Hii nguvu ya Umma waliyonayo wapinzani imetokana na upinzani au inaletwa na CCM?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Uwezi kuwa chama tawala ukashindwa kutawala kwa nguvu ya umma na nguvu ya hoja.

Zipo nguvu tatu muhimu na za msingi katika utawala wa kisiasa ambazo ni
1. Nguvu ya umma- Hii utokana na namna mwanasiasa anavyokubalika na makundi mbalimbali ya jamii anayotaka kuiongoza. Nguvu ya umma udhihirika kwa kuangalia idadi ya wanachama pamoja na idadi wafuasi wanaoweza kukuunga mkono pale unapohitaji wakuunge mkono.

Masharti ya nguvu hii ni kuwafanya watu wakuunge mkono kwa hiari yao bila kuwarubuni au kuwalaghai kwa kutumia uchanga wa elimu, kipato wala nguvu nyingine nyuma ya pazia.

2. Nguvu ya hoja- Uwezo wa mtu kujenga hoja na kuzisimamia kinaweza kuwa kigezo chake kukubalika na watu, hapa ndipo pale usikia watu wakisema huyu nampenda japo si wa chama changu. Wengine usema huyu angehamia chama chetu ningefurahi sana nk. Hawa ni watu wenye nguvu ya hoja zinazovuka mipaka ya itikadi za vyama.

3. Nguvu ya dola- Hii Ni nguvu ya kikundi kidogo Cha watu kwa kutumia madaraka yao uweza kuamua Nani atawale wapi na Nani asitawale wapi. Kiongozi anayetumia nguvu hii mara nyingi Ni yule asiyekuwa na nguvu namba 1-2 hapo juu. Huyu uamini yeye Ni zaidi na mawazo yake tu ndiyo sahihi wakati wote.

Nguvu hii ikitumika kwa kiasi kikubwa umwondolea mtumiaji hata kile kiasi kidogo alichokuwa nacho Cha nguvu ya umma na nguvu ya hoja. Mara nyingi nguvu ya dola inavyoongezeka ndivyo hata wenye dola uanza kuathirika na nguvu hiyo na hivyo kuanza kutafuta upenyo ambao upenyo huo mara nyingi uzaa kuasi aidha moyoni au kuasi adharani.

Nimeeleza hizi nguvu tatu nikiwa na lengo la kujenga hoja ifuatayo:
Kwa namna chama Cha Mapinduzi kilivyokuwa hapo awali na Sasa Ni tofauti, chama kilianza na nguvu ya umma enzi ya Mwalimu hadi mwishoni mwa utawala wa mzee Mwinyi. Mkapa akaingia kwa nguvu ya hoja, umma na wingi wa nguvu ya dola, Kikwete awamu ya kwanza akapata uungwaji mkono mkubwa wa umma ukisaidiwa na dola huku nguvu ya hoja ikiwa hakuna.

Awamu ya pili ya Kikwete akakumbana na kizingiti, akapoteza kwa kiasi kikubwa nguvu ya umma, akakosa kabisa nguvu ya hoja na kusaidiwa kwa kiasi kikubwa na Dola.

Alipoingia Mzee Magu, Mambo yakawa mabaya zaidi, dola ikasimama hadi akaingia Ikulu huku Lowassa akiwa na nguvu kubwa ya umma na wawili Hawa wakiwa na nguvu kidogo sana ya hoja.

Leo tumeingia 2020, nadhani tulidhani miaka mitano ni mingi sana, hatukuona umuhimu wa kurudisha nguvu ya umma tuliyopoteza toka awamu ya pili ya JK, tukajikita kutegemea nguvu ya dola. Uchaguzi umefika ccm wakiwa hawajajiandaa kutumia nguvu ya umma wala nguvu ya dola wakati wenzao hasa CHADEMA na ACT graph zao za nguvu ya Umma na nguvu ya hoja zipo juu na nguvu hizi zinapambanishwa majukwaani. Kujisau kwetu kumepelekea kushtukizwa, hatukuandaa chakusema kwa sababu tulitumia dola tukawachukua wapinzani wengi ambao Leo hii hata wakihitisha mkutano hakuna atakayefika.

Ni vigumu wabunge nchi nzima wawaambie wananchi kuhusu ndege ( wanaojua manufaa ya ndege ni wachache), Ni vigumu wagombea wote waseme kuhusu reli( wanaona treni Ni wale tu wanaopanda na waliokandokando), wanaoona madaraja ya ubungo Ni wale tu ambao hawajui miundombinu kuko nje ipoje nk

Kwa mazingira haya upo umuhimu wa kumwadhibu aliyekishauri chama tawala kufuta majukumu ya kisiasa kwa miaka mitano maana alitengeneza chuki miyoyoni, upo umuhimu wa chama tawala kuwaadhibu wale wote waliokidanganya chama kinunue wabunge na viongozi wa upinzani badala ya kukipa chama mbinu za kupata nguvu ya umma( leo Mashinji alikuwa katibu mkuu wa chama kikuu Cha upinzani na alikuwa anakubalika, karejea CCM amekuwa liability kwa chama na asset kwa familia yake), upo umuhimu wa kumwadhibu katibu mkuu wa Sasa ambaye ameleta elimu ya darasani kwenye siasa na kuwaaminisha watu kuwa ukiwa na dola ukaondoka madarakani wewe ni mjinga. Alishindwa kufahamu kwamba watu hawapo madarakani kwa ajili ya madaraka tu Bali wanakaa madarakani wakiwa na baraka za wanaowaongoza, shinda Uchaguzi kwa nguvu ya dola kama maisha yako yote hautaongoza ukiwaabudu wenye dola.

Nguvu ya umma na nguvu ya hoja yatosha kuingoza Tanzania.
 
Siku zingine unaamuaga tu kwa makusudi kuwa jinga.

Leo umeargue kiweledi na kizalendo na sio kama wale wazalendo feki

Pale lumumba ukiwafundisha wapuuzi akina Bashiru,Kabudi etal wawe na fikra hizi halafu wao in turn wambadilishe jiwe wote tungekuwa upande wake.

Tatizo leo mnashauri mazuri,kesho buku saba isipoingia unarudi hapa kutia mouth diarhea.

At least mnaunga mkono upuuzi kwenye media lakini moyoni mnajua mnazingua.
 
Back
Top Bottom