Kigongoi kwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2018
- 581
- 696
Wakuu ninaona kwamba kuna haja ya chama cha Mapinduzi,kiwe kimeshinda au kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu kukaa na wapinzani na kushauriana njia sahihi za kufanya chaguzi zetu za kila baada ya miaka mitano .
Hii inakuja baada ya kuona kwamba kikifika kipindi cha uchaguzi kunakuwa na hali ambazo kama taifa zinatufanya tugawanyike na kutengeneza uadui wa kiitikadi.
Kuna haja pia ya kurekebisha katiba kuwe na mfumo shirikishi wa kuongoza serikali kama ilivyokuwa kwa umoja wa kitaifa wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa sababu ni wazi kwamba kuna maeneo ccm inakubalika na pia kuna sehemu ccm haikubaliki kabisa.
Binafsi natamani hoja ya kusema ushindi kwa chama fulani ni lazima isiwepo; hii itatufanya tuendelee kuwa wamoja kuliko kutengeneza uadui, itatusumbua siku za usoni.
Bado nakumbuka maneno ya Rais mstaafu J K wakati wa mchakato wa katiba uliovurugika aliposema kwamba ni bora tukae tujadili mambo yetu tukiwa wamoja kuliko kukaa tukiwa tumevurugana