Nimekupata vema Deus, kuna siku niliomba wapenda haki tukutane,ulikuwa miongoni mwa waliochangia ile mada.Ilichangiwa na watu 150,waliotumia vichwa na vifua kuchangia hawakuzidi watano, wengine wengi walitumia viuno,kutumia kichwa, kifua na kiuno ni jambo la kifalsafa,nadhani unanielewa.Wengi watashabikia cdm hadi siku ya uchaguzi,baada ya matokeo ya dhuluma wanafanya nini.Watz wengi wamebaki kulalamika tu bila kuchukua hatua,ccm ya sasa sio ya kulalamikia tu, inahitaji vifua vikiongozwa na vichwa.Deus mimi na wewe tunaelewa kuwa haki haiombwi bali inadaiwa na kupiganiwa,katika haya mawili ya mwisho ni watz wangapi wanaweza kufanya hivyo. Katika vurugu za uchaguzi kenya uliweza kuona hata wanawake wanapigania haki,hapa kwetu ccm kwa vitisho tu vya kawaida wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwazuia akina mama kuhudhuria mikutano ya cdm,hawa watadai haki yao kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa?Mkuu umefanya Uchambuzi Mzuri sana, kwa kuongezea machache ni kwamba;Ikumbukwe kuwa kuna walioapa kuilinda Serikali ya CCM kufa na kupona,Hawa wana uhakika wa kwenda Lunch Marekani na Dinner wakaenda Swiss kabla ya Kwenda London Kulala.. Hawa wana watoto wao wanaosoma huko huko ambao hawakuwahi kusikia njaa tangu kuzaliwa kwao.. Ama hao watoto wana watoto wao ambao wanataka nao wakija kuwa na watoto wao wawe kama wao. Watu hawa Kuwanyang'anya Ikulu si kazi ndogo.. Ni kazi ya KUFA NA KUPONA: Sasa kama ambavyo wao waliapa kuilinda Serikali ya CCm isiondoke madarakani KUFA NA KUPONA basi CHADEMA nayo inahitaji watu WALIO TAYARI KUFA NA KUPONA ili haki itendeke.
Sina mpango wa kuwajibia viongozi wangu lakini kwa hali inavyoonekana na umakini wao wanaendelea na maandalizi ya kuweka na ama wameshaweka plan B. Hata hivyo what i believe ni kwamba si sahihi sana kuweka Silaha zako za kivita machoni pa adui yako kwa sababu atang'amua na kutengeneza silaha kali kukushinda wewe.
Thanks very much!
Tayari Jumuia ya Kimataifa wanazo taarifa za ndani zaidi juu ya mpango wa CCM kung'ang'ania madaraka au hata kujichagulia 'kukasimu' uongozi kwa JWTZ nje kabisa ya maelekezo ya katiba.
Wewe ngoja tu utaona kitu gani watakachofanyiwa wakati huo na hawa wadau wa demokrasia kote duniani endapo CCM watarogwa kufuata hizo ndoto zao za maangamizi.
...wewe anzisha yako ya kujichukiza...Nyie nao naona mmeanzisha thread ya kujifurahisha,peleka hii kwenye jukwaa la jokes.
Mkuu umefanya Uchambuzi Mzuri sana, kwa kuongezea machache ni kwamba;Ikumbukwe kuwa kuna walioapa kuilinda Serikali ya CCM kufa na kupona,Hawa wana uhakika wa kwenda Lunch Marekani na Dinner wakaenda Swiss kabla ya Kwenda London Kulala.. Hawa wana watoto wao wanaosoma huko huko ambao hawakuwahi kusikia njaa tangu kuzaliwa kwao.. Ama hao watoto wana watoto wao ambao wanataka nao wakija kuwa na watoto wao wawe kama wao. Watu hawa Kuwanyang'anya Ikulu si kazi ndogo.. Ni kazi ya KUFA NA KUPONA: Sasa kama ambavyo wao waliapa kuilinda Serikali ya CCm isiondoke madarakani KUFA NA KUPONA basi CHADEMA nayo inahitaji watu WALIO TAYARI KUFA NA KUPONA ili haki itendeke.
Sina mpango wa kuwajibia viongozi wangu lakini kwa hali inavyoonekana na umakini wao wanaendelea na maandalizi ya kuweka na ama wameshaweka plan B. Hata hivyo what i believe ni kwamba si sahihi sana kuweka Silaha zako za kivita machoni pa adui yako kwa sababu atang'amua na kutengeneza silaha kali kukushinda wewe.
Thanks very much!
Hivi kama wakibaki ikulu na wabunge hawana sisawa na bunduki bila risasi??
Ni imani yangu kuwa cdm watashinda kwa ushindi wa kawaida katika uchaguzi mkuu ujao. Ushindi huu wa kawaida si dalili njema kwa cdm, na hasa ukizingatia ccm wanavyohaha huku na huku kutafuta namna ya kuokoa jahazi, hata wamediriki kutoa uhai wa watu.Watazoea, na hata ikifika 2015 kuendelea kutoa uhai kwao si issue. Hayo ni mazingira magumu sana kwa cdm kusubiri kukabidhiwa dola kikatiba. Kenya wameishi kwa kuibiana kura kwa muda mrefu sana,wakati matokeo yanaonyesha kuwa Kibaki ameshindwa, kitu ambacho hakukitarajia sana,aliamua kuiba kura ambazo tayari zimekwisha hesabiwa.Kitendo hicho kilimfanya Moi kutamka maneno yafuatayo " Huyu mutu ya ajabu sana, wengine naiba mahindi yakiwa kwa shamba,yeye naiba ikiwa kwa stoo" .Unaweza kuona uzoefu wa nchi za kiafrika katika kusigina haki ya wanachi ya kuchagua.
Nataka kusema nini!
Washauri wa ccm ni hao hao (kenya,zimbabwe nk).Walau kwa watu wa kenya wameamka kiasi na wanaweza kuyakataa matokeo kama yamekwenda ndivyo sivyo, kwa watz bado sana.Tutaikataa ccm kwa kupiga kura tu,lakini isipokubali kuondoka hatuna plan B. Tutajikuta tunakuwa wanyonge na kuendelea kuumia kwa miaka mingine mitano. Siku za mwizi ni arobaini,lakini siku ya arobaini akiiba kwa mtu muoga huenda tukaendelea kuhesabu ya 41. Ni wakati sasa cdm kutueleza imejipanga vipi kuhakisha matokeo halisi yanatangazwa 2015.Naelewa kuwa kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha haki inatendeka, lakini viongoza wana nafasi nzuri zaidi kuliko sisi wanachama wa kawaida,lakini hata hivyo miongoni mwa majukumu ya kiongozi ni kuonyesha njia.
Nyie nao naona mmeanzisha thread ya kujifurahisha,peleka hii kwenye jukwaa la jokes.