CCM haitaanguka bila kusaidiwa

CCM haitaanguka bila kusaidiwa

Joined
Jul 3, 2020
Posts
6
Reaction score
97
Shalom!

CCM haitaanguka yenyewe,
Bila kusaidiwa kuanguka. Tusipowasaidia, wataendelea kutawala.

Na kwa uzoefu tulionao, hawajali watu wanawaza nini ili washinde.
Watafanya watakacho ili waendelee kushika dola.

Walivyoweza kujipanga kwa nguvu baada ya sakata la Lowassa mwaka 2015, tulipaswa kujifunza kuwa wanaweza kufanya hivyo tena mwaka huu.

Hawahitaji idhini ya umma, wanahitaji ushindi wao ndani tu kisha waendelee walipoishia kwa nguvu mpya.

Historia inatufunza kwamba,
Mara zote Migogoro yao ya ndani siyo mwisho wao bali
Ni hatua ya kujipanga upya kwa mikakati, sura na makucha mapya.

Na kila wanapomaliza kujipanga, huja kwa mikakati na nguvu zaidi dhidi ya upinzani wa kweli.

Kama sasa walivyogawanyika namna hii, na hatuwezi kutetea uhuru wa ibada,
Kuilinda CHADEMA,
Na kushinikiza REFORMS,
Tutawezaje kuwakabili wakishajipanga tena, wakiungana na kuwa wamoja?

Huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo pilika za kisiasa huwa ni nyingi na kuna tahadhari pia ya kutopoteza ushawishi kwa chama na viongozi ila under their watch
bado imewezekana

Kufungia makanisa,
Kusitisha shughuli za chama kikuu cha upinzani na kufuta uongozi wake
Na kisha kumweka gerezani mwenyekiti Lissu, kiongozi mwenye ushawishi mkubwa zaiadi wa kisiasa nchini, ila pia kuwapoka jukwaa waandishi nguli wa habari.

Sasa tujiulize:
Wakimaliza migogoro yao na wakishinda tena Urais,
Watafanya nini?

Watamalizia kabisa mabaki ya upinzani na watafuta hata chembe ya uhuru wa habari iliyosalia.

Tusijidanganye.
Kukaa kimya tukitarajia CCM igawanyike na kuanguka yenyewe kisha tuokote dodo kwenye muarobaini ni kujilisha upepo.

CCM haitajiangusha, bila shinikizo toka nje na ndani na
bila mbano wa kisiasa kutoka kwa wananchi. Wataendelea kututawala kwa kuwa hatuna strategy na mara zote tunajadili matukio yao badala ya kuimarisha mikakati yetu.

Wana msemo wao:
“Yeyote atakayeshinda ndani ya CCM, CCM imeshinda.”

Kwao si muhimu sana nani anashinda, yeyote akishinda
Ni mfumo wao unabaki hai.

Na sisi je?
Tuko wapi?
Tuna mpango gani?

Huu ndio wakati wa kuonyesha nguvu zetu.

Kisiasa kwa harakati.
Kiimani kwa msimamo.
Kiutetezi kwa ushawishi.

Huu ni wakati wa mikakati makini na ya nguvu,
Si maombi pekee ya kimyakimya tukisubiri miujiza ya maanguko ya wengine bila kusababisha.

Political chaos is not a pit.
It is a ladder.

Wataojipanga na kupanda sasa, huandika historia.
Wanaolala, hubeba matokeo ya wale waliothubutu kusonga mbele.

Tunayo nafasi adimu sana.
Leo CCM iko katika hali ya kugawanyika, kushukuana, na kutoaminiana kuliko wakati mwingine wowote.

Lakini pia tofauti na 2015, leo uongozi wao kwa miaka kadhaa wamevuruga kila eneo muhimu la kijamii.

Wamevuruga CHADEMA ambayo ni sauti kubwa ya watu.
Wamevunja daraja na makanisa kwa kufungia baadhi na tumesikia pia viongozi wa dini kutekwa na wengine kuumizwa na pia
Wamechafua mahusiano ya kikanda na kimataifa.

Huu siyo mgogoro wa kawaida, hii ni fursa ya kihistoria ambayo haitajirudia kwa miaka mingi ijayo, kwakuwa wakitoka hapa salama wata amend baadhi ya mambo.

Mwaka 2015 walivurugana wao kwa wao pekee ila hali ilikuwa mbaya sana kwao, tulikosea finishing tu ili kushinda ule Uchaguzi.

Sasa basi, si itakuwa zaidi sana ambapo leo wamevuruga kila kundi muhimu katika jamii na bonus ya mgogoro mkubwa wa wao wenyewe ndani kwa ndani?

Swali ni Je,
Tunafanya nini kutumia fursa hii adhimu?

Au tunatazama tu, tukisubiri muujiza tena ambao wengi wetu hatuko tayari kukiri kuwa MUNGU kwa sasa ndiye tegemeo letu pekee?

Ukweli ni kwamba mbali na maombi na imani, viongozi, wadau na wanachama wote tunahitaji kuchukua hatua za haraka na dharura kwa akili na weledi. Hii ni vita ya nguvu dhidi ya maarifa.

Tukijenga ngome kimya kimya mtaa kwa mtaa.
Na kuunganisha sauti za viongozi wa dini, wanazuoni, na wanaharakati wa ndani na nje. Wanahabari walioumizwa na wana CCM wanaohisi kuonewa,

Sambamba na kuibua simulizi ya matumaini, na si malalamiko na pia
Tukajenga mawasiliano ya ujasiri, na si ya hofu kwa jamii za Kimataifa,

Na kuamsha harakati ya chini kwa chini.
Inayoeleweka kwa mtu wa kawaida na siyo harakati ya wasomi peke yao — tunaweza kujiweka pazuri kuliko kukaa and do nothing huku tukisherehekea mgogoro wa CCM ambao wote humu tunajua wakishamalizana they will turn on the remaining of the opositions.

Siasa si ibada ya kusubiri miujiza pekee, ni hatua ya maamuzi wakati fursa iko mbele yako.

Na huu ndio wakati huo.
Tukikosa kuchukua hatua sasa, tutajuta baadaye coz ukweli mchungu ni kwamba, they will hit us HARD na kwakuwa so far wameshatuvunjavunja itakuwa rahisi kutumaliza kabisa.

Tukumbuke kuwa baada ya UCHAGUZI mkuu, miaka mitatu ijayo shughuli za kisiasa huwaga zinapoa.

Na je, kama tulishindwa kufanya jambo kwenye mwaka ambao shughuli za kisiasa ni za moto —
tutaweza wakati zimepoa?

Fredrick Mbwambo.
 
😀. Ccm
IMG_1893.jpeg
 
Back
Top Bottom