CCM eleweni jinsi Uchumi wa Kibepari ulivyo!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,961
Reaction score
51,102
Yaani kila kona CCM wanataka kuwajaza hofu watanzania kuwa kuna "hatari" inawanyemelea kupokonywa "mali yao" kwa ama hisa zinazouzwa ama viongozi wanaoteuliwa. CCM mmeukumbatia wenyewe mfumo wa Kibepari (ingawa kiuchwara) lazima mkubaliane na jinsi unavyoendeshwa.

Hisa ni mfumo ambao mwenye hela ndiye anayekuwa na maamuzi ya mwisho kwenye jambo analolimiki. PSG ni Timu ya Mpira wa Miguu ya Ufaransa, lakini wanaoimiliki ni Qatar Sports Investment na Nasser Bin Ghanim Al-khelaifi ndiye Rais wake!

Kwenye Ubepari uzalendo ama maslahi ya taifa huwa yanahusiana na ushawishi kwa wanaonunua hisa ama mikataba inalazimisha nafasi kwa wazawa wakati wa uuzaji wa hisa. Sasa CCM wanataka kuendesha uchumi wa Kibepari kwa fikra za kijamaa, hili haliwezekani.

Kwa mfano, Vodacom. Jee hii kampuni ni mali binafsi ya watu ama ni shirika la umma. Kampuni hii imeanzia Tanzania ama ni kampuni tanzu ya Kampuni kubwa yenye matawi kwenye nchi nyingine pia? Kuwalazimisha Vodacom kuajiri mtanzania mliwasaidia kuwekeza mtaji?

Hivi Vodacom inapopata faida huwa inawagawia watanzania ama inapopata hasara serikali huwa inawafidia? Serikali ina hisa kwenye Vodacom? Kuna watu wanahoji mambo ya Elimu kwenye biashara za watu, kama Vodacom inaona wanaemteua anakidhi matarajio yao, hilo ni jambo lao binafsi na wala si la umma.

Ukija kwenye suala la Simba na Yanga, utaona watu wanavyojazwa hofu ya "kukosa sauti" kwenye klabu hizo ambazo sasa zimepachikwa jina kwamba ni za wananchi. Yaani "wenye Klabu" ambao michango yao kwa mwaka haifiki milioni 100, wabakie na "sauti" dhidi ya watu wanaotumia mabilioni ya shilingi kuziendesha hizo Klabu, huu si uendawazimu?

Mpira ni biashara na "sauti" kwenye mambo ya vilabu vya kisasa vya mpira si historia ya kuwepo wakati Jengo la Klabu linajengwa, bali ni wingi wa hisa ulizo nazo. Wanaojidai kulinda maslahi ya wana Simba na Yanga ni kwa nini hawahoji umiliki wa Klabu ya Azam?

Tunaishi katika zama za Ubepari (hata kama ni uchwara) na CCM ambao ndiyo wanaoongoza serikali yetu kwa sasa,lazima wajifunze jinsi ya kuenenda na mfumo huo wa kibepari.
 
Muhimu kujiuliza; hili suala lina maslahi makubwa kwa taifa? Kama jibu ni ndio tuache unazi usio na sababu. Pili, sheria (e.g. za ajira) zinasemaje? Maamuzi yaliyofanyika yako kinyume na sheria? Kama sivyo, kelele za nini?
 
Msingi tuanzie jee makampuni makubwa ya kimataifa (Multinational Companies) yanamilikwaje na yanaendeshwaje. Wakati wanapohimizwa kuja kuwekeza nchini mwetu huwa wanapewa masharti gani?
 
We Allen ! Tafakari upya ulichokiandika
 
Msingi tuanzie jee makampuni makubwa ya kimataifa (Multinational Companies) yanamilikwaje na yanaendeshwaje. Wakati wanapohimizwa kuja kuwekeza nchini mwetu huwa wanapewa masharti gani?
Uwekezaji wowote wa kimataifa ni lazima uzingatie, tena kwa uangalifu, factors nyingi sana kama culture ya mahali husika (rejea Hofstede's Cultural Dimensions), existing and anticipated competition, legal and regulatory frameworks, etc.

I hope Voda walizingatia yote hayo kabla ya kutia mguu nchini. So, wala hawahitaji kupewa masharti, wanatakiwa wazingatie mazingira ya uwezekaji, masharti (sio ya mdomo), sheria, na taratibu za mahali husika. Ukiwekeza just kwa kuangalia regime iliyopo na ahadi za mdomo mlizopeana hotelini huko Davos, ni hatari sana (rejea Mkataba wa Buzwagi uliodaiwa kusainiwa hotelini London ``usiku wa manane``).
 
Muhimu kujiuliza; hili suala lina maslahi makubwa kwa taifa? Kama jibu ni ndio tuache unazi usio na sababu. Pili, sheria (e.g. za ajira) zinasemaje? Maamuzi yaliyofanyika yako kinyume na sheria? Kama sivyo, kelele za nini?
Mbaya zaidi kaleta hoja ikitanguliza uvyama,ccm inakujaje?,suala hili lipo kitaalam na kisheria zaidi za nchi husika na za kimataifa.
Uchangiaji hapa hautakua na weledi,simba na yanga
 
Yaani kila kona CCM wanataka kuwajaza hofu watanzania kuwa kuna "hatari" inawanyemelea kupokonywa "mali yao" kwa ama hisa zinazouzwa ama viongozi wanaoteuliwa. CCM mmeukumbatia wenyewe mfumo wa Kibepari (ingawa kiuchwara) lazima mkubaliane na jinsi unavyoendeshwa.

Hisa ni mfumo ambao mwenye hela ndiye anayekuwa na maamuzi ya mwisho kwenye jambo analolimiki. PSG ni Timu ya Mpira wa Miguu ya Ufaransa, lakini wanaoimiliki ni Qatar Sports Investment na Nasser Bin Ghanim Al-khelaifi ndiye Rais wake!

Kwenye Ubepari uzalendo ama maslahi ya taifa huwa yanahusiana na ushawishi kwa wanaonunua hisa ama mikataba inalazimisha nafasi kwa wazawa wakati wa uuzaji wa hisa. Sasa CCM wanataka kuendesha uchumi wa Kibepari kwa fikra za kijamaa, hili haliwezekani.

Kwa mfano, Vodacom. Jee hii kampuni ni mali binafsi ya watu ama ni shirika la umma. Kampuni hii imeanzia Tanzania ama ni kampuni tanzu ya Kampuni kubwa yenye matawi kwenye nchi nyingine pia? Kuwalazimisha Vodacom kuajiri mtanzania mliwasaidia kuwekeza mtaji?

Hivi Vodacom inapopata faida huwa inawagawia watanzania ama inapopata hasara serikali huwa inawafidia? Serikali ina hisa kwenye Vodacom? Kuna watu wanahoji mambo ya Elimu kwenye biashara za watu, kama Vodacom inaona wanaemteua anakidhi matarajio yao, hilo ni jambo lao binafsi na wala si la umma.

Ukija kwenye suala la Simba na Yanga, utaona watu wanavyojazwa hofu ya "kukosa sauti" kwenye klabu hizo ambazo sasa zimepachikwa jina kwamba ni za wananchi. Yaani "wenye Klabu" ambao michango yao kwa mwaka haifiki milioni 100, wabakie na "sauti" dhidi ya watu wanaotumia mabilioni ya shilingi kuziendesha hizo Klabu, huu si uendawazimu?

Mpira ni biashara na "sauti" kwenye mambo ya vilabu vya kisasa vya mpira si historia ya kuwepo wakati Jengo la Klabu linajengwa, bali ni wingi wa hisa ulizo nazo. Wanaojidai kulinda maslahi ya wana Simba na Yanga ni kwa nini hawahoji umiliki wa Klabu ya Azam?

Tunaishi katika zama za Ubepari (hata kama ni uchwara) na CCM ambao ndiyo wanaoongoza serikali yetu kwa sasa,lazima wajifunze jinsi ya kuenenda na mfumo huo wa kibepari.
Hoja nzuri japo imejaa CCM CCM CCM,jambo ambalo litapelekea watu kujadili kwa kuzingatia mirengo ya kisiasa.
 
Mbaya zaidi kaleta hoja ikitanguliza uvyama,ccm inakujaje?,suala hili lipo kitaalam na kisheria zaidi za nchi husika na za kimataifa.
Uchangiaji hapa hautakua na weledi,simba na yanga
Sasa kwa nini mambo mazuri inatajwa CCM? Uchama mliuanza zamani wakati nchi bado ni changa!!

Hizi ni sera za CCM na sheria zinakubaliwa na CCM. Umeona dudus katoa hoja za msingi sana lakini alipotaja kusainiwa mkataba wa Buzwagi Hotelini si analeta swali ni nani aliyeusaini mkataba huo?

Halafu anaposema "ahadi za Davos" bila ya shaka anarejea enzi za Kikwete wakati akiwa Rais. Nyakata zote hizo ni CCM ndiyo walikuwa wanasema kwamba tuko kwenye njia sahihi.

CCM imeingia kwa kuwa yenyewe ndiyo inaoongoza nchi yetu kwa sasa na yenyewe inadai inaongoza nchi kijamaa wakati kila tendo la chama hicho linaonesha tuko kwenye zama za ubepari Uchwara.
 
Sasa kwa nini mambo mazuri inatajwa CCM? Uchama mliuanza zamani wakati nchi bado ni changa!!
Tetea hoja yako,kama huwezi kaa kimya upewe taarifa ilionyooka kuhusiana na hoja yako,siasa weka kando kwanza,hapa ni weledi wa sheria na taaluma husika
 
Unapozungumzaia sera lazima uwe unazungumzia chama kilichoko madarakani na mitizamo yake.
 
Hiyo ulioleta ni sera ya ccm au yako ?
Kama CCM wasingekuwa na woga wa Simba na Yanga kumilikiwa na wenye hisa nyingi wangewaambia kina Kiganja wakae kimya. Ni uzembe wa CCM kutokuwaandaa wasomi wa watanzania kushindania nafasi za kazi na wenzao wa Afrika Mashariki, leo hii mjadala wa Sylvia Mulinge usingekuwepo.
 
Back
Top Bottom