Najua humu JF kuna wasomi wengi tu...je, ni kweli tumefanywa watumwa na CCM kama anavyodai huyu jamaa? Au ni mtazamo finyu?
MWANASIASA mkongwe nchini, Musobi Mgeni ameibuka na kukishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuwafanya wasomi kuwa ni watumwa....je, ni kweli tumefanywa watumwa na CCM kama anavyodai huyu jamaa? Au ni mtazamo finyu?
Tatizo huyo jamaa naye hajitambui kuwa naye si mwelewa. Kunatofauti kubwa kati ya msomi na mwelewa, mtu anaweza kusoma sana na akawa msomi somi lakini asielewe.
Tatizo la TZ na mimi hakika nikiwemo tumesoma vitabu na tumepta shule lakini uelewa sasa ndio mbinde ,sisi sio walewa ndivyo tulivyo na huyo jamaa akiwemo pia.
Mkuu wewe je ni Mwelewa? ama ndo wale wale watumwa?
Usikurupuke rudia tena kusoma nini nimeandika.Sisi tuna matatizo sana
Tulia Mtumwa!
TMtaisingizia sana ccm lakini tuna matatizo sana,kama mkuu umejibu bila kuelewa hapo unafikiri mambo magumu utaelewa??
Response ya Kitumwa tumwa hii......jaribu kuwa mwelewa kaka....achana na hilo jinamizi CCM
Sidhani kama CCM imewafanya wasomi kuwa watumwa ila wasomi wenyewe ndio wamejifanya kuwa watumwa,woga na magoigoi. Wasioogopa tumewaona na waliochoka kufanywa watumwa tunawaona ,wakiikimbia CCM. Wasomi hawa wanatumika katika kuendeleza dhulma ,wapo wanaotumia maneno mazuri katika kuwalaghai wapiga kura na wapo pia wanaotumia vishindo na vitisho ,wote hawa wamesahau walipotoka baada ya kuonjeshwa utamu wa madaraka ya kibabe.
Tulia mtumwa MkamaP😀Tulia Mtumwa!
ni kweli tumeshindwa kujitambua pamoja na usomi wetuu ila kwa kiasi kikubwa mfumo wa utawala ulisaidia kutufanya kutokujitambuaa..Mimi nadhani ametumia maneno mazito sana, ingawa kuna ukweli wa aina fulani katika aliyoongea, ukweli mkubwa unabaki palepale kuwa wasomi wetu wamejigeuza wenyewe kuwa watumwa nchini mwao kwa kutokutumia usomi na shahada zao vizuri na badala yake kuwa wanakimbiza mlio wa shilingi popote uliapo!
Na kwa hilo huwezi ilaumu CCM bali wasomi wenyewe kukubali kuwa watumwa.
Naona itakuwa haku tukisema wasomi wamepeleka kwenye utumwa wa CCM. Si haki kuilaumu CCM kwa kila kitu, mbona Dr Mkumbo hayuko CCM. Nakumbuka kuna siku Shivji alikuwa anawaasa sana maprof wenzake kuwa wasiingie kwenye mchezo huo wa kujichafua na kuharibu sifa yao. Mmoja anaitwa Baregu alimtukana sana Shivji, lakini baadaye ikajaonekana alichosema Shivji ni kweli, Baregu sasa hivi hata akitaka kujiunga na chama chohcote ataonekana hana maana labsa ccm tu.
Respect Mkuu, nashukuru kwa kuni update. Naona na yeye amegundua kuwa NCCR ni tawi la kisiasa la UWT.Mbona Baregu ni memba wa Chadema! fanya utafiti kabla ya kupost mambo hapa!
Tatizo huyo jamaa naye hajitambui kuwa naye si mwelewa. Kunatofauti kubwa kati ya msomi na mwelewa, mtu anaweza kusoma sana na akawa msomi somi lakini asielewe.
Tatizo la TZ na mimi hakika nikiwemo tumesoma vitabu na tumepta shule lakini uelewa sasa ndio mbinde ,sisi sio walewa ndivyo tulivyo na huyo jamaa akiwemo pia.