CCM haina tena imani na Watanzania

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,694
34,766
CCM haiamini tena kama kuna watanzania wa kutosha watakaopiga kura kwenye uchaguzi wowote ule na kukichagua chama hicho.

Vitendo vya kupora Fomu za wagombea wa vyama vingine, kufunga Ofisi ili fomu zilizochukuliwa zisirudishwe, kuzuia wagombea wa vyama vingine kuchukua fomu, na kuruhusu kila aina ya uhuni kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa ni dalili kwamba CCM haina Imani tena ya kuchaguliwa na watanzania kwenye uchaguzi ulio huru.

Kama CCM ingekuwa ina imani kwamba watanzania wataichagua bila ya shaka hizi sarakasi zote tunazoziona zisingekuwepo.

KIZA KINAPOKUWA KINENE NDIPO KUNAPOKARIBIA KUCHA!!
 
Magufuli alidhani sera za kuuwa kufunga na kunyang',anya mali za watu zitamsaidia amekuwa mwenyekiti wa kwanza ccm kufanya organised crime kukataa uchaguzi yaani hana ushawishi watanzania walimkataa 2015 na sasa anathibitisha mwenyewe kwamba ni nguvu ya soda kisiasa Bure kabisa ni tapeli na hana nia njema na nchi hana wagombea ha ha
 
Screenshot_20191016-224559-picsay.jpeg
 
Kila chenye mwanzo, Hakikosi kuwa na mwisho. Haijalishi ni mwisho wa aina gani. Hao wanaojiona ni bora zaidi watafika mwisho wala hakuna atakaewakumbuka. Watasahaulika kabisa. Manung'uniko ya watu yakiwa mengi sana hugeuka kuwa laana. Wenye hekima hujihadhari na kujiepusha na manung'uniko kwao.
 
Magufuli alidhani sera za kuuwa kufunga na kunyang',anya mali za watu zitamsaidia amekuwa mwenyekiti wa kwanza ccm kufanya organised crime kukataa uchaguzi yaani hana ushawishi watanzania walimkataa 2015 na sasa anathibitisha mwenyewe kwamba ni nguvu ya soda kisiasa Bure kabisa ni tapeli na hana nia njema na nchi hana wagombea ha ha
Umenena Mkuu.. Kama anakubalika hana haja ya kulazimisha na kuhadaa.. Na hiinitawaumiza sana maana wanafanya haramu ku justify halali.. Kama wanakubalika waache wananchi wawe guru na vyama vipige siasa kama kawaida.. Ni aibu hata wakienda nchi jirani maana watashidwa kuelezea ilikuwaje contestant wengi hivyo kukosa sifa kipindi hichi..
 
Back
Top Bottom