CCM Hai kwachafuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Hai kwachafuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, May 9, 2011.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  *Vigogo wawili wavuliwa gamba
  *Mmoja anyang’anywa uanachama

  Na Omary Mlekwa, Hai
  [​IMG]HALI ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, si shwari, baada ya viongozi wawili kujiuzulu na wengine kuvuliwa uanachama.
  Hatua hiyo imekuja baada ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya hiyo kuishutumu Kamati za Siasa za Kata na Wilaya kwa kukihujumu chama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
  Waliojiuzulu ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Wilaya ya Hai, Moses Munuo; na Mwenyekiti wa Kata ya Machame Kaskazini, Nassoro Mushi.
  Viongozi hao walitajwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya kuwa ni miongoni mwa wanachama mamluki waliokihujumu chama mwaka jana.
  Katibu Uenezi alituhumiwa kujihusisha na kampeni katika vyama vya upinzani na kushindwa kuvunja makundi yaliyojitokeza kipindi cha kura za maoni na kuendeleza siasa za fitina.
  Akizungumza katika kikao, mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, Justine Swai, alisema baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya walichangia kushindwa kwa CCM.
  Wakitangaza kujiuzulu nyazifa hizo katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Hai, Munuo alisema kuwa kutokana na wajumbe kukosa imani naye, anaamua kujiuzulu nafasi hiyo na kuendelea kuwa mwanachama wa CCM
  Munuo, ambaye pia alishawahi kuwa diwani kupitia Chama cha Demokrasia na
  Maendeleo (CHADEMA), alisema kuwa tuhuma dhidi yake si za kweli, na ili kulinda heshima ya chama, ameamua kujiuzulu, lakini akaahidi kuwa mwanachama mwadilifu wa CCM.

  Kwa upande wake, Mushi, ambaye alikuwa meneja kampeni katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu, alisema anajiuzulu ili kupisha wanachama wengine kuongoza chama hicho.
  Awali, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hai, Dk. Amini Uronu, alipongeza hatua zilizofikiwa na wajumbe hao wa Kamati ya Siasa na kusema kuwa wataendelea kukisafisha chama kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho mwakani.
  Alisema usafishaji huo unalenga kuandaa “jeshi imara” kwa ajili ya kujipanga kulikomboa Jimbo la Hai mwaka 2015. Kwa sasa Mbunge wa Hai ni Freeman Mbowe wa Chadema.
  Pamoja na kujadili kwa kina utendaji wa Kamati ya Siasa, wajumbe hao
  walipendekeza kuvuliwa uanachama aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu mwaka 2005-2010 na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Rehema Mzava, kwa madai ya kutojali maslahi ya chama.

  Wajumbe hao waliazimia kwa pamoja kumwondoa mjumbe huyo na kumnyang’anya kadi ya chama bila kujali wadhifa wake ili kuondoa mamluki.
  Pia katika kikao hicho wajumbe walisema kuwa hawana imani na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Christopher Awinia, kutokana na kushindwa kutoa ushirikiano na kushindwa kuvunja makundi baada ya kushindwa katika kura za maoni. Walisema kuwa Awinia alionyesha nia ya kuisaidia Chadema.
  Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga, aliwataka wajumbe hao kufuata taratibu za CCM, kwani Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Mkoa ndiyo wenye mamlaka wa kunyang’anya kadi. Aliwataka wajumbe wavute subira juu ya suala la Mzava.
  Katika kikao hicho, wajumbe walijadili taarifa za utekelezaji wa Ilani ya
  Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010.

  Akiwasilisha taarifa, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla, alisema Sh bilioni 4.9 zilitumika katika sekta ya maji kwa kuwezesha wananchi wa mijini na vijijini kupata maji safi na salama.
  Sigalla alisema kati ya fedha hizo, Sh bilioni 3.8 zilitokana na ufadhili wa Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali


  Source: Gazeti la Mtanzania, Mei 9, 2011

  SAFI SANA CCM KWA KUVUA MAGAMBA KATIKA NGAZI MBALIMBALI ZA UONGOZI
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  khaaaa!!endeleeni kumtafuta mchawi...gamba kuu lipo ikulu sijui atanyang'anywa kadi na nani...akina RACHEL wanazid kupeta tu!!
   
 3. M

  Maga JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Asubuhi wakati wa kupitia magazeti TBC1 hili gazeti lilikuwa juu kabisa lakini kwa mshangao wangu yule dada Amina Mollel alilitoa haraka sana baada ya kuona kichwa hicho cha habari na hakulisoma tena.
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,001
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  halafu gamba lenyewe mbona km limeanza kuota lingine? si karibia wiki kadhaa sasa zimepita tangu gamba livuliwe? mnataka mnambie halijachipuka lingine? kama gamba lingine halijachipuka watakuwa wanaishije wkt ndo vazi lao rasmi?
   
 5. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Magamba imekula kwao:bange:
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wana kazi ccm mwaka huu! Wapo bize kufukuzana na vidagaa wakati wanaliona li kambale. Chama kimekufa hicho na maiti imeshaanza kutoa harufu! Wanahitaji kuzaliwa upya na sio ufufuo maana mwili umeoza!
   
 7. x

  xman Senior Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwakuanza nawapongeza c.c.m kuanza kujivua gamba katika ngazi za chini lakini kama jamaa hapo juu alivyosema kuna lile gamba kuu ambalo lipo ikulu na lenyewe linabidi litolewe haraka la sivyo itakuwa kazi bure.
   
 8. d

  dotto JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  nimeipenda hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. p

  plawala JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanapewa maelekezo nadhani,sio amina tu,hata na watangazaji wengine wanakwepa habari yoyote inayokula kwa ccm
   
 10. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hili si ni gazeti la RA, limewezaje kuanika haya?
   
Loading...