CCM ina Miaka 32 na siyo 50!

nani anaweza kunieleza baada ya kuzaliwa kwa tanzania na ccm nini kilibadilika mbali ya majina.hapa tunazungumzia miaka 50 ya utumwa wa ccm samahani uhuru.

Au tuseme una gari Toyota halafu ukatoa engine yake ukaweka engine ya Nissan, je gari hiyo ikitembea mtaani utaiita Toyota au Nissan? je uta update card ya gari au la?
 
Au tuseme una gari Toyota halafu ukatoa engine yake ukaweka engine ya Nissan, je gari hiyo ikitembea mtaani utaiita Toyota au Nissan? je uta update card ya gari au la?

Hapa gari imebadilishwa kila kitu, kitu pekee kilichobakia ni Number Plate!!

Kwa bahati mbaya sana kwenye maisha ya nchi yetu hii kuna mambo mawili yalitokea yanashabihiana lakini hayafanani kabisa kama tui la nazi na maziwa vinavyoshabihiana lakini hafifanani.

Kwanza kuna Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, na miaka 13 baadaye vyama vilivyoziongoza hizi nchi mbili kupata uhuru wake vikaungana na kuunda Chama kimoja, CCM. Kabla ya 1977 kulikuwa hakuna CCM bali kulikuwa na TANU na ASP kama vyama pekee kwa Zanzibar na Tanzania bara (Usiniulize kwa nini inaitwa hivyo).

kwa hiyo Uhuru wa Tanganyika hauhusiani na Mapinduzi ya Zanzibar na wala si TANU au ASP kimojawapo kilizaa kingine. Hivi vyama kila kimoja kina Historia yake kwenye mapambano dhidi ya Ukoloni na historia hizo hazichangamani. TANU kilikuwa ni chama Pekee Tanganyika kama kilivyokuwa kwa ASP kwa Zanzibar.

Kama ilivyo kwa wanadamu huwezi kuhesabu umri wa mtoto kwa kuchanganya na ule wa wazazi wake ndivyo ilivyo kwa CCM. Kama tunataka kuhesabau umri kwa CCM kwa kigezo cha Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 tunayaachaje Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964? Kama sote tutakubaliana kwamba CCM ilizaliwa mwaka 1977, basi nadhani itakuwa rahisi kuchunguza ni kwa nini vyama hivi havikuungana mwaka 1964 wakati nchi hizi mbili za Tanganyika na Zanzibar zilipoungana.

Hapo pia tutaweza kujua ni kwa nini mwaka huo wa 1977 ASP walikubali chama chao kufa na kuzaliwa kwa CCM yenye mfumo mmoja wa kitaifa, wakati mwaka 1964 walikataa nchi yao "kufa" ili izaliwe Tanzania yenye serikali moja. Hatua moja ya kuupata ukweli ni kuukubali ukweli, na katika hili ukweli ni huu, CCM ina miaka 34 tangu ianzishwe na wala si miaka 50 kama wengi wetu tunavyosema.
 
Back
Top Bottom