William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
- Tayari kuna viongozi wameanza kuingiwa na homa kali kuhusiana na hii dharura, ambayo inaaminika kwamba kuna la mgambo nyuma yake!
Field Marshall Es = Wazee Wa Sauti Ya Umeme!
Tanzania Daima
Makanisa yamjadili Kikwete
na Betty Kangonga
VIONGOZI mbalimbali wa madhehebu ya dini wamefanya kikao cha siri na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa madarakani viongozi wote waliohusika katika kashfa mbalimbali kabla ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kikao hicho kinachofanyika Dar es Salaam, kinawakutanisha viongozi wa dini zaidi ya 160 kutoka sehemu mbalimbali nchini wanaotathmini hali ya siasa na kushuka kwa kiwango cha elimu.
Vyanzo mbalimbali vya habari kutoka ndani ya kikao hicho, vililiambia gazeti hili kuwa kikao hicho cha siku tatu kilifunguliwa na kiongozi mmoja maarufu wa dini. Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema viongozi hao walijiridhisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kuwachukulia hatua wanachama wake waliohusishwa na kashfa mbalimbali huku wakiachwa kuendelea na nafasi zao.
Kuna uhusiano wowote na utabiri wa Sheikh Yahya niliousikia leo (Radio Clouds, taarifa ya saa 12 joni)?
-Uchaguzi utaahirishwa
-Karume ataongezewa muda na blah blah nyingine kama kaiwaida ya watabiri
Can these dots be connected?
Kwa nini unayaamini sana hayo magazeti huna habari wakati mwingine source za habari zao zinatoka JF na waandishi wao wengi wapo humu.Tujadili mambo yaliyoandikwa katika ''Mwananchi'',''Nipashe'',''Raia Mwema'',''Majira'',''Uhuru'',''Habari Leo'',''The Guardian'',nk.
Hakuna sababu ya kujadili hizi speculation.
Ganesh,Tujadili mambo yaliyoandikwa katika ''Mwananchi'',''Nipashe'',''Raia Mwema'',''Majira'',''Uhuru'',''Habari Leo'',''The Guardian'',nk.
Hakuna sababu ya kujadili hizi speculation.
Ganesh,
Tuletee hizo issues zilizoandikwa kwenye hayo magazeti. JF ni mahali ambapo habari huvunjika kabla ya kunaswa na hayo magazeti.
Kuna watoto wakisikia wazazi wanaongea wanaenda kusema kwa majirani kinachozungumzwa, au wazazi wanawaambia nenda kaseme?
Nkamangi una maana gani au mleta hoja..............Kuna watoto wakisikia wazazi wanaongea wanaenda kusema kwa majirani kinachozungumzwa, au wazazi wanawaambia nenda kaseme?