi inayostahili? - Jilinganishe na nchi jirani au nchi tulizokuwa kwenye uchumi sawa
  2. Haiwezekani kuwa makubwa zaidi yanaweza/yangeweza kufanya? - Hapa tatizo linaweza kuwa watu(watekelezaji) au mipango yenyewe inapangwa hovyo

  etc ....wengine wanaweza kuongeza....
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Kama watetezi wa CCM wangekuwa objective kama mkuu Pundamilia07 basi ingekuwa inanoga kweli kweli... Kudos mkuu!
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Moja ya ahadi kuu za CCM iliyo chakachuliwa na kuwa:

  "Nitasema uongo daima, fitina kwangu ujiko"

  Mbegu zilipandwa na waasisi wa CCM, miche ikachomoza na kutoa majani. Waasisi wameondoka tu, majambazi yamejazana na kuanza kukata matawi, mashina na hata kubugia mbegu hizi za amani na utulivu.

  Pamoja tuing'oe mijambazi hii ili mti huu wa mema kwa Taifa uendelee kukua hata kuzaa matunda ya kulisha Watanzania wote badala ya "royal families" chache zilizo jitokeza!!

  Btw, Mkuu Pundamilia, karibu tena jamvini. Ulipotea mwenyewe sikuamini kama uchaguzi ungepita bila wewe kujitokeza.

  Kula CCM, Kura Slaa!!
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hali imezidi kuwa mbaya kwa CCM kwani majeshi mapya ya kukodi ya Agosti na Septemba ya akina Malaria Sugu, Tandaleone, Jey Key, yaya na wengineo yamezidi kueelemewa na imebidi kuita majeshi ya zamani ya reserve - enter Pundamilia na bado ! Hata familia nayo imebidi iingie vitani baada ya kutokuwa na imani na wanamtandao - duh, safari hii kazi kweli kweli.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Yaani mwaka huu nyoka ameamua kutoka pangoni. Siku za kuchukulia mambo ni business as usual zimeshapitwa na wakati.
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Recruitment ya troops wapya imeanza kusuasua, sasa wameaamua ku-deploy reserves na retirees!!! lol
   
 11. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ahsante sana kwa link yako. Hata hivyo post yangu imelenga kuelezea baadhi yale ambayo serikali ili ahidi kufanya ndani ya kipindi cha 2005 - 2010.

  Pili, hii forum ni ya watu wenye mitazamo, uelewa na maono tofauti. Vema basi tukaweka articles ambazo pia zita balance mada ndani ya forum.

  Kukataa moja kwa moja kwamba serikali ya awamu ya nne haijafanya kitu ni kusema uongo na ndiyo maana nikawakumbusha wengi wenu humu ambao in one way or another mnaifahamu kwa vitendo ahadi ya 8 ya CCM; NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO.

  Lastly, hiyo blog inawakilisha mawazo binafsi kwani composition yake ni kwa yale mambo ya upande mmoja bila ya kuelezea mafanikio ni yapi ili wasomaji waweze kupima utendaji wa serikali.

  Ninakubaliana na mashabiki wa vyama vya siasa kutaka vyama vyao vishinde, lakini kwa CCM haina kitu muhimu cha kujivunia kama rekodi ya yale iliyoyatekeleza katika kipindi cha 2005 - 2010.
   
 12. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nimependa ulivyoongea kwa namba lakini hebu jaribu kwenda some extra miles na kujiuliza maswali kadhaa.

  Katika context hiyo hiyo linganisha kati ya awamu ya pili na ya tatu; ya kwanza na ya pili. Nenda mbali kidogo fanya utafiti katika kipindi hicho katika nchi za majira zetu, halafu changanua uone je bei za bidhaa kwa vipindi hivyo except cha awamu ya 4 zilikuwa zikipungua kwa kiwango gani au kama ziliongezeka ni kwa kiwango gani. Don't forget kuangalia other factors kama uzalishaji, ukame, na nyingine kama hizo.

  Nadhani ukifanya hivyo utakuwa na upana mkubwa wa kujenga na kuboresha hoja yako. Kwa sasa hivi hoja yako bado ni nyepesi sana.

  Otherwise umeanza vizuri hoja, nakupongeza.
   
 13. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu umeanza vizuri sana tena sana tu kwa kusema chagua mgombea wako.

  Lakini yaliyofuatia ni tofauti na ulichotakiwa kufanya nacho nikutueleza kwanini unamwombea kura huyu mwanaCCM wa zamani. Aidha kitendo cha kuanza kuongelea masuala ya JK na serikali yake na kusahau kueleza kwanini si mgombea wako, haikusaidii wewe wala huyo unaempigia debe.

  Chagua Kikwete, Chagua CCM kwa maendeleo ya taifa lako.
  Kikwete na serikali yake wana rekodi nzuri ya kiutendaji na utekelezaji.
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Upande wa pili wa CCM na Serikali yake je?
   
 15. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  deny_all

  I agree with you kuwa katika utekelezaji wa jambo lolote vikwazo ni sehemu ya changamoto kwani mambo haya yanafanywa na binadamu.

  Mimi nimejitahidi kusema kuwa serikali ya CCM imefanya mambo kadhaa na kuweka takwimu. Sasa unapokuja na hoja ya kupinga, kanuni kuu ya kukataa takwimu ni kuja na takwimu nyingine zitakazo weka nguvu kwenye hoja hiyo.

  Otherwise nitaona hukujitayarisha kujibu hoja zangu. Ninakushauri omba msaada kwa watu wa CHADEMA wakusaidie kupata takwimu then njoo ujenge hoja yako.
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Thanks Mkuu for your compliments

  Ninapenda sana kukaa hapa jukwaani na kuchangia lakini, wakati mwingine (kwa mtazamo wangu) naona kuwa tunaishia kubishana bila ya tija. Ikifika hapo ninajiengue ninaendelea shughuli nyingine. Na hili si mimi tu ninaefanya hivi wapo wengi pia.

  Baadhi yetu tunadhani kupinga kila kitu hapa kwenye forum ndiyo ushindi wa vyama vyetu, la hasha, ushindi utatokana wapiga kura wamekuelewa nini hata kama unaongea sana at the end of the day box la kura litaamua.

  Kuwa objective na kumheshimu kila mtoa mchango humu ni muhimu sana.
   
 17. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Steve Dii
  Ahsante sana Mkuu, ninapenda kuwa hapa lakini unajua tena masuala mazima ya demokrasia unapoona kuwa hupati tija basi unaamua kufanya jambo jingine.

  Lakini kipindi hiki cha uchaguzi ni kipindi nyeti sana, kwahiyo walau mara moja kwa miaka mitano nitaweza kuingia hapa na kujadili mawili matatu.

  Kikubwa zaidi kwetu sisi watanzania na hasa wapiga kura tunatakiwa kuwa makini na wagombea na sera zao, lakini kikubwa zaidi ni uwezo wa wagombea hao katika kuelezea yale sera za vyama vyao na rekodi ya utendaji. Kwangu previous rekodi ndiyo mhimili mkuu wa wapiga kura kwani hicho ndiyo kipimo cha kuelezea uwezo wa kiongozi na serikali yake. Kuonesha kuwa hayo ni muhimu basi nilitafuta data ambazo zitanisaidia kujenga hoja baada ya kuridhika na utendaji wa mgombea wa CCM Mh Jakaya Kikwete.

  Kwahiyo jakaya na CCM wanahitaji kura zote za ndiyo ili waendelee kutuletea maendeleo.
   
 18. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #18
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masikini wameongezeka kwa kasi zaidi, mishahara na marupurupu ya viongozi wa serikali imeongezeka kwa ari zaidi, mfumuko wa bei umekuwa kwa nguvu zaidi
   
 19. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mag3
  Habari za siku nyingi ndugu yangu?

  Ni kweli siku nyingi sijaonekana kwa sababu mbalimbali ikiwemo zingine nimezitaja hapo juu.

  Hiki kipindi ni cha uchaguzi, na kazi kubwa kwetu sisi CCM ni kuhakikisha kuwa tunashinda uchaguzi huu kwa kishindo kabisa kudhirisha kuwa 'we mean it' inapokuja katika ushindani wa kisiasa. Delpoyment ya wapiganaji wakati wa vita hasa reserves ni kitu cha kawaida. Kwa mfano hapo Dar pekee kama ulimsikia Mh Kinana Meneja wa kampeni, kuna wapiganaji wasiopungua 15,000 ambao wanafanya kazi za uchaguzi za CCM. Kwahiyo unaponiuona nipo hapa ni wazi kabisa ninaridhikana kazi inayoendelea kwenye battle field.

  Ushindi ni lazima
   
 20. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  We mean business Ndahani,

  Wakati Mgombea wetu akihutubia pale Lumumba alituasa tusiwadharau wapinzani. Yale yalikuwa maelekezo halali ya kamanda mkuu. Na akasema wakati wote tujenge jeshi kubwa zaidi ya lile wapinzani wetu. kazi inakwenda vizuri sana na ndiyo maana niko hapa nikiwa na furaha sana kukuhimiza wewe na wengine msisahau kupiga kura (kama ni mpiga kura) hapo Oktoba 31.
  Nenda kapige kura umchague kiongozi unaemtaka.
   
Loading...