CCM, chama kimoja karne ya 21 ni ndoto za mchana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, chama kimoja karne ya 21 ni ndoto za mchana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Nov 22, 2010.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM wanafanya juhudi kubwa kupita kiasi za kuhakikisha kuwa wanaendelea kuifisadi nchi katika mfumo wa chama kimoja. Kazi yao kubwa ni kuhakikisha kuwa wanadhoofisha vyama vya upinzani. Waliua TLP, wakaua NCCR mageuzi, wameua CUF, sasa wanainyemelea Chadema. Lakini wamechelewa sana, hakuna mtanzania wa karne ya 21 atakayekubali zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM. Ndio maana wabunge wa Chadema mwaka huu wameongezeka mara dufu, na wataendelea kuongozeka. Kizazi cha sasa kinataka Uhuru wa kufikiri na kuamua. Hivi, kuna watanzania ambao bado wanataka kuwekeza ubongo wao kwa CCM ili wawasaidie kufikiri na kuamua? CCM hawawezi kutawala fikra za kizazi cha sasa, chama kimoja karne ya 21 ni ndoto za mchana.
   
 2. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  mwiho wao umefika na kiboko yao ni chadema
   
 3. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani unamaanisha mwisho wa CCM umefika.
   
Loading...