Ukichunguza hoja za wachangiaji wengi humu hasa wa chama tawala utagundua wanatumia jazba zaidi kuliko ukweli.
Nawashauri waingie youtube wasikilize hotuba za wagombea wote. Waangalie mikutano ya kampeni na mwenendo mzima wa kampeni.
Wasisahau kuwasikiliza makada mbalimbali na hata maafisa wa serikali kuhusiana na uchaguzi. Wasikilize hata na vyombo vya habari vya nje nk.
Baada ya hapo ikiwezekana hata kwenye mikutano ya kampeni japo michache waende kusikiliza.
Watafiti hivi ni watu wa aina gani huudhuria kampeni, wanaendaje, na nini kinawasukuma kwenda.
Ukifanya hivo unaweza kuja na maoni sahihi hapa bila ya hivo itakuwa ni mihemko tu.
Mimi nimefuatilia yote hayo na nimegundua kwamba uchaguzi huu ni mgumu sana na kiukweli kusema hasa nani atashinda ni ile wiki ya mwisho ya kampeni.
Kushinda au kushindwa kwa CCM kutatokana na mgombea wake na sio wana ccm wenyewe. Tena wana ccm na wapambe wa mgombea wanaweza wakamharibia ushindi kwa mbinu wanazotumia sababu nyingine ni ovu na zimejulikana.
Kushinda kwa mgombea wa CDM kutatokana aina ya mgombea wake, uwezo, ujumbe, ujasiri na mvuto wake. Pia kutatokana na makosa yaliyofanywa na ccm na mgombea wake.
Kushindwa kwake kutatokana na uoga na uelewa mdogo wa wananchi wengi ambao hawana habari sahihi na za kutosha, hajajiandikisha na wasiopiga kura. Pia kunaweza kutokana na uminyaji wa haki na uhuru katika mchakato wa uchaguzi.
Ushauri
Kwa ccm wangeachana na hili neno ubeberu halina mashiko yoyote. wajikite zaidi kwenye mafanikio na sera. Pia kuna hoja za upinzani hawajazijibu, wazijibu.
Kwa upande wa cdm wajikite kwenye sera yao ya uhuru, haki na maendeleo ya watu na waendelee kuidadavua in and out kwa mifano. Waachane na kumshambulia mtu bada yake waeleze namna mhusika alivyosababisha mapungufu katika sera yao kuu. Cdm kikubwa pia kuwashawishi vijana wakapige kura.
Kwa sasa issue ni Magufuli vs Lissu vs Magufuli.
WATU WAPASWA KUFAHAMU (Mwl. Nyerere)
Sent from my Nokia 6.1 using
JamiiForums mobile app