CCM ijue kuna tofauti kati ya chama (CCM) na serikali

Nimeshangazwa sana na huyu msemaji wa ccm Ole Sendeka kwa kauli yake "Serikali haijapiga marufuku mikutano ya siasa ila imepiga marufuku maandamano" na kuwaambia madiwani ruksa kufanya mikutano ya maendeleo. Anasema ''hatujazuia mikutano...maandamano marufuku''

Anaongea yale na kutoa matamko yake yeye kama nani? Pia kuna wakati viongozi wa ccm huwa wanatoa ufafanuzi rasmi juu ya maagizo, maamuzi ya serikali na mipango ya serikali, wakati hilo ni jukumu la vyombo husika vya serikali kuyatolea ufafanuzi mambo yake katika idara au mamlaka husika. Mipango ya serikal inaweza kuwa imeanzia ndani ya chama lakin utekelezaji wake na mlolongo wake wote including kulizungumzia linabaki kuwa ni jukumu la chombo husika cha serikali kama ni polisi, wizara, jeshi, tra n.k. Tujifunze kwa wenzetu waliotulea mfumo wa vyama vingi, wenzetu mambo ya chama yanaishia ndani ya mikutano yao ya kichama baada ya hapo serikali inaendelea na mambo yake na utaratibu wake.

CCM karibu wote wanashindwa kutofautisha kati ya serikali na chama, wanashinda kutofautisha mamlaka ya serikali na mamalaka ya chama, wanashindwa kutofautisha mikutano ya serikali na mikutano ya chama, wanashindwa kumtofautisha Raisi na Mwenyekiti wa chama, wanashindwa kutofautisha mali za serikali na mali za chama. Yani hapa ni vurugu tupu. Kila kiongoz wa ccm anajiona na ye ni serikali, yaani ni vurugu tupu.Kuna baadhi ya viongozi wa cmm inafikia wakati wanaliagiza jeshi ya polisi wafanye hili wafanye lile mpaka mtu unakaa na kustaajabu nini nchi hii inafanya.

Hili suala ni la kulaaniwa na vyama vyote, msajili wa vyama, serikali, jeshi la polisi na mwenyekiti wa ccm wakiwa kwenye vikao vyao awaeleze bayana kuwa serikali ni kitu kingine (mchanganyiko wa watumish wa umma plus baadhi ya wanaccm wachache waliopigiwa kura navkuteuliwa) na ccm ni nyingine.
Ndo mana sipendi kusikia kauli ya "hii ni serikali ya ccm", maana inawafanya wanaccm kuwa wehu na kufikiri kwamba wao ndio ndo wenye mamlaka na wana uwezo wa kufanya chochote.

Nawaomba CCM muelewe kuwa, ccm sio serikali bali kuna baadhi ya wanaccm wachache wamechaguliwa na kuteuliwa kuongoza kwenye serikali, hivyo sio kila mwana ccm ni serikali, nukta.

Siku tutakayoanza kutofautisha seriakali na chama, ndio siku tutakayoona faida ya vyama vingi vya siasa na kuelekea wenye maendeleo ya kweli.

Second July.


ha haha ha ha haha ha hahaaaa...

simple!!! ameongea kama Msemaji wa chama chenye serikali madarakani..

Kwani wewe una hoji kama nani??

mnachezea kichapo saa hizi mpaka mmechanganyikiwa!!, mnaacha kupambana na mambo ya msingi mko bize kujadili na semantics..
 
Tatizo vijana hamjui hata nchi hii inaongozwa na chama gani. Hujui kuwa serikali inaongozwa na chama cha mapinduzi? Hukusikia pale Magufuli aliposema wana CCM ni maboss wa watendaji wa serikalini?

Jifunze kujua kwamba serikali ya sasa hivi ni ya CCM nyie ni wapinzani wa serikali ya CCM.

Kwa hiyo Ole Sendeka yupo sahihi.
 
Kuna ugonjwa mbaya Sana umewakumba hao ccm uuitwao mkurupuko. Ugonjwa huu huwapata zaidi wale wote waliojitwalia madaraka bila ridhaa ya watoa Kigali ambao no wananchi. Hivyo hujawa hofu na mihemko ambapo hupelekea kutokujiamini kwani hawapo kihalali na wanajilazimisha kukubalika. Panya na kambale wote huzaliwa na sharubu na huwezi kumtofautisha mkubwa na MDOGO kwani wanafanana. Hapa ninamaanisha kuwa nchi hii huwezi kujua tamko lipi ni LA chama na lipi ni LA serikali. Na ni yupi ni msemaji wa chama na yupi ni wa serikali. Mkurupuko.
 
Back
Top Bottom