CCM haitabaki salama!

CCM haitabaki salama!

shauri zako, ngoja mwigulu akusikie, Ngumi moja tu huamki, kasema mwenyewe.

Tehe................... alikuwa anamtishia Mchungaji................... hajui Mchungaji angekemea tu kwa neno jamaa anapiga chini!
 
Mussa Tesha=Condom ya Mwigulu,anatolewa kafala bila kujielewa.Ignorance is the problem.

nawalaani sana wale makada wa chadema waliommwagia tindikali musa tesha
[h=2]Makada watano CHADEMA kortini.[/h]
*Ni watuhumiwa wa tindikali Igunga 2011
*Waachiwa na kukamatwa, wapelekwa Tabora

MAKADA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Igunga, wakituhumiwa kummwagia tindikali Musa Tesha mwaka 2002.

Watuhumiwa hao, walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora jana, ambapo upande wa mashitaka uliondoa shitaka lililokuwa likiwakabili mahakamani hapo, hivyo kuachiwa huru lakini walikamatwa tena hapo hapo na kurudishwa korokoroni.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ajali Milanzi, mwendesha mashitaka wa polisi, Cosmas Mboya aliondoa shitaka lililokuwa likiwakabili watuhumiwa hao kwa kutumia kifungu cha 98 (A) cha Sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1985, kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kuhusu mwendesha mashitaka kufanya hivyo.

Baada ya kuondoa shitaka hilo, Hakimu Milanzi alikubaliana na upande wa mashitaka na kusema kuwa, washitakiwa wako huru.

Baada ya kufutiwa shitaka hilo, watuhumiwa walianza kutoka nje ya mahakama lakini ghafla walizingirwa na askari zaidi ya 40 waliokuwa wamesheheni silaha aina ya mabomu, bunduki na pingu ambao waliwakamata tena.

Walifungwa pingu, kisha wakapakiwa ndani ya magari mawili ya polisi ambayo yaliondoka eneo la mahakama kwa kasi huku yakiwaacha wananchi waliokuwa wamefurika mahakamani hapo katika mshangao.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga (OCD), Abeid Maige aliwaambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa wamepelekwa Tabora kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka mengine mapya. Hata hivyo hakuyataja.

Washitakiwa hao ni Evodius Justian (30) mkazi wa Bukoba, Osca Kaijage (36) mkazi wa Ndala mkoani Shinyanga, Rajabu Daniel (24) mkazi wa Singida na Seif Magesa (37) mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza.

Wote walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Igunga Aprili 12 mwaka huu, kwa kosa la kummwagia tindikali Mussa Tesha (26) mkazi wa Igunga Mjini, wakati wa kampeni za Uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba mwaka 2011.

Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Picha ya Musa Tesha kabla na baada ya kumwagiwa tindikali
paperclip.png
Attached Thumbnails

mtatumika sana na chadema kumwagia watu tindikali lakini siku ya mwisho lazma sheria ife na nyinyi
 
lazima pia Mwigulu Nchemba awe shahidi namba moja wa jamhuri.
Jamhuri iwe shahidi wa Jamhuri? yawezekanaje? Kwa sasa Mwigilu ndiye amirijeshi mkuu wa majeshi yetu na anachotaka ndiyo kinafanyika kwa amri yake - Ila cheo chake hiki kipya kinaisha baada ya mwenye -kigoda kumaliza muda wake, yawezekana pia ukawa mwisho wa kisiasa wa huyu kijana mwenzetu mwenye speed kali.
 
Kwani mwigulu ana akili timamu? Ni kichaa anayeua chama, huku mwenyekiti wake akishangilia.

Ina maana huyu Nchemba amewafanya watu wote kuwa mazezeta kiasi kwamba kila anachoongea kinaonekana kuwa ni sahihi na kupigiwa makofi? Ufike wakati watu wenye akili wagundue kuwa huyu anakipeleka Chama kusiko.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Watu tushindane kwa hoja,,,na chadema wakiamua kutembea na waliovunjwa miguu na kupoteza viungo vyao na POLICE CCM,,si jukwaa halitatosha,,,hayo tumeona tumuachie ALLAH,,,TULIANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU
 
Katika siku za hivi karibuni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Mwigulu Nchemba amekuwa akitembea katika kila kona ya nchi ya Tanzania na mfuasi mwenzetu wa CCM aitwaye Tesha. Mfuasi huyu anadaiwa (hasa na Mwigulu) kumwagiwa tindikali na wafuasi wa CHADEMA wakati wa harakati za Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Igunga.

[COLOR=#000000 [B]Mwigulu Nchemba[/B] ameshazunguka sehemu mbalimbali akiwa naTesha-wa-Igunga. Mwigulu anaomba uungwaji mkono wa watanzania kupitia mhanga huyu wa tindikali. Ni hivi katibuni tu Mwigulu Nchemba alikuwa na Tesha-wa -Igunga katika Kampeni za uchaguzi za Udiwani wa Arusha.[/COLOR]

Nia hasa ya Mwigulu Nchemba ya kutembea na kuutangazia umma kuwa Tesha-wa-Igunga amemwagiwa tindikali na CHADEMA na kuwa kama alivyo sasa ilikuwa ni kupaka matope CHADEMA na kuonesha chama hicho kama chama cha unyama na hakifai kuaminiwa na kuungwa mkono na watanzania.

Nia nyingine ni kuanzisha kesi dhidi ya CHADEMA. Hili sasa linafanywa na Polisi na Kurugenzi ya Mashtaka. Lakini,vyombo hivi vya kisheria vilikuwa wapi tangu uchaguzi wa Igunga hadi Mwigulu Nchemba alipoanza kutembeana Tesha-wa-Igunga? Vipi kuhusu Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage waliomwagiwa Tindikali hata kabla ya Tesha-wa-Igunga? Nani alizunguka nao? Wao hawana thamani?

Siasa ni hoja,sera na ushawishi.Si vinginevyo. Ushindi wa mezani umepitwa na wakati. Si kila mtu anafurahia ‘kunyanyaswa’ kwa CHADEMA.Wengine wanaona huruma na kuona kuwa chema kinakatazwa kisiwasaidie watanzania.

Tesha-wa-Igunga hataisaidia chochote CCM yetu zaidi ya kupandikiza umakini wa kutenda,KUCHUNGUZA na kusema kwa CHADEMA. CCM,katika hali hii,haitabaki salama.Italindwa,itatumikiwa lakini ipo siku itasalitiwa na kukimbiwa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Tujikumbushe mazingira ya Tesha kumwagiwa tindikali

[video=youtube_share;GhPg5hQKthw]http://youtu.be/GhPg5hQKthw?t=4m17s[/video]
 
wakati mwingine kumuongelea sana huyu mwigulu ni kupoteza muda, dawa yake huyu ni vidole vya maxxxko tu, atakuja mikoani tu....
 
CCM Haiwezi kubaki salama kwani dhambi walizozifanya ni kubwa na nyingi so wananchi lazima tuwahukumu mwaka 2015 Roho za ndugu zetu waliotangulia hazitaenda bure, na machozi tunayolia sasa hivi hayamwagiki bure
 
Kwani mwigulu ana akili timamu? Ni kichaa anayeua chama, huku mwenyekiti wake akishangilia.

Kama Mwigulu anayeshangiliwa na mwenyekiti wake hana akili timamu, hata mshangiliaji hana akili timamu! Na walioko CCM wote hawana akili timamu kwa kuwa ni lazima watekeleze matakwa ya mwenyekiti ambaye hana akili timamu. Hivyo nchi inaongozwa na watu ambao hawana akili timamu. Tutegemee nini kwa uongozi wa nchi ya aina hii?! Ni mabalaa nchi nzima, na ndicho kinachotokea!
 
kwa wataalamu wa sheria kupitia majukwaa ya kampeni wafuasi wa chadema tayari wamehukumiwa na mh. Mchemba mwigulu kuwa ndio waliofanya kitendo kile hapo hapo wafuasi wake wanashtakiwa kwa kosa ambalo mh mchemba mwigulu ameshatoa hukumu........sheria hapa inasemaje? Wanashtakiwa ili kukazia hukumu ya mh.mchemba au itatolewa hukumu ingine? vuta-nkuvute

hapa umenena.ninavyojua hapa hakuna kesi.wataalam wa sheria mtujuze.
 
Ivi Kweli watu wote wenye akili timamu CCM...Mmekaa pembeni chama mmemwachia mwigulu...
 
Baba yetu mzazi,wengi kwa sasa wanamwita babu<hasa kizazi cha 90s> ila sisi tuliokuwepo toka enzi za uhai wake mpk mauti yanamkuta tunamuita Baba wa Taifa,huyu mzee pamoja na mabaya yake,mazuri yalifunika uovu wake wote na mpk sasa tunaishi kwa kupitia maono yake,na daima hatakuja kutokea mtu wa hivyo tena.

Alicheza issue zake chini kwa chini na kwa tahadhali za hali ya juu japo yeye ndiyo alikuwa kila kitu i mean amri jeshi mkuu,kuliko sasa ambapo watu wamekuwa miungu watu,wanafanya umafia waziwazi na wala hawana wakumuogopa si Rais wala Waziri mkuu,wanaua raia wenzao kama nyati,ambao ni masikini kama walivyokuwa wao awali kisha wakikutana wanacheka na kupongezana<................NIMEKOSA NENO NZURI LA KUWEKA> Kifupi hii siyo ccm tuliyorithishwa na mzee mchonga,kwa vile bado tupo tupo sana na Mungu sio Mwanamalundi ipo siku Kazi ya mikono ya Mungu itakamilka
 
Umeongea vizuri, Siasa ni Sera na Ushawishi.
Unaweza kuta Kijana ameahidiwa Maisha Mazuri na Mambo Mengine, ila hajui au hawajui kuwa wanajidhalilisha tu.
Hivi CCM hakuna Washauri wa Siasa?? Watanzania aka Wananchi tunataka Maisha Bora yenye kuzingatia Haki na Usawa na Kufuata Sheria na Katiba ya Nchi.

Katika siku za hivi karibuni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Mwigulu Nchemba amekuwa akitembea katika kila kona ya nchi ya Tanzania na mfuasi mwenzetu wa CCM aitwaye Tesha. Mfuasi huyu anadaiwa (hasa na Mwigulu) kumwagiwa tindikali na wafuasi wa CHADEMA wakati wa harakati za Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Igunga.

[COLOR=#000000 [B]Mwigulu Nchemba[/B] ameshazunguka sehemu mbalimbali akiwa naTesha-wa-Igunga. Mwigulu anaomba uungwaji mkono wa watanzania kupitia mhanga huyu wa tindikali. Ni hivi katibuni tu Mwigulu Nchemba alikuwa na Tesha-wa -Igunga katika Kampeni za uchaguzi za Udiwani wa Arusha.[/COLOR]

Nia hasa ya Mwigulu Nchemba ya kutembea na kuutangazia umma kuwa Tesha-wa-Igunga amemwagiwa tindikali na CHADEMA na kuwa kama alivyo sasa ilikuwa ni kupaka matope CHADEMA na kuonesha chama hicho kama chama cha unyama na hakifai kuaminiwa na kuungwa mkono na watanzania.

Nia nyingine ni kuanzisha kesi dhidi ya CHADEMA. Hili sasa linafanywa na Polisi na Kurugenzi ya Mashtaka. Lakini,vyombo hivi vya kisheria vilikuwa wapi tangu uchaguzi wa Igunga hadi Mwigulu Nchemba alipoanza kutembeana Tesha-wa-Igunga? Vipi kuhusu Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage waliomwagiwa Tindikali hata kabla ya Tesha-wa-Igunga? Nani alizunguka nao? Wao hawana thamani?

Siasa ni hoja,sera na ushawishi.Si vinginevyo. Ushindi wa mezani umepitwa na wakati. Si kila mtu anafurahia ‘kunyanyaswa’ kwa CHADEMA.Wengine wanaona huruma na kuona kuwa chema kinakatazwa kisiwasaidie watanzania.

Tesha-wa-Igunga hataisaidia chochote CCM yetu zaidi ya kupandikiza umakini wa kutenda,KUCHUNGUZA na kusema kwa CHADEMA. CCM,katika hali hii,haitabaki salama.Italindwa,itatumikiwa lakini ipo siku itasalitiwa na kukimbiwa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Ni kweli, ingawa mfa maji haishi kutapatapa lakini kutapatapa huku kwa CCM kutaiangamiza pia na CCM yenyewe
 
Back
Top Bottom