CCM imeacha siasa inapambana

CCM imeacha siasa inapambana

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Sisi tuliokuwepo enzi za chama kimoja miaka ya 70 tulijionea wenyewe jinsi chama hiki kilivyokuwa na nguvu ya ushawishi kwa wananchama wake kupelekea wananchi kukiamini kuwa mkombozi wao, kulikuwapo watu walioweza kujenga hoja majukwaani (Kolimba) tofauti na sasa ambapo kimeacha siasa za majukwaani za kistaarabu na kuanza siasa za mapambano ya uhasama huku kikitegemea polisi kujibu hoja za wapinzani.

Hii ni hatari sana, kama CCM imeshindwa kufanya siasa tunaomba waiache nchi salama kama walivyoikuta, watambue nchi ni ya watanzania si ya CCM, siasa wanazofanya kamwe hazitawasaidia kubaki madarakani milele sana sana wanaongeza makovu yatakayopelekea ulipizaji kisasi huko mbeleni.
 
Vilipoanza vyama vingi tu CCM ikafa moja kwa moja kisiasa. Tangu 1995 ilianza kutumia mbinu chafu dhidi ya NCCR, 2000 ikatumia dhidi ya CUF ambayo kwasasa ni shoga wake, 2005 ilijaribu kwa CHADEMA lakini ndio ikawa kama imekoleza moto. 2010 Ndio usiseme. Hasa wanahaha kila uchwao maana safari hii ndio Great Depression yao imetimia.
CCM tulikupenda CCM lakini Kuzimu kumekupenda zaidi. Upumzike kwa vurugu mwaka 2015 mahala pabaya Jehanam ya moto.
 
CCM haina cha kuwaambia wananchi waliyokusudia kuwadanganya wananchi yote yameisha, hawana maendeleo ya kujivunia zaidi ya kusema mwaka 1970 tulikuwa na shule 100 sasa tuna shule 2000 bila kueleza miaka hiyo watanzania tulikuwa wangapi kilichobaki ni kutumia maguvu, haitasaidia.
 
waacheni wa angaike sana ila mwisho wa siku watakabidhi ikulu kwa dr slaa bila shida yoyote...na atutalipiza kisasi juu ya haya mnayo fanya ila tutakacho kifanya wale wote walio sababisha mauaji wa raia wasio kuwa na hatia hakika hao tutakula nao sahani moja bila chenga.
 
Vilipoanza vyama vingi tu CCM ikafa moja kwa moja kisiasa. Tangu 1995 ilianza kutumia mbinu chafu dhidi ya NCCR, 2000 ikatumia dhidi ya CUF ambayo kwasasa ni shoga wake, 2005 ilijaribu kwa CHADEMA lakini ndio ikawa kama imekoleza moto. 2010 Ndio usiseme. Hasa wanahaha kila uchwao maana safari hii ndio Great Depression yao imetimia.
CCM tulikupenda CCM lakini Kuzimu kumekupenda zaidi. Upumzike kwa vurugu mwaka 2015 mahala pabaya Jehanam ya moto.

Kwa lugha nyingine hiyo inaitwa PARAPANDA ITALIA PARAPANDA ( rudia mara 4 ) , CC LAWRENCE MASHA ! Maana huo ndiyo wimbo uliomg'oa Nyamagana , Kwi! Kwi! Kwi! Kwi!
 
Mkuu , nilishawahi kupigwa Teke kali sana na Ng'ombe wangu nilipokuwa namkamua Maziwa ! ( just imagine , ng'ombe alitambu uonevu !) Hapo ndipo nilipogundua kwamba hakuna kiumbe kinachoweza kuvumilia uonevu , sembuse binadamu ?
 
Back
Top Bottom