Kufanananisha uchaguzi wamwaka huu na 1995 enzi ya Mrema nikujidanganya.
Ikumbukwe 1995 ulikuwa niuchaguzi wakwanza kwamfumo wavyama vingi natulikuwa ndokwanza tunamiaka mitatu tangu mfumo huo uanze. Kwa waliokuwepo watakumbuka matangazo mbalimbali yakuwahadaa wapigakura kwamba wakichagua wapinzani watasababisha vita. Watu waliowengi waliyaamini matangazo hayo nakwa kiasi flani inawezakuwa ilichangia kumpunguzia mrema kura. Tujiulize kwa watanzania waleo walioshuhudia makeke mbalimbali yawapinzani kama kina Tundu lisu, John Mnyika, Peter Msigwa, Mr.Sugu, David Kafulila nk, ninani wakuambiwa wapinzani wataleta vita akaamini? Jibu ni0.
Vilevile 1995 mtu aliyefanyakazi kubwa kubadili upepo alikuwa baba wa Taifa. Alikuwa ndomtu pekee ambaye watanzania tulimuamini kutokana nautumishi wake uliotukuka. Mwalimu hakutuibia, alituongoza kwa weledi mkubwa. Mungu amlaze mahala pema baba wawatu. Leo tujiulize nikiongozi gani mstaafu atatueleza lolote watanzania tumuelewe? Hakuna hatammoja wote niwezi nawanafiki wakubwa.
Mfano tumeshuhudia kashfa mbalimbali zakuliumiza taifa, nahao wastaafu wapo. Hatujawahi kuskia sauti zao wakikemea popote. Ila Mwl angekuwepo tunaimani walahata kutokea hizo kashfa zisingetokea. Au zingetokea angetoka Butiama hata kwamguu endapo wangemnyima usafiri.
Kwahiyo huu moto wamwaka huu umeshawaka nahakuna wakuuzima. Hilo likowazi kwamtu mwenye kufuatilia hali yamambo utajua tu.