Mzimu wa Kolimba bado waitesa CCM

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Hayati Horace Kolimba, aliyewahi kuwa katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi aliwahi kusema baada ya tafiti zake ndani ya chama chake kuwa chama kimepoteza dira na mwelekeo.

Aliitwa kwenye kikao kujieleza, mauti nayo yakamsogelea na kuiacha dunia baada ya kudondoka ghafla na kukimbizwa hospital alipoaga dunia.

Akiwa mtendaji mkuu wa chama, sidhani kama alifanikiwa kuelezea tatizo lililo pelekea kuiona hali halisi iliyo inyemelea chama chake.

Matokeo yake CCM ya leo badala ya kuhangaikia sababu za kujikwaa ina hangaika na ilipo dondokea.

Hali inayo endelea kwa sasa, kweli mzimu wa Kolimba utaitesa sana CCM, mpaka pale watakapo kubali na kuchunguza kuwa chama hakina dira wala mwelekeo.

Maamuzi ya kamati kuu juu ya wanachama watatu yamewastua wafuatiliaji wa siasa za ndani ya CCM na nje ya CCM.

Chama kimeacha misingi yake na kuruhusu uhuru wa mawazo, hali inayo kigawa chama katika matabaka.

Lipo tabaka la wenye haki zote ndani ya chama, linalo lindwa na vyombo vya dola linalo mlinda M/kiti na fikra zake kuonekana sahihi.

Lipo tabaka la wahanga wa chama, wanao tukana na kudhalilishwa na tabaka la kwanza bila chama kuchukua hatua, hili lina lindwa na wanao itakia mema CCM.

Kwa mpasuko huu CCM haiko salama, ndiyo maana pamoja na katiba yao bado hawaiamini.

Mara ngapi uhuru wa mawazo umefungwa ndani na nje ya chama!!!

Tumeona sakata la korosho lilivyo wanyamazisha wawakilishi/wabunge wa walipa kodi wa nchi hii wakiwamo wakulima wa korosho.

Leo ukitetea wananchi na kusimamia misingi ya haki wewe ni aduia wa CCM-MPYA.

kwa kulijua hilo na kulisimamia, M/kiti wa taifa alimwambia waziri mkuu kuwa, amemuagiza katibu mkuu wa chama angalie wanao pigia kelele korosho, kama watagoma wataanza kwa kuchapwa Shangazi zao then watafukuzwa ndani ya chama kwa kuwa akidi ya wabunge huko bungeni inatosha, hivyo hawatishiki.

Kauli moja ya M/kiti wa CCM - MPYA ilitosha kuwafunga midomo wabunge wa CCM kutoka kusini.

Haikuishia hapo, kwa mara ya kwanza chama kikaasisi utaratibu mpya wa mgongano wa hoja kwa msamaha.

Ndiyo maana kwa hili la Membe kufukuzwa ndani ya chama, wenye akili waliweka akiba ya maneno, tukiamini wakati ni Mwalimu mzuri.

Wapo wanachama waaminifu kwa chama ambao hawakulelewa kwa utaratibu na utamaduni wa uoga ndani ya chama, ambao kwa mfumo huu wamegeuka kuwa majeruhi wa siasa za kihafidhina ndani ya chama, hawa ndiyo wanao angamizwa na lile tabaka la kwanza nililo litaja hapo juu.

Kimanti, kile chama walicho aminishwa kuwa cha wakulima na wafanyakazi sasa kimehodhiwa. Kimekuwa chama - dola, kinacho lindwa na nguvu ya vyombo vya dola kwenye himaya mpya ya kifalme.

Hii haikiweki chama sehemu salama.

Wastaafu wapo kimya, wazee wameficha kichwa chini kama mbuni kiwili wili kipo nje, wamekubali kuandika mafumbo kwa kuwa nafasi yao kwenye chama ni ndogo.

Ndiyo maana leo Tuna ongea nao Lugha moja, demokrasia makini na tume huru.

Hofu, uoga na kujipendekeza kuna igharimu nchi. Na kwa kuwa samaki hujikangaa kwa mafuta yake mwenyewe,sisi yetu macho, hatutachoka kuhubiri injili mpya dhidi ya mfalme Uhihuhi kama mli bahatika kusoma kitabu cha Bulicheka.
 
Back
Top Bottom