Sio kweli kwamba CCM haina imani na watanzania kushinda uchaguzi. CCM inajua watanzania wanakiamini chama na uchaguzi ukifanyika watashinda kwenye sanduku la kura. Wasio na imani na watanzania kwamba wataipigia CCM kura ni watendaji wa serikali. maRC, maDC na wakurugenzi wa serikali za mitaa hawa ndio hawaamini kwamba bado watanzania wanaipenda CCM. Viongozi wa CCM hata Magufuli mwenyewe wanaamini kwamba wanapendwa ndio maana inapotokea uchaguzi unafanyika bila viongozi wa serkali kuingilia kati huwa wanashinda vizuri na wapinzani huwa wanatulia kwa sababu wanajua CCM wameshinda kihalali. Hivi vyeo visivyo na specific qualification kuvipata vinaleta tabu sana katika jamii. Wengine wameteuliwa kwa uchapakazi wao lakini kwa sababu aliye wateua huwa haweki wazi vigezo alivyotumia kuwateua huwa wanahangaika sana kuhisi kwa nini ameteuliwa. Hisia yao kubwa ni kwamba wameteuliwa kusaidia kazi za viongozi wa CCM. Wanawaogopa wananchi kwa sababu hawajui siasa wala hawana uwezo wa kuwashawishi hivyo unapofika uchaguzi wao wanahofu zaidi ya wana ccm kupoteza uchaguzi katika maeneo yao. Kwa kuliona hilo siku hizi wanaccm wenyewe huwa hawahangaiki sana na ushindi wa chama chao, wamewaachia watendaji serikali wafanyanye, wao wapewe majibu. Ndio maana ikitokea ccm imeshindwa kwenye uchaguzi sehemu fulani huwa hawendi kuwauliza wanachama wao wa eneo hilo, imekuwaje wameshidwa. Wanaenda moja kwa moja kwa Mkurugenzi au DC au RC kumhoji kuwa kwa nini hajafanyakazi yake ccm imeshindwa.
Ukifuatilia hata kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa wanaopongezana sana kwa ccm kupìta bila kupingwa ni viongozi wa serikali kuliko hata viongozi wa ccm wenyewe.