MAKULILO
Member
- May 30, 2010
- 84
- 95
Usiwe mgumu wa kuamini kinachoendelea. Tumia mfano mdogo huu, halafu uangalie kauli yako kuwa "upinzani bado sana kuing'oa CCM".
Mwaka 2005, Kikwete alishinda kwa kupata kura 9,123,952 sawa na 80.28%, aliyefuata ni Lipumba (CUF) kwa kura 1,327,125 (11.68%), na watatu ni Mbowe (CHADEMA) kwa kura 668,756 (5.88%)…na wengine kufuatia. Watu waliopiga kura ni 11,365,477 sawa na 72.4% ya wote waliojiandikisha.
Mwaka 2010, Kikwete akiwa rais aliye madarakani, amiri jeshi mkuu, kiongozi mwenye mamlaka yak u-influence matokeo ya uchaguzi, kuteua mkuu wa tume, kuteua watu wenye uwezo wa kumsaidia, na kubwa zaidi hakukuwepo mpasuko ndani ya CCM 2010 kwani kwa utaratibu wao hakuna mtu kumpinga rais akiwa madarakani kama anataka kugombea tena awamu ya pili. Sasa tuangalie matokeo yapoje. Kikwete alipata kura 5,276,827 (62.83%), wa pili ni Dr. Slaa (CHADEMA) kura 2,271,491 (27.05%), na watatu ni Lipimba kwa kura 695,669 (8.28%), na wengine kufuatia.
Sasa jiulize, ilikuaje Kikwete atoke 80.28% hadi 62.82% mwaka 2010? Kumbuka na hiyo 62.82% ni baada ya kuiba kura, kutumia mbinu za madaraka ya kiti cha urais, na kubwa kutokuwepo mpasuko ndani ya chama wakati wa 2010.
Kumbuka 2010, upinzani haukuungana. Walikuwa wanapambana wao kwa wao pia. Miaka yote ya nyuma upinzani haukuweza kuunganisha nguvu.
Sasahivi inakuaje? CCM ina mpasuko mkubwa sana. Kwa mara ya kwanza hata CCM wanahofia kupteza utawala wao. Kwa mara ya kwanza, wapinzani kuungana kwenye chaguzi kuanzia udiwani, ubunge na urais…japo sio vyama vyote, ila vyama vyenye nguvu (kuondoa NLD). Kwa mara ya kwanza, mtu ambaye ni muhimu katika siasa za Tanzania, Lowasa kuondoka chamani…huku akiwa na kambi nzito ndani nan je ya chama.
Kama bado una imani kuwa upinzani hauwezi kuchukua nchi, Kikwete anajua wanaweza. Ndio kwa mara ya kwanza, rais aliye madarakani wa CCM anamsindikiza mgombea urais kuchukua fomu za kugombea urais tume ya uchaguzi. Hali ni mbaya. Kwa mara ya kwanza, wananchi wameenda mbali kuona enough is enough. Matumizi ya internet na social media yameongeza uelewa mkubwa sana tofauti na 2010. Hata ukiangalia mapokezi ya Magufuli vs Wenje umejionea.
Kipindi cha 2010 na miaka ya nyuma, vyama vya upinzani havikuwa na fedha za kutosha na pia serikali ilikuwa inazua baadhi ya vyombo vya habari kurusha habari za upinzani. Sasahivi upinzani wanarusha LIVE mikutano yao yote kama vile CCM nao. Kwa mara ya kwanza, media imetawaliwa na upinzani ambapo kila kinachoendelea upinzani ni hot topic na badala ya CCM. Baada ya CCM kumkata Lowasa, media ikahama na Lowasa atafanya nini. Na kila tukio ambalo lingeipa CCM au magufuli airtime linazimwa na tukio la UKAWA. Mfano Magufuli, Kikwete nk kwenda kuchukua fomu, muda uleule CHADEMA wanarusha live Lowasa kupitishwa. Media zinaangalia kipi cha maana zaidi, kutoa habari za aliyepitishwa au anayepitishwa? Hata Lipumba kuondoka, bado inaongeza watu kuongelea UKAWA kwa namna moja au nyingine. Wenye kuamini kuwa CCM imetumia rushwa nk kumshawishi Lipumba kutoka, wanapata hasira na kusema tutaonana Oktoba, tutawaonesha sisi ni akina nani kwenye kura.
CCM walizoea kuiba kura. Kumbuka, Lowasa ni CCM kwa zaidi ya 30 years. Anajua kila kitu, kila mbinu. Viongozi wengi wa CCM wanakwenda UKAWA. Viongozi wengine wanabaki CCM kuhakikisha wanaiua CCM toka ndani kwa ndani. Mtu kama Bashe ni kambi ya Lowasa inafahamika wazi. Amebakia CCM, unadhani kabakia kufanya nini? CCM haijui nani ni nani ndani ya chama.
Mwisho: Kumbuka Ufaransa alivyoshindwa kutoka kombe la dunia…alipofungwa na Senegal na mechi zake zote. Nani alitegemea Ufansa bingwa wa Kombe la dunia la awali la 1998 na Kombe la Ulaya kuja kuabika vile kuondoka na point 1. Nani aliyejua/dhania kuwa Hispania itaondoka na point moja kombe la dunia? Hispania ambaye alikuwa bingwa wa kombe la dunia la awali na bingwa wa Ulaya, na timu nzito kama ile? Nani aliyejua Brazil inaweza kubamizwa vile?
Kila taasisi, inazaliwa, inakuwa na inakufa. Muda wa CCM umefika. CCM inaondoka sasahivi. Waanze kujiandaa kuwa wapinzani kisaikolojia. Sasahivi sio jukumu la UKAWA tena, hii imebadilika na kuwa MOVEMENT ambapo wananchi wamefikia hali ya kusema ENOUGH. Wananchi wamepata uelewa zaidi. Wananchi wanaamini wana uwezo wa kuiondoa CCM madarakani tofauti na miaka yote. Umejionea kwenye chaguzi za serikali za mitaa, ubunge nk hali ya CCM ilivyokuwa mbaya.
Kinachoendelea sasahivi Tanzania na siasa: Imevuka ile hali ya CCM vs CHADEMA, CCM vs CUF, CCM vs NCCR etc. Sasahivi imebadilika na kuwa MOVEMENT. Wananchi wengi wana wanataka CCM iondoke madarakani. Na kwa mara kwanza katika siasa za Tanzania, uchguzi huu, CCM yenyewe imeona hilo kuwa inaenda kuondolewa. Imevurugwa sana. Na wananchi kila siku wanaona jinsi walivyo na nguvu ya kuiondoa CCM madarakani kwa kura. Watakaopiga kura watakuwa wengi, wengi wameona thamani ya kura zao sasa. Katika MOVEMENT hii, watu wengi wapo hata kupigia kura jiwe dhidi ya CCM. Hata kama UKAWA wakiweka jiwe, watu wengi wamedhamiria kuona CCM inaondoka madarakani, ili ikajifunze upya kama KANU na vyama vingine vya "ukombozi".