Kwa hili swala la ugaidi, CHADEMA anzeni mapema kutafuta mwenyekiti na katibu mpya wa chama.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Kwa jinsi CCM na kitengo chao cha propaganda cha Polisi walivyocharuka, unachosema kina uwezekano mkubwa sana kutokea hapa nchini!!
Kama hivi sasa mtu anaweza kujifungia chumbani akafanya utundu wake wa Teknohama, na baadaye akapeleka tu clip iliyoandaliwa kiujanja na ikaonekana Mwenyekiti na Katibu wa CDM wana mpango wa kumteka Mwigulu Nchemba au Nape Nnauye, halafu Polisi wanafungua kesi kiurahisi tu ya ugaidi, hivi unadhani kweli ifikapo 2015 CDM itakuwa na wagombea wale hasa ambao chama kilikuwa na nia ya kuwasimamisha??!!
Kwa hali tunayokwenda nayo, baada ya CCM kuona kwamba hawana tena nafasi ya kushinda uchaguzi 2015, kwa hiyo kinachofanyika na CCM kwa ushirikano wa karibu kabisa wa Jeshi la Polisi na usalama wa Taifa, ni kufanya mbinu ya kuwabambikia kesi ya ugaidi viongozi wote wa juu wa Chadema, hatua ambayo itafuata ni fujo ambazo zitawafanya serikali ya CCM itangaze hali ya hatari nchini, kwa maana ipate kisingizio cha kutofanyika uchaguzi mkuu mwaka 2015!!
Kwa mtu anayeyaangalia kijuu juu maswala haya, anaweza kuyaona ni simple, lakina kwa uhakika kabisa inaonekana wazi CCM kishaanza kuuvuruga uchaguzi wa mwaka 2015, ili usifanyike, ili wao waendelee kutawala kwa kisingizio cha hali ya hatari!!
Kwa mazingira haya vyombo vya habari vina mchango muhimu sana wa kulifanya Taifa letu liendelee na utulivu, kwa kusema bila kificho kuwa mipango yote miovu ya nchi hii, inafanywa ikiwa na baraka zote za Rais wa nchi yetu, na kwa yeyote atakayelipinga hilo, aniambie sababu za msingi za Rais wetu kutoweza kumfukuza kazi IGP Mwema, pamoja na kuwa katika kipindi cha uongozi wake ndiyo kumetokea mauaji mengi ya raia yenye utata na matokeo ya kutekwa na kuteswa raia wasio na hatia, bila wahusika kukamatwa na badala yake wanakamatwa wanaharakati, kwa makosa ya kufikirika eti walikuwa na mpango wa kuteka, na hapo hapo wanafunguliwa mashtaka ya ugaidi!!
Iwapo tukio la utekaji linatokea na aliyetekwa anawataja waliomteka,kama ilivyokuwa kwa Dr Ulimboka, Polisi haitaki kuwakamata, badala yake inawakamata watu kwa maelekezo ya Ikulu, hivi kweli nchi yetu Tanzania inaelekea wapi? Kwa kweli kwa hali tuliyofikia nchi hii, kila mtu kwa nafasi yake, atafute muda wa kumwomba Mungu, ili aweze kulinusuru Taifa letu na hili janga la dhahiri, linaloelekea kutupata la kuteketea!!