CCM chama kinachokufa, ili kipone kifanye yafatayo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM chama kinachokufa, ili kipone kifanye yafatayo...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CANCER, Mar 7, 2012.

 1. C

  CANCER Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Kwa hali yoyote ili chama kihesabike kinakua ni pale kinapoongeza wanachama wapya hasa vijana kwa maana vijana ndio watakuja kushika uongozi baadaye.

  Kwa hali ilivyo kwa chama chetu tawala mambo siyo kimepoteza uungwaji mkono kwa wasomi ,vijana na wafanyakazi.nguzo yake imebaki kwa wafanyabiashara wakubwa maana wananufaika kwa kukwepa kodi na kundi jingine ni wakulima ambalo linategemewa sana na chama ccm ili kupata kura zake katika chaguzi zake .Hali inavyoendelea sasa wakulima wengi wameanza kukichoka chama sababu ni mfumko wa bei wa vitu.

  Hivi sasa vitu vingi vijijini kama mafuta, sabuni, chumvi n.k hazishikiki pia mgomo wa madakitari umeongeza machungu na kukomelea mwiba kwenye kidonda. kwa sasa ukionekana umevaa T-shirt za ccm watu wapokuona wanapata kichefuchefu na machungu. chama kinategemea zaidi uungwaji mkono wa watu wote na wanachama kuwa huru kukitangaza chama bila woga wa kunadi sera zake kitu ambacho chama chetu kimekosa.

  Ili kurejesha ari kwa wakulima na baadhi ya watu wa makundi mengine hatimaye kupata ridhaa ya watu bila hila wafanye
  1.Raisi na serikali yake wasimamie watendaji wa ngazi za chiniwanaotafuna fedha za wananchi na kufanya huduma za jamii kuwa mbovu
  2.waachane na program ya kujivua gamba
  3.wavunje makundi ndani ya chama
  4.rais avunje baraza la mawaziri na kuteua wenye uwezo .
  5.watumie hoja kujibu hoja za vyama pinzani badala ya kusingizia
  6.wateue wagombea katika chaguzi kwa kufata kukubalika kwa watu badala ya fedha
  7.wabunge wake watoe hoja na kutetea watuwao badala kuunga mkono hoja
  8.watafute ufumbuzi wa matatizo ya wananchi badala ya kutumia mabavu na polisi
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kikifa kimekufa hakifufuki tena milele
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  kikipona kitakuwa ccm tu
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mi nafikiri kuna illusion kubwa mno
  kama uliiona sherehe za ccm mwanza
  safari bado ndefu
   
 5. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wewe unakuja kwetu, nilitaraji utuambie tayari upo kuhakikisha ccm wanayatekeleza. Au unataka tukusaidie kumpelekea baba riz?
   
 6. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mpaka sasa hivi hakuna mwananchi wa kawaida anayekiamini na kukithamini chama cha mapinduzi, na ni vugumu sana kuvunja makundi katika chama kilichoraniwa na damu za watanzania, leo watu kila sehemu wanateseka na mfumo mbaya wa kigaidi, wenye roho za ibirisi, roho ubinafisi, roho za kiuwaji. Leo hii watanzania wanapata matatizo makubwa raisi kimya. RAISI ni mtua anayeheshimu matatizo ya watu wake, ni mtu mwenye maamza mazuri, mwenye akili za ziada katika maamzi yake, mwenye sympath na watu wake. SIJUTI KUZALIWA TANZANIA ILA NAJUTA KUISHI KATIKA UONGOZI MBOVU
   
 7. T

  Tata JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,735
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Chama Cha Mapinduzi hakifi kama mwandishi anavyodhani. Hiki ni chama dola na kitakufa pale tu dola itakapoondoka mikononi mwake.
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Kipaza sauti cha chama cha maandamano.....tumekusoma.
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hadithi za alfa ulela, bulicheka na Abunuasi bado zipo. CCM haianguki leo
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tumechoka kuona mabaya wa CCM tu hivi vyama vingine 18 vya siasa havina kasoro?

  Tuwe makini kama kweli tuna nia ya kupata chama mbadala wa CCM.

  Nguvu ya vyama vya upinzani haitokani na ubovu wa CCM bali uimara wake.

  upo uezekano wa CCM ikiondoka tukapata CCM tena kwa sababu tunaogopa kuvitupia jicho vyama pinzani kila siku ni CCM.
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ni sikio la kufa hilo wala hawawezi kukuelewa!!!!!
   
 12. C

  CANCER Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  ukitaka kuthibitisa kuwa inakufa fanya tathimini inavyotumia nguvu nyingi kwenye chaguzi na imani ya wananchi kwa serikali yake
   
Loading...