- Thread starter
- #41
Hilo hata mie limenishangaza sana. Jee ni kweli maneno ya Makongoro yaliwakilisha mawazo ya familia ya Mwalimu akiwemo mama Maria? Kama ni kweli basi hata ile heshima iliyokuwa anapewa yule Mama haimstahili tena. Ajitokeze na kumkana mwanae kuwa hawakumtuma, vinginevyo hata yeye tutachukulia kuwa hastahili heshima tena sio hapa Tanzania tuu bali hata nje ya nchi.
Najua watu wanaendeshwa na ushabiki wanaweza kuliona hili ni jambo dogo tuu, lakini heshima ya Mwalimu haikupaswa ivunjwe na kizazi hiki alichokiacha kikiwa hai hata kidogo labda wajukuu zake ambao eitha hawakuwepo wakati wa Mwalimu au walikuwa wadogo sana kuweza kumfahamu.
..msimlaumu mama wa watu.
..she is an old lady, she deserves our respect no matter what makongoro is doing in public rallies.
..makongoro ni mtu mzima mwenye mke na watoto.
..kwetu kijijini tunasema makongoro ni mtu mwenye "mji" wake.