CCM: Dr. Slaa awekwe 'busy'

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,105
17,104
Huku kikiwekwa roho juu na harakati za CHADEMA kujiimarisha hadi vijijini,CCM imeapa 'kula sahani moja' na Dr. Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA. Vikao mbalimbali vya kimkakati ndani ya CCM vimeapa kumweka 'busy' Dr. Slaa kwa hoja za majibizano ili kumpunguza kasi ya kiutendaji ndani ya chama. ' Utulivu na kuimarika kwa chama ni uongozi hasa Katibu Mkuu. Hoja ziwe ni kadi za CCM,Zitto na Urais na nyinginezo. Hizi zitatusaidia. Dr. Slaa lazima atatingwa nazo tu' alisema Mjumbe wa CC kwenye kikao ambacho hata Nape Nnauye alikuwepo jana.
 
ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,210
554
Viongozi wa ccm waibane serikali yao juu kuwajibika kwa wananchi,vinginevyo hiyo itakuwa sawa na kuzuia maji kwa neti. 2015 kazi wataiona!
 
Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
1,081
Dr. Slaa kawashika pabaya sana hawa watu!........
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,159
19,146
ukiwa ccm unakuwa na uhakika wa kupata vijihela hata kama ni vya wizi...nashukuru baadhi ya magamba bado wanaipenda nchi ndo maana wanatoa siri za vikao vya wanga
 
Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
538
It is too late and too wrong for CCM to fight against Dr.Slaa.
Kuna vichwa vingi sana kwa sasa ndani ya CHADEMA vinafanya harakati kubwa sana za ukombozi wa nchi yetu kwa sasa.
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,785
9,623
slaa keeps their heads ringing...!!
:laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh:
 
Mkurdi

Member
Dec 6, 2012
18
7
slaa keeps their heads ringing...!!
:laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh:

I also propose to ignore gossips, I suggest to hold on in discusssing future of our generations. Nape and the Rest are hunting for their bread,
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,896
5,295
Wao badala ya kukaa na kujadiliana ni jinsi gani ya kuishauri serikali itatutoa kwenye umaskini tulionao wao
wanatumia muda na vikao kumjadili DR Slaa.Mijitu mingine bwana!

Wanatekeleza agizo la muheshimiwa rais la kupambana na CDM.
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
45,973
57,121
Dr Slaa kama ataendelea kumjibu Nape hizi hoja za kipumbavu nitamdharau sana na nitamuona na yeye ni wale wale, ila nashangazwa sana na waandishi wa Tanzania kumpa airtime Nape kwa habari za Kijinga kabisa, ila wahariri wenyewe kama ndio kina Absalom Kibanda sishangazwi na hali hii.
 
MLERAI

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
668
271
Wao ndio walio na serekali njia ya kurudisha imani kwa wananchi ni kupunguza ugumu wa maisha bidhaa zishuke bei waondoe kodi ambazo si za lazima raia athaminiwe kuliko mwekezaji na waache wizi.
 
Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,292
1,137
Dr Slaa kama ataendelea kumjibu Nape hizi hoja za kipumbavu nitamdharau sana na nitamuona na yeye ni wale wale, ila nashangazwa sana na waandishi wa Tanzania kumpa airtime Nape kwa habari za Kijinga kabisa, ila wahariri wenyewe kama ndio kina Absalom Kibanda sishangazwi na hali hii.

Kuanzia sasa amwachie Mnyika na Heche wa deal na Nape yeye aendelee kukijenga chama
 
Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
Mtabaki kumtetea mtu hata kama hana sifa za uongozi kama vile maadili, utendaji nk!
Hivi Chadema hakuna anaefaa kuwa Katibu Mkuu zaidi ya Slaa? mbona kuna vijana hodari na wachapakazi wenye maadili kama Zito Kabwe?
Chadema kinahusishwa na udini na ukanda! Slaa ni Padre na mlei wa Kanisa aliesaini mkataba wa KIFISADI wa MOU 1992 akiwakilisha Kanisa na Edwad Lowasa kama Waziri ktk Serikali ya awamu ya Pili!

kama mnataka kufuta hisia za kidini Chadema hamna budi kumsimamisha Mgombea urais mwingine mwenye sifa za uongozi!
Slaa ni msalaba wenu na mkiendelea kumlea na kumuenzi, basi mjue Chadema itafia mikononi mwake!
 
KOMBAJR

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
5,829
1,267

Hivi nyie magamba hakuna vijana zaidi ya Mangula,Kinana,Wasira? Dr. Slaa anawaumiza kichwa sana eh? Zitto mbona ni kiongozi tayari.
 
Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,785
1,635
Mtabaki kumtetea mtu hata kama hana sifa za uongozi kama vile maadili, utendaji nk! Hivi Chadema hakuna anaefaa kuwa Katibu Mkuu zaidi ya Slaa? mbona kuna vijana hodari na wachapakazi wenye maadili kama Zito Kabwe? Chadema kinahusishwa na udini na ukanda! Slaa ni Padre na mlei wa Kanisa aliesaini mkataba wa KIFISADI wa MOU 1992 akiwakilisha Kanisa na Edwad Lowasa kama Waziri ktk Serikali ya awamu ya Pili! kama mnataka kufuta hisia za kidini Chadema hamna budi kumsimamisha Mgombea urais mwingine mwenye sifa za uongozi! Slaa ni msalaba wenu na mkiendelea kumlea na kumuenzi, basi mjue Chadema itafia mikononi mwake!
pilipili usoila yakuwashia nini?
 
Kidzude

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
4,429
1,355
Huku kikiwekwa roho juu na harakati za CHADEMA kujiimarisha hadi vijijini,CCM imeapa 'kula sahani moja' na Dr. Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA. Vikao mbalimbali vya kimkakati ndani ya CCM vimeapa kumweka 'busy' Dr. Slaa kwa hoja za majibizano ili kumpunguza kasi ya kiutendaji ndani ya chama. ' Utulivu na kuimarika kwa chama ni uongozi hasa Katibu Mkuu. Hoja ziwe ni kadi za CCM,Zitto na Urais na nyinginezo. Hizi zitatusaidia. Dr. Slaa lazima atatingwa nazo tu' alisema Mjumbe wa CC kwenye kikao ambacho hata Nape Nnauye alikuwepo jana.

Dr Silaa is problem kwa kweli.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
96,514
165,511
Inafahamika siku nyingi tu kwamba bila kumsakama Dr Slaa au Cdm , hutaweza kupata cheo CCM , Mfano mzuri ni Nape Nnauye na Mwigulu Mchemba , taarifa za uchunguzi zinaonyesha pia kwamba ili thread yako ipate wachangiaji wa kutosha hapa JF ni rahisi sana , unatakiwa kushambulia Dr Slaa au Cdm ! Tujirekebishe , tujadili mustakabali wa nchi na wala si mtu mmoja mmoja .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom