GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Wanabodi,Kila binadamu ana mapungufu yake ambayo wewe mwenyewe huwezi kujiona bali wanaokuangalia ndio wenye majibu sahihi juu yako.
Watendaji wa serikali ndio wanaotuangusha chama cha mapinduzi sana,Hawa watendaji wengi hawana elimu ya siasa wao wanafikiria familia na kulinda mishahara yao tu.
Kosa la kwanza,Wakati wa hali tata na katikati ya mapambano,Wanaibuka na kukoleza kutajwa tajwa kwa Tundu Lisu na wananchi,Kukataza matangazo ya BBC,VOA na DW kulikofanywa na waziri Mwakyembe na TCRA kuna jenga chuki kwa wananchi kwa ccm bila sababu za msingi ,Inapelekea lissu kushangiliwa huko Kahama kwa kuwa anatembelea mapungufu ya watendaji kuwa wananchi hamtaona BBC wala DW au VOA.Kuwa kutoonekana BBC, DW na Voa ccm ndio wamefanya hilo na wananchi limewaingia na kushangilia
Kosa la pili,Television ya Taifa yaani TBC sijaelewa kwanini mtendaji wake bado yupo ofisi anatengeneza chuki kwa CCM kuwa wanaogopa hoja za upinzani na wanaficha maovu,Hili ni kosa kubwa sana kimkakati kwa chama ,Ni pyschology ya kawaida hata Nyumbani Baba anapojisifia yeye tu kuwa anawasaidia watoto,Watoto baadae wakigundua ukweli familia nyingi Mababa wanadharaulika sana,Yapasa awe na asilimia katika kuonyesha mambo sio kila siku upande wa ccm tu.Leo hii watu wanadharau television ya Taifa na kuita Tbc ccm, Kila kitu kwenye Tbc wananchi wanachukulia ni uwongo na propaganda, Kuna mambo yamefanyika kweli lakini kuonyesha upande mmoja watu wanasema ni picha za kuchorwa kweli?
Kosa la tatu, Matamko ya Jeshi la polisi hasa watendaji wa juu kwenye mambo ya siasa yanafanya watu kuamini chama cha CCM hakishindi kihalali maeneo mengine bali kwa kubebwa na polisi,Wakati kuna maeneo ccm inashinda kwa uhalali kabisa hata wapinzani wanakubali matokeo.
Ni rahisi sana kuzijibu hoja za Tundu Lissu kisomi majukwaani kama watendaji wa serikali wangetambua chama kinachotawala kinahitaji hoja zenye mashiko.
Hoja za Tundu Lissu sio nyingi sana ,Kama wakati ule hoja za Dkt Slaa zilikuwa zikijibiwa na Nape Nnauye kwa ustadi mkubwa na vijembe vya hapa na pale kwanini leo?
Mosi,Hoja ya uhuru wa habari na kuongea,Hapa TBC na ndugu Mwakyembe walipasa kuwa wajanja wanaonyesha sehemu za mikutano ya Tundu Lisu halafu wanapigilia nondo zao kwa kuonyesha taarifa za Magufuli kuziba mabonde,Bila hivyo watu wanatafuta habari za Tundu lisu kinguvu.
Pili,Hoja za Malalamiko za wafanyakazi , wafanyabiashara na wakulima hapa watendaji walipaswa kuonyesha kitu gani kimefanyika kisheria,Mapungufu walioyaona kwa miaka mitano,Na nini matarajio ,Bora kukili mapungufu na kuahidi kuboresha,Kutokuongelea hili Tundu Lisu anazidi kutembelea udhaifu huu.
Hoja ya upendeleo wa mkoa wa Geita hasa chato ni suala rahisi sana kulijibu ,lakini kitendo cha kuuliza chato ni wapi sio jibu ya hoja hii,Hapa watendaji walipaswa kueleza sababu za kwanini wameweka mbuga au uwanja chato na sababu zipo nyingi za kushawishi Raia wa Mwanza ,Mbeya au Dar es Salaam,Kujibu kirahisi kunazidi kumpa sifa Tundu Lisu.
Chama cha mapinduzi kisiwaonea haya hawa watendaji wa serikali wanaotafuta sifa huku wakiharibu sifa na upendo wa chama kwa wananchi.
Watendaji ndio wasimamizi wa hii miradi na utendaji wa serikali kila siku ndio wa kujibu hizi hoja sio kukimbilia kuzuia hoja na kuzidi kumpa umaarufu Tundu lisu mbele ya wananchi
Watendaji wa serikali huu ulikuwa ndio muda wa kwenda Tbc kufanya mdahalo na watu wa upinzani kwa kuelezea mmejenga shule, Hospital na mm jifunza kitu gani na kitu gani kimebaki kwa miaka mitano ijayo sio kuelezea mafanikio tu wakati kuna mambo dhahiri hayajakamilika kwenye shule au hospital
Mfano mzuri na ambao utadumu,Ni kitendo cha kuwaacha watu huru kumpokea Tundu Lissu airport ,Hakuna fujo wala ugomvi uliotokea watu walishangilia sana na kurudi makwao kulala ,ccm ilichukua sifa kubwa kwa hili kwa wananchi ,Mbinu kama hii ya hamsini kwa hamsini ndio ujanja wenyewe.
Muda huu ndio mtu kama Humprey polepole angeacha vitisho na majigambo bali angekuwa anaitisha mijadala na wanasiasa wa upinzani.
Muda huu ndio ilikuwa unamuita Nape Nnauye kwenye Mdahalo na Halima Mdee wanabishana kwa hoja.
Bila mdahalo wa hoja za pande mbili wananchi wanazidi kuaminishwa ugumu wa maisha umesababishwa na ccm wakati kiuhalisia watendaji ndio wameleta matatizo na chuki kwa wananchi
Wafuatao walipaswa kutenguliwa kwa muda ile kujenga imani na kujitenga nao na chama, ccm ieleze kuwa hawa ndio wamezima bbc, Voa na DW, Pia ieleze kuwa hawa ndio wanaeneza chuki kwa ccm, Yote wanayofanya ccm iwaambie wananchi kuwa ni hawa watendaji na sio chama kinakosea
Mkurugenzi wa Tbc
Mkurugenzi wa TCRA
Mkurugenzi wa idara ya habari Maelezo au Msemaji wa serikali
Tukutane Octoba,