CCM imekong'otwa, Polisi mnalala mabwenini

CCM imekong'otwa, Polisi mnalala mabwenini

Losambo

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
2,611
Reaction score
868
Wimbi la wasanii kutoa nyimbo zinazoikandia CCM limeshika kasi baada ya msanii mwingine kutoka Mbeya kutoa remix ya uliokuwa wimbo wake wa dini. Sipendi kuongea mengi ila pateni truck hiyo ina mdundo mzuri na mpangilio mzuri wa mashairi.

CCM safari hii wameshikika.
 
Attachments

Kwan Wimbo Ndo Utapiga Kura?? Hamasishen Wazee Na Kinamama Wawapgie Kura Hasa Vijjn Maana Hao Bado Weng Wao Hawawez Kutenganisha Chama Na Serikali, Tazama Huko Ruvuma Baada Ya Ccm Kufanya Kampen Na Kuzindua Tawi La Chama Wanakjj Wameanza Kujenga Shule Ya Miti! .Je Hko Kuna Wapinzan? Ukawa Wemekaa Kimya Hawataki Kumjibu Makomeo Anaetoa Vitisho Kuwa Tz Itageuka Kuwa Libya Kama Wakichagua Wapinzani!, Na Kwakuwa Vijana Wanaonekana Kuipa Matumaini Upinzani Mkazo Utiliwe Kwa Kinamama Na Wazee Ambao Bado Wanakienz Chama Cha Mapinduzi , Namtumbo, Nangurukulu, Mtwara, Mbinga Handeni, Lushoto, Karema ,korogwe Katavi ,Njombe Tunduru, Kisarawe Haya Ni Baadhi Ya Maeneo Machache Miongoni Mwa Mengi Ambayo Kile Kinachoitwa Mabadiliko Ni Lugha Ya Kigeni Tena Kichina Na Upinzani Maanayake Kwa Waliowengi Ni Vurugu Au Vita!. Kuamini Machifu Nayo Ni Silaha Kwa Baadhi Ya Maeneo Ambao Ccm Huwatumia Kushawishi Wananchi Waichague!
 
Hata Jinga lao la Zari litatoa ya kwake!
 
“Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,malofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
Kwan Wimbo Ndo Utapiga Kura?? Hamasishen Wazee Na Kinamama Wawapgie Kura Hasa Vijjn Maana Hao Bado Weng Wao Hawawez Kutenganisha Chama Na Serikali, Tazama Huko Ruvuma Baada Ya Ccm Kufanya Kampen Na Kuzindua Tawi La Chama Wanakjj Wameanza Kujenga Shule Ya Miti! .Je Hko Kuna Wapinzan? Ukawa Wemekaa Kimya Hawataki Kumjibu Makomeo Anaetoa Vitisho Kuwa Tz Itageuka Kuwa Libya Kama Wakichagua Wapinzani!, Na Kwakuwa Vijana Wanaonekana Kuipa Matumaini Upinzani Mkazo Utiliwe Kwa Kinamama Na Wazee Ambao Bado Wanakienz Chama Cha Mapinduzi , Namtumbo, Nangurukulu, Mtwara, Mbinga Handeni, Lushoto, Karema ,korogwe Katavi ,Njombe Tunduru, Kisarawe Haya Ni Baadhi Ya Maeneo Machache Miongoni Mwa Mengi Ambayo Kile Kinachoitwa Mabadiliko Ni Lugha Ya Kigeni Tena Kichina Na Upinzani Maanayake Kwa Waliowengi Ni Vurugu Au Vita!. Kuamini Machifu Nayo Ni Silaha Kwa Baadhi Ya Maeneo Ambao Ccm Huwatumia Kushawishi Wananchi Waichague!

Wimbo haupigi kura bali unahamasisha kwa sababu muimbaji kagusia mambo mengi ambayo jamii yetu ndiyo inayoyasibu kila siku. Mfano amezungumzia kuhusu kuhusu suala la askari kulala kwenye nyumba mbovu na huku wakitumika n.k

Hivyo wahusika watajikuta wanahamasika kupiga kwa upande watakaoona unafaa ila kwa wimbo huu ni UKAWA.
 
Kurudi madarakani itakuwa ngumu maana wamezoea kurithishana uongozi na kutumia nguvu. Hoja kabisa za nguvu kama za wapinzani wa sasa hawana. Kumbuka watakuwa wapinzani wakati huo, na kuwa na hoja za kurudisha imani kwa watz itakuwa ngumu sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom