CCM imeua utaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM imeua utaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 12, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Makundi ya vijana tuyaonayo sasa chanzo chake ni TANU ambayo ilikuwa na kundi la vijana wa TANUuthrigi, na enzi hizo kama hujajiunga na umoja huo ilikuwa vigumu mtu kupata ajira. Hali kadhalika kulikuwa na Umojua wa wanawake Tanzania, lakini leo naona kuna msisitizo wa umoja wa wanawake kila chama. Bado tu umoja wa wanaume wa kichama.

  Mtiririko huu wa split kwa misingi ya chama ndio kuzaliwa kwa watu kuishi kimatabaka, na kabisa mfumo wa vyama vingi ulipoanza basi kila kilichowezekana kikatekwa na CCM kama ilivyo viwanja vya michezo, majengo mbalimbali na kadhalika.
  Tukiendelea na hali hii tutafika wapi?

  Vyama vya siasa ni itikadi si mgawanyiko wa watu, na kwa misingii hii ya kugawa watu kwa itikadi za kisiasa ni kuchafua hali ya hewa kitaifa na matokea yake tunashuhudia maafa ambayo yakitendwa na vyombo vya dola vinatafsiriwa na serikali kama kuthibiti uchochezi wa uvunjaji wa amani. Hawa vijana wanalinda nini kwenye vyama wakati tuna vyombo vya ulinzi? Sipingi vijana kuwa wafuasi wa itikadi za vyama lakini hii ya kuwafanya vijana wanamgambo katika vyama vya siasa inachochea mgawanyiko wa kitaifa.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Candid Scope,

  Ni kweli kbisa kwa kauli hii na badala yake hii CCM Fotokopi hivi sasa imetuletea tu U-MIMI kote nchini. Na hapo ndipo mlango wa kaburi la CCM lilipo tena!!!

  Safari hii Jaji Makame Mwingine akijiingiza huko tume ya uchaguzi na kusaidia kukwapuliwa kwa kura zetu tena basi huyo mtu atakua amesaidia kwa bei nafuu sana kutuua Watanzania kwa zaidi ya robo ya idadi yetu kitaifa; amini ninawaambieni tena juu ya hili!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hakuna utaifa kabisa katika nchi hii
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unapoona mihimuli mikuu inaendesha makujuku kwa misingi ya matabaka ya itikadi za kichama hapo utaifa umesambaratika, kwani vyombo vya umma vinapaswa kuendesha makujuku kwa haki ili kulinda umoja kitaifa.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ningetazamia tuwe na umoja wa vijana Tanzania badala ya umoja wa vija wa vyama vya siasa. Umoja wa vijana wa vyama vya siasa kunaendekeza utengano ndani ya taifa moja.
   
 6. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2013
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakika, tangu leo, CCM siiti tena CCM bali maCCM.

  CCM ya Nyerere ilitetea wanyonge, wakulima, wafanya kazi na wafanyabiashara kwa ujumla. CCM chini ya mwenyekiti wake J. K Nyerere, ilihubiri umoja wa kitaifa, usawa katika utoaji wa elimu (bure). kwa kuwa rasilmali zilitosha kutoa huduma hzo bure, madawa vifaa vya mashuleni na huduma kwa wamama mahospitalini walipewa maziwa ya lactojeni na hata sukari bure kwa ajili ya makuzi bora ya taifa lijalo. Alikemea udini, ukanda ubaguzi wa kirangi, kikabila na kijinsia.

  Ndipo haya yote yalianza kumomonyolewa na makuwadi wa siasa, na mahafidhina yasiyopenda mwelekeo tofauti na ule yanavyowaza.

  Nami tangu sasa nayaita maCCM kwani hayana huruma. Yamehubiri kinyume na mwasisi wao. Ubaguzi wa rangi (S. A. Salim) kuwa ni mwarab maCCM yakamvunjia heshima mzee wa watu. Yakamdharau, hayakukomea hapo ili yaingie madarakani bila woga wowote yakahubiri udini, ilimradi yamepata kura, na sasa udini umeshamiri, ukanda umeshamiri, hata yalidai kiongozi wa nchi hangetoka kaskazini (hakuna aliyekemea hilo), na sasa kuna issue ya wana Mtwara. Je Geita, Mara, Kahama, Mwadui, Kigoma, Kilimanjaro, Tanga nk. nao wakizuia rasilimali za taifa kama Mtwara itakuwaje?

  Kubomoa ni rahisi kuliko kujenga, kazi mnayo maCCM.
   
 7. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2013
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kinachowaponza watanzania ni kuishabikia ccm na kuiweka madarakani kila kunapofanyika uchaguzi!!! Hizo ndizo faida za rushwa ya chumvi, kanga na vikofia vya kijani!!! Endeleeni kulialia!!!
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Candid boresha kidogo ni TANU Youth League. Ila umesomeka.
   
Loading...