CCM ina gundu gani?

Ni mtazamo pia lakini uliokwepa kabisa kujadili kilichomo kwenye mada kuu...inawezekana hukuona umuhimu wa kukijadili au uliamua kuhamisha goli...
 
[emoji38] [emoji38] mkasahau baada ya uzinduzi wa juzi mada iligeukaikawa TBCCM wafukuzwa kwenyemkutani.
 
Si ndo neema yenyewe upande wa pili?
 
Laana
Iaana inawatafuna
 
Achana na Sera za chadema hapa tunajadili matukio ua hovyo kwenye mikutano ya CCM.
 
Alaaniwe mwasisi wa uharamia wa kuwapoka wapiga kura haki yao ya Kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka,yamkute mabaya hata tarehe 28/10/2020 asifike.
 
Mkuu, haya mambo yako juu sana ya upeo kwa wavivu wa kufikiri na wasio na "macho" yenye kuona.
 
Mkuu, haya mambo yako juu sana ya upeo kwa wavivu wa kufikiri na wasio na "macho" yenye kuona.
 
Tukutane october, wacheni longolongo!View attachment 1552613
SISI SIO WAJINGA

Ulipochukua tu madaraka ukaanza na kubomoa nyumba zetu ktk bonde la Msimbazi. Bila huruma ukatuacha tumelala nje na watoto wetu. Ulidhani tutahama mjini lkn sisi bado tupo.

SISI SIO WAJINGA
Ulipokuwa unapanua barabara ya Ubungo - Kibaha ukabomoa nyumba zetu. Mbunge wetu Mnyika aliomba utulipe fidia ukampinga mbele yetu. Lengo lako tufe masikini lkn kwetu sisi maisha yanaendelea.

SISI SIO WAJINGA
Baada ya kuwa tumefanya kazi kwa miaka 40 na tumebakiza miezi 3 tustaafu ukatufukuza kazi kwa kisingizio cha vyeti feki. Ulidhani tutakufa kwa njaa lkn Mungu anatupigani bado tunaishi.

SISI SIO WAJINGA
Tulipopata tetemeko la ardhi Watanzania wenzetu walituchangia pesa nyingi lkn wajanja wakatafuna. Ulipokuja Bukoba tulidhani utatutetea wanyonge badala yake ukatusimanga na kutukumbusha majanga ya Ukimwi, MV Bukoba kwamba yote yanatupiga sisi. Sasa nasikia unakuja kuomba kura kwetu! Je, ni kweli ww utakanyaga Bukoba?

SISI SIO WAJINGA
Tukaenda Mtwara kulima korosho. Ukatuma askari wako wakatunyang'anya korosho halafu wakadai tuwaonyeshe mashamba yetu. Mbona wanaolima mahindi, pamba, mpunga, n.k.hamuwaulizi mashamba yao? Ukasema hao askari watabangua korosho kwa meno ili kila Mtanzania atapata 2kg, lkn hatujapata mgao. Sasa nasikia unakuja kuomba kura! Landa uishie Nangurukuru kwa sababu SISI SIO WAJINGA.
 
Wanaoshiriki kampeni za chadema ni watu wahusika wa eneo hilo,hawaendi vijiji vya jirani kubeba watu kwa malori,mkutano wa chadema hauna waigizaji ni mkutano wa kigumu na wagumu
Mtu ana miaka zaidi ya 5 hajawahi toka wilaya moja kwenda nyingine au hajawahi fika mjini leo umekuja usafiri wa bure kwanin asiende kuona taa za dodoma, na wengi wanakuja kwa akiri hiyo.
 
Binafsi nilikuwa najua Lissu ataleta upinzani mkubwa zaidi ya ule wa 2015 kwa JPM mwaka huu, lakini baada ya kufuatilia kampeni zake.

Duuh, hata kumtetea JPM nimeacha maana napoteza muda tu. Atashinda hata Lissu akihesabu kura mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…