CCM Dar yampiga marufuku Samwel Sitta!

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika hali isiyo ya kawaida Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam John Guninita amemshambulia vikali waziri wa ushirikiano Afrika Mashariki Samwel Sitta kwamba anataka kuua chama.

Guninita alitoa shutuma hizo jana kwenye mikutano ya CCM.

Ifuatayo ni sehemu ya hotuba yake kama ilivyonukuliwa na gazeti la majira la leo:

''Viongozi wa namna hii tusiwavumilie hata kidogo mtu kama Waziri Sitta hawezi kukaa kwenye mkutano kama ule na kusema maneno ya namna hiyo ikizingatiwa yeye alikuwa waziri tangu enzi za hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini pia utaratibu wetu ni kwamba mtu akikerwa na jambo fulani anakaa kwenye vikao na kuzungumza hivyo kuzungumza maneno hayo ndiko kunakusababisha chama kishindwe kwenye chaguzi.

"Isiwe kuwa ni hasira ya kuondolewa uspika ndiyo inayo mpelekea kusema hivyo kwani kilichofanyika bungeni ni kutaka 50 kwa 50 kwamba kipindi hiki aongoze mwanamke ambaye ni Mheshimiwa Anne Makinda, hivyo aache kuleta nongwa kwenye chama, ninawaomba ndugu zangu wana CCM mpuuze Waziri Sitta kwani inaonekana ana mipango yake mingine anayoijua mwenyewe," alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema kuwa maneno ya Waziri huyo ni ya kukibomoa chama kwani hajatumwa na Katibu Mkuu Taifa, Bw. Wilson Mukama wala Rais Kikwete na kwamba viongozi hao hawawezi kumtuma maneno ya kubomoa serikali yao na kuuyumbisha umma kama alivyofanya''

Mwisho wa kunukuu......
 
CCM ya siku hizi imepanua demokrasia au ndiyo inavunjika vipande vipande?????
 
Aache kudanganya, na vipi kuhusu NAPE anaye kejeli viongozi wa muafaka wa Z'bar kuwa SHARIFF njaa ndiyo ilimfanya akubali muafaka ili pamoja na mengine alipwe staili zake kama WK msitaaafu, maana SITTA na NAPE wanasafiri pamoja mikoani kwa sasa, hivyo wamepangana kila mmoja la kuongea ili kuwapa watu hamasa ya kuendelea kukipenda Chama
 
Alisema nini

Bill,
Habari yote ya majira ni hii:

Samuel Sitta apigwa 'pini' Dar

Na Anneth Kagenda

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta, ametakiwa kuacha mara moja tabia yake ya kuikashfu ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na utekelezaji
wake kwa kuwa kufanya hivyo ni kuupotosha umma.

Kadhalika, Bw. Sitta ametakiwa kutoitisha mkutano wowote kwa wakazi wa Dar es Salaam hadi apate barua kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete na endapo hatapata aendelee kufanya katika mikoa mingine.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Bw. John Guninita alipofanya ziara katika Kata ya Mbezi na Kata mpya ya Msigani kuzungumza na viongozi wa chama hicho ambapo alisema kuwa pamoja na kutoruhusiwa kufanya mkutano huo, pia Bw. Sitta aache kuleta maslahi ya kunyimwa uspika kwenye chama.

Kauli ya Bw. Guninita inashabihiana na iliyotolewa juzi na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki aliyewazuia Bw. Sitta na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye kufanya mkutano jimboni mwake kuhubiri siasa zao za kuvuana magamba.

Bw. Guninita alisema kuwa hivi karibuni Bw. Sitta alikaririwa kwenye mkutano wake mkoani Mbeya akisema maneno ya 'kuikashfu ilani ya CCM' huku akisema kuwa Tanzania siyo nchi maskini kama inavyoelezeka, eti serikali haijatekeleza ilani na kusema kuwa kufanya hivyo anakuwa hakitendei haki chama hicho huku akiupotosha umma wa Watanzania kwa maneno yake hayo.

"Viongozi wa namna hii tusiwavumilie hata kidogo mtu kama Waziri Sitta hawezi kukaa kwenye mkutano kama ule na kusema maneno ya namna hiyo ikizingatiwa yeye alikuwa waziri tangu enzi za hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini pia utaratibu wetu ni kwamba mtu akikerwa na jambo fulani anakaa kwenye vikao na kuzungumza hivyo kuzungumza maneno hayo ndiko kunakusababisha chama kishindwe kwenye chaguzi.

"Isiwe kuwa ni hasira ya kuondolewa uspika ndiyo inayo mpelekea kusema hivyo kwani kilichofanyika bungeni ni kutaka 50 kwa 50 kwamba kipindi hiki aongoze mwanamke ambaye ni Mheshimiwa Anne Makinda, hivyo aache kuleta nongwa kwenye chama, ninawaomba ndugu zangu wana CCM mpuuze Waziri Sitta kwani inaonekana ana mipango yake mingine anayoijua mwenyewe," alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema kuwa maneno ya Waziri huyo ni ya kukibomoa chama kwani hajatumwa na Katibu Mkuu Taifa, Bw. Wilson Mukama wala Rais Kikwete na kwamba viongozi hao hawawezi kumtuma maneno ya kubomoa serikali yao na kuuyumbisha umma kama alivyofanya.

Bw. Guninita alisema kuwa ikiwa watu wa namna hiyo wataendelea kuachwa upo uwezekano mkubwa wa kukipoteza Chama ifikapo uchaguzi wa 2014/2015 na kusema kuwa hali hiyo inasababisha upinzani kuendelea kujipanga ukiwa na matumaini kuwa wakipata urais basi watakuwa wamemaliza kila kitu.

"Huyu Bw. Sitta mimi nashindwa kumuelewa anapokaa barabarani na kusema adharani kuwa Ilani haijatekelezeka anataka tukienda viongozi tupigwe mawe kwa sababu kufanya hivyo ni kutaka wananchi watuone hatufanyi kazi yoyote ya kuwaletea maendeleo kwani CCM ndicho chama kinachotawala anaposema nchi siyo maskini anamaanisha kwamba viongozi hawawajibiki ipasavyo," alihoji.

Akizungumzia kuhusu kujivua gamba alisema kuwa watu wamekuwa wakipotosha kuhusu neno hilo na kusema kuwa maana ya kujivua gamba ni kubadilisha tabia na wala siyo kufukuzana na kusema kuwa kufukuzana ni kukibomoa chama hicho.

"Nimekuwa nikienda sehemu mbalimbali utawasikia wanachama wakisema mvue gamba huyo katibu, hatuwezi kwenda hivyo kinachotakiwa ni kukaa kwenye vikao, kuelezana, kuelimishana na kusema ukweli mtu akionekana hakubaliani na yale anayotakiwa kufanya hatua zitachukuliwa dhidi yake lakini siyo kwamba mtu anajivua gamba anafukuzwa hata Rais Kikwete hapendi tabia hii," alisema.

Aliwataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanawajibika ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wananchi na kujua matatizo waliyonayo na kusema kuwa kufanya hivyo ndio utakuwa muarobaini wa kukifanya chama hicho kiweze kushika dora
 
aache kudanganya, na vipi kuhusu NAPE anaye kejeli viongozi wa muafaka wa Z'bar kuwa SHARIFF njaa ndiyo ilimfanya akubali muafaka ili pamoja na mengine alipwe staili zake kama WK msitaaafu, maana SITTA na NAPE wanasafiri pamoja mikoani kwa sasa, hivyo wamepangana kila mmoja la kuongea ili kuwapa watu hamasa ya kuendelea kukipenda Chama
Hapo kwenye red, ndo ukweli wenyewe, Big up NAPE. Shariff katumia cuf kurejesha mafao yake tu, vita mbinu bana. Na kwakuwa keshapata alichohitaji sishangai akirudi ccm-A sasa.
 
sitta yuko sahihi, kwani sio kweli kuwa tz sio maskini?, kwani sio kweli kuwa ilani haijatekelezwa ipasavyo?, Guninita anapigania dhana ya kuendelea kuoneana aibu katika maovu! Sitta ni mfano wa kuigwa kiutendaji!

Sitta anaijua vema falsafa ya '' transparency, responsibility, integrity'' kuwa ndio maendeleo ya kweli!

WELL DONE MZEE 6, KANYAGA TWENDE USISIKILIZE MAFISADI HAO!
 
Katika hali isiyo ya kawaida Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam John Guninita amemshambulia vikali waziri wa ushirikiano Afrika Mashariki Samwel Sitta kwamba anataka kuua chama.Guninita alitoa shutuma hizo jana kwenye mikutano ya CCM.
Ifuatayo ni sehemu ya hotuba yake kama ilivyonukuliwa na gazeti la majira la leo:

''Viongozi wa namna hii tusiwavumilie hata kidogo mtu kama Waziri Sitta hawezi kukaa kwenye mkutano kama ule na kusema maneno ya namna hiyo ikizingatiwa yeye alikuwa waziri tangu enzi za hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini pia utaratibu wetu ni kwamba mtu akikerwa na jambo fulani anakaa kwenye vikao na kuzungumza hivyo kuzungumza maneno hayo ndiko kunakusababisha chama kishindwe kwenye chaguzi.

"Isiwe kuwa ni hasira ya kuondolewa uspika ndiyo inayo mpelekea kusema hivyo kwani kilichofanyika bungeni ni kutaka 50 kwa 50 kwamba kipindi hiki aongoze mwanamke ambaye ni Mheshimiwa Anne Makinda, hivyo aache kuleta nongwa kwenye chama, ninawaomba ndugu zangu wana CCM mpuuze Waziri Sitta kwani inaonekana ana mipango yake mingine anayoijua mwenyewe," alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema kuwa maneno ya Waziri huyo ni ya kukibomoa chama kwani hajatumwa na Katibu Mkuu Taifa, Bw. Wilson Mukama wala Rais Kikwete na kwamba viongozi hao hawawezi kumtuma maneno ya kubomoa serikali yao na kuuyumbisha umma kama alivyofanya''

Mwisho wa kunukuu......

Huyu si ni mgombea wao wa urais 2015, vipi tena mambo haya? mnatu-comfuse sisi wananchi.
 
Inachekesha kuona Guninita anamshambulia Sitta kwa kutofuata ngazi za vikao vya chama, huku Guninita akiongea katika hotuba live, bila kufuata ngazi za vikao vya chama.

Hypocrisy of the highest order.
 
Hivi M/kiti wa ccm mkoa anaweza kumzuia Waziri asifanye mkutano kokote kule nchini? Guninita hana ubavu wa kumzuia 6 kama anavyodai, hapo alitaka kuwafurahisha tu magamba waliokuwa wakimsikiliza.
 
ccm cham cha mazuzu***** na watu wenye akili za kawaida na mbaya kabisa, Sitta kilema wa ufahamu, na hao wengine ni watu wasio aminika kabisa, hiko ni chama kinachoangamia ....! kazi yao malumbano,. kelele na rushwa kama si Ufisadi
283509_141022539312971_100002156774748_272727_7021239_n.jpg

Gunia ishhhh Guninita njaa inamuumiza, nadhani anajichimbia kaburi mapeeeema bila yeye kujua anawashika sharubu wazee wa fitna ohoooo
 
Hapa kuna mambo mawili. Alichosema Sitta ni kweli, tatizo ni kwamba kawafumbua macho wananchi wakati wenzake wa ccm wanataka wananchi waendelee kuwa mbumbumbu. Na hivyo hii kutishia ccm kupoteza kura nyingi kipindi kijacho. Guninita angempinga Sitta kwa kusema kuwa Sitta ni muongo maana nchi ni maskini kweli akatoa ushahidi, pia akasema ilani imetekelezwa na si kama Sitta anavyosema kuwa haijatekelezwa. Kwa maniki hii tatizo ni Sitta kuwaeleza wananchi ukweli!!!! This being the case hongera Bw. Six, kama huamini piga hii nikupe ya mdomo 0752 965846
 
Sitta ana chama ndani ya chama, anaweza kusema lolote, kwanza nashangaa eti anakaimugi nafasi ya w/mkuu bungeni.
 
Back
Top Bottom