Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Imekuwa kawaida kwa chama cha mapinduzi kutengeneza hila za wazi pale inapopoteza jimbo au halmashauri nchini.Wamefanya hivyo Arusha katika uchaguzi wa Meya na kusababisha vurugu zilizopelekea vifo vya raia pale walipotumia mamlaka ya jeshi la polisi kujinufaisha kisiasa. Khali hiyo imetokea Mbeya,Iringa na Morogoro.Hatimaye wamerudi Mwanza.Mhe.Pinda alipozuru jijini Mwanza alizomewa kutokana na utendaji mbovu wa serikali ikiwemo kushindwa kudhibiti mfumo wa bei.Kwa hasira alipozomewa aliagiza halmashauri ya jiji igawanywe yaani Ilemela na Nyamagana.Uchaguzi ulifanyika na ccm walishinda na kuchukua umeya.Kuhusu Ilemela,wameona haiwezekani kushinda basi wamemhonga Henry Matata,Diwani aliyefukuzwa na CHADEMA kwa uchaguzi fake amekuwa Meya kitu ambacho kitaleta vurugu jijini hapa endapo wananchi wataamua kupinga.Chini ya CHADEMA,jiji lilikuwa tulivu na machinga walijiona wapo nyumbani. CCM mnataka vijana wafanye shughuli gani na wapi bila miundombinu? Damu ya Watanzania inawalilia ccm