Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,506
Wakati akimnadi mgombea urais wa CCM, Benjamin Mkapa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alipata kusema, "CCM ni kama kokoro. Linabeba samaki, wakubwa kwa wadogo. Linabeba hata takataka."
Kauli ya Mwl. Nyerere ilitoka baada ya nchi kuingia kwenye mageuzi ya kisiasa na kiuchumi bila kuwepo kwa misingi imara ya kupambana na changamoto za soko huria la kiuchumi na kisiasa.
Mwaka 1925, Mahatma Gandhi aliwahi kuorodhesha Seven Social Sins, mojawapo ilikuwa ni politics without principle. He went on to say having politics without truth(s) to justly dictate the action creates chaos, which ultimately leads to failure and violence.
Kwa kukosekana na misingi imara ya kisiasa, CCM ilijikuta ikivamiwa na wanachama/viongozi ambao wana kila aina ya uchafu na hawana maadili. CCM ilikuwa ni kama mzoga ambao ulikuwa unavuta mainzi na mafisi. Kukaibuka kaulimbiu inayosema; ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri.'
Uchafu wa kisiasa na kukosekana maadili kilipekea kuibuka kwa kikundi kinachojiita wanamtandao (party cartel). Wanamtandao kimsingi kilikuwa ni kikundi ambacho kilikuwa ni chama ndani ya CCM katika msingi wa kupata nguvu na madaraka ya juu nchini kwa njia yoyote.
Kama ilivyo kawaida, Mtandao una maisha mafupi, Mwaka 2012 ilikuwa ni mwanzo wa mwisho wa maisha ya wanamtandao kama party cartel within CCM.
Baada ya uteuzi wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Magufuli, tumeshuhudia kumeguka kwa wanamtandao ambapo pande lingine kwa sasa linatafuta maisha yenye heri ndani ya CHADEMA/UKAWA.
CHADEMA ambayo ilikuwa tofauti na CCM kwa sasa imeanza kuvaa mavazi ya CCM ya mwaka 1995. CHADEMA imeanza kuachana na misingi yake ya kupambana na ufisadi na kwa kufanya hivyo, inakuwa kama mzoga unaovutia mainzi na mafisi ya kisiasa. Kauli mbiu iliyokuwa CCM inayosema ‘Nunua siasa, siasa ikununulie utajiri' kwa sasa imeanza kupata nafasi ndani ya CHADEMA/UKAWA.
Kwa sasa ndani ya CHADEMA/UKAWA hakuna vetting na tunaambiwa mwanachama anayeijiunga leo hana tofauti na yule aliyejiunga miaka 20 iliyopita. unaweza kujiunga leo na kupewa uongozi leo. Dhana ya makapi iliyotolewa na Katibu Mkuu, Dk. Slaa ndani ya CHADEMA sio hoja tena.
Wapiga kura makini nchini kwa sasa wako kwenye limbo. Wapiga kura makini kwa sasa wanakabiliwa na zoezi la kuchagua shetani mzee (CCM) chini ya Magufuli au shetani kijana(CHADEMA/UKAWA) chini ya Lowassa.
Kwa sasa siasa za Tanzania huwezi kuzitofautisha na upuuzi ambao huwezi kuepuka kwenye sanduku la kura!
Kampeni za mwaka huu zitakuwa ni kivutio chenye matokeo yale yale!