CCM imechanganyikiwa?

Mimi binafsi naamini udhalimu huu Mungu hataufumbia macho milele, iko siku wenyewe kwa wenyewe wataanza kunyosheana vidole baada ya mambo kwenda tofauti na matarajio yao, wana wanunua watano au kumi, wenye akili zao timamu 100 au 200 wanaondoka kimyakimya, mmefanya nini! haya yana mwisho tu za watu kama mengine yaliyofikia mwisho. tununueni wote 6m hapo mtakuwa mmeweza.
 
Hivi, hii dhana ya wapinzani kununuliwa (viongozi na wanachama wa upinzani na sio wa CCM) inatokana na ile video ya akina Lema na Nasari?
Na ni kwa nini mnataka watu waamini katika sinema (Kufikirika)? Manataka kutuaminisha kwamba kitendo cha watu kuhama kutoka chama kimoja cha siasa na kwenda kwenye chama kingine (tawala au pinzani) huwa wamenunuliwa? Je, mmeisha jua bei iliyoko mnadani (CCM na CHADEMA)?
Endeleeni kuweweseka na siku mkizinduka mtakuta mmeendelea kubaki wapinzani dhaifu!
Acheni kulalamika! Tafuteni dawa!
 
Tuache vyote ila tukiua vyama vya upinzani ni kuua uchumi ...maana watu watakua wanapiga tu bila hata woga maana hakuna wa kuwasema.
 

Akina Zitto, Kitila, Mwigamba, Kafulila, Msando nk wote walihama enzi za Slaa. Sasa sijui unamaanisha nini kwamba watu wanahama kwakuwa Slaa hayupo. Ni hivi, sasa hivi ccm imeamua kununua wapinzani ili ijenge taswira inakubalika kitu ambacho sio kweli.
 
Huna rafiki ambaye ni Major General? Unamlinganisha Mugabe na Magufuli au ZANU PF na CCM? Vipi, kitumbua kimetiwa mchanga?
 
Kabla ya kufa na kuoza KANU ya Kenya ilinunua kila iliyemhofia akiwemo Raila Odinga huyu unayemfahamu , na akapewa UKATIBU MKUU wa KANU .

Kwahiyo haya yanayotendeka , ni njia ya ccm kufa kibudu .
 
Hakuna ushahidi wa arumeru ni fununu tu na flash.
 
Inawezekana wananunuliwa je hatua gani zinachukuliwa ili wasikubali kununuliwa? Je aina hii ya viongozi wanaonunulika kirahisi kuliko machangudoa wa kona bar inafaa kuongoza nchi yenye rasilimali nyingi kama hii?
 
Hata hapa kwetu kuna ma kabila makubwa mawili yaani ccm na chadema ukipenda mwangaluka na shimboni shafo. CCM hoyeeeee



Vyasaka msituletee upuuzi wenu.

Fanyeni mfanyavyo, ila msituchokoze na siasa zenu za kipuuzi.

Sisi ni wachapa kazi.

Majungu pelekeni kwenu, pumbavu kabisa
 
Hii ni kadi ya mwaka mpya kwa magufail.
 
Ukiona unanunulika ujue upo biasharani hutufai!!
Ukiona unatishika ujue hujakomaa hutufai!!
Ukiona unalaghaika kwa namna yoyote ile ili kuidhohofisha kesho ya taifa hakika bora usingeingia kwenye siasa maana u msaliti ambae adhabu itakukumba tu uwe utawalani au mbadalani!!
 
Inawezekana wananunuliwa je hatua gani zinachukuliwa ili wasikubali kununuliwa? Je aina hii ya viongozi wanaonunulika kirahisi kuliko machangudoa wa kona bar inafaa kuongoza nchi yenye rasilimali nyingi kama hii?
Yaani mpaka leo hujui?
Huwezi kumlinda mtu.

Au hukuona jinsi ilivyotakiwa kuwa na minyororo mikubwa ili kuwadhibiti watu?
 
Very well said
 
Mwenendo wetu kijamii, kisiasa kwa kweli unaacha maswali mengi kuliko majibu. Wale wahenga wenzangu watanielewa pale Mwalimu alivyotuambia kuwa ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, kati ya hayo uongozi bora ni mojawapo. Jinsi tunavyo endelea na maisha ya sasa naona viongozi wetu wamekuwa so impulsive na hawana vision kabisa. Tunachoona sasa hivi ni siasa za maji taka, maigizo na viongozi waliokuwa na unmanageable egos.
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la political prostitution ambapo viongozi waliochaguliwa na wananchi kwa kodi za wananchi wanadiriki kuwaambia wananchi hao hao waliowachagua kuwa wanamuunga mkono kiongozi fulani hivyo kujivua ubunge/udiwani. Dr. Martin Luther King Jr, aliwahi kusema hivi " We need leaders not in love with money but in love with Justice. Not in love with publicity but in love with humanity." Yardstick hii hapa kwetu hakuna wa kuitimiza na hivyo basi future ya taifa letu ni tete.
 
Inawezekana wananunuliwa je hatua gani zinachukuliwa ili wasikubali kununuliwa? Je aina hii ya viongozi wanaonunulika kirahisi kuliko machangudoa wa kona bar inafaa kuongoza nchi yenye rasilimali nyingi kama hii?

Inapokuja kwenye suala la pesa sioni mtu anayemudu kugomea kwenye jamii inayogubikwa na umasikini. Kwa maneno ya mtaani hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Na bahati ccm ambayo ndio mnunuzi wanafahamu vyema kwamba penye udhia ni kupenyeza rupia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…