CCM, CHADEMA na CUF live radio wapo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, CHADEMA na CUF live radio wapo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiby, Apr 7, 2011.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Wawakilishi wa vijana katika vyama vya ccm,chadema,cuf wanaunguruma radio wapoFM 98:0 live wakijadili mambo mbali mbali yanayohusu vyama vyao.
  Tutawajuza zaidi kwa kadri tutakavyofuatilia.
  .
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe sema tuwashe redio zetu. utatujuza maana yake nini?

  kwani umeambiwa sie hatuna redio?
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Wanajadili nini?
  Kwani cuf na ccm kuna tofauti gani?......siamini km wanaweza kupingana kwa hoja za msingi najua hapo itakuwa chadema vs ccm and cuf (ccm-b)...
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Babu wa cuf anasema kile vijana walichokuwa wanalalamikia na kuiondoa serikali ya Misri madarakani kipo pia hapa tanzania.
  Tuna, umaskini,ufisadi nk na pia anamlipua mtu mwenye dhamana serikalini alikutwa na pesa bank cha nje na alisema ni vicent tu hivyo.
  Watoto wa Tz wanauza ndizi badala ya kwenda shula kwa sababu ya umasikini.
  -mihogo ni chakula kilichopewa jina la kikwete.
  -umeme unawaka kwenye migodi ya wageni ilhali wenyeji hawana.
  -anazungumzia matatizo yanayosababisha migomo vyuo vikuu.
  -anatoa wito kwa serikali watatue matatizo yao.
  - mitaani yanasemwa kuwa Jk ndie rais dhaifu tuliewahi kuwa nae. Anatolea mfano wa kumzuia magufuli kuvunja nyumba za walio katika eneo la barabara na kesho yake anatoka na kauli nyingine ya kuruhusu zibomolewe.
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Mbona anapingana na viongozi wake wa cuf na ccm na waislamu wanosema maandamano ya huko uarabuni ni haramu?.................si ahamie cdm tu maana yuko tofauti na itikadi ya viongozi wake

   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,688
  Trophy Points: 280
  Nimewasikia wanasema eti MIHOGO imepewa jina jipa.....MIKATE YA KIKWETE hahahahaha
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Chitanda wa chadema.
  Anasema kile kinachotokea kwa wenzetu kitatokea hapa Tz.
  -Tz sii masikini ila viongozi ndio wameifanya nchi kuwa masikini
  - tufike mahali tukubali kuwa serikali hii imechoka na haiwezi kuleta mabadiliko.
  -sera za mikopo zinabagua, na mtanzania hana haki ya kukopeshwa
  - mambo yote tunayoyataka yateletwa na katiba.
  - mabadiliko ya katiba yakiruhusu manunguniko yatasababisha mpasuko wa taifa
  -lazima katiba ya Tz ijadiliwe na watu wote na wala sii kundi moja wala taasisi fulani
  -lazima katiba izungumzie tume ya uchaguzi.
  -mfumo wa uchaguzi sii mzuri na unaruhusu rushwa kama zawadi kwa wapiga kura.
  -kilimo ni lazima kiendane na elimu kwani elimu ni suluhisho la matatizo yote.
  -wazee wote wastaafu lazima watibiwe bure, na wazee sii tu wale waliokuwa wameajiriwa serikalini bali pia na waezee wakulima.
  .
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Huyu kaongea la maana........

   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Sanda wa ccm.
  -anawashauri wenzake wazungumze kwa takwimu na ushahidi, na kuhusisha mambo ya kwetu na yanayotokea A. Kask ni kuchochea.
  -kuna kukua kwa ufahamu na hivyo ni changamoto na kiwango cha kuwa mkweli.
  -uadilifu na ukweli ni jambo ambalo kwa sasa halikwepeki.
  -uvccm na ccm sii tu kwamba wametulia baada ya kushika dola hapana, bali wapo tayari pia hoja zote zinazotolewa na wenzetu.
  -tunawasikiliza wale tunaowatumikia na tunayatendea kazi.
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaaaaaa..........mwana ccm anazungumzia uadilifu?..........siamini kweli siasa ni mchezo mchafu kupita kiasi...


   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Umeambiwa kituo kinachorusha hayo matangazo na frequence zake, sasa ulitakaje? Kama unaredio si ufungue? Nani kakwambia huna redio? Acheni ujinga wenu wa kuharibu mada za msingi na kutupepeleka kwenye upuuzi. Umetumwaaa nini!?
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Tujuzeni bana hiyo wapo redio huku haishiki!
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Chatanda chadema.
  Vijana wa vyama hutuna mausiano mabaya, hatugombei fito.
  -wakati umefika wa kuweka uzalendo mbele.
  -unakuta mtu anasaign mikataba mibovu na hii inaonyesha jinsi kusivyo na uzalendo.
  -ccm wasifikiri kwamba ndio wao tu wenye haki ya kuongoza nchi wenyewe, hata ndani ya chadema akiwepo fisadi ni lazima aondoke.
  -sii lazima chadema waandamane ndio ccm wajue sukari imepanda bei. Sasa ni wakati wa wananchi kuiondoa serikali ya ccm madarakani.

  .
  E. Sanda ccm.
  Sioni kama kuna mahusiano mazuri.
  -sisi kama wanaccm tunaunganishwa na kanuni.
  -hofu ya maandamano ya chadema hayaonyeshi kama kuna mahusiano mazuri.
  - sina matatizo na chitanda wala babu ila tunatofautiana tu kwenye itikadi ya vyama vyetu.
  -ccm inajenga mahusiano na vyama mfano anc ya south .A.
   
 14. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Angalau anajua kutembea ktk yale yaliyokuwa ktk Ilani ya Chama chake na kusherehesha hoja kwa kuelezea kitu halisi kilichopo.

  Muwaulize wa CCM na CUF wanayosema yamo ktk Ilani za vyama vyao?
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Babu wa cuf.
  -hatuna mahusiano mazuri na ccm.
  Ccm kwa matendo yao ya kutaka tu kunyakua dola hili limefanya tusiwe na mahusiano na ccm. Wala hatutataka kuwa na mahusiano nao.
  -kwa upande wa vyama vingine vya upinzani tuna mahusiano nao mazuri.
  - chadema nao hatuna nao uhusiano mbaya ila tunatofautiana tu kimtizamo.
  .
   
 16. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Babu-cuf.
  -kiongozi tunaemtaka sisi nikiongozi kijana, ama awe kiongozi mwenye mawazo ya ujana.
  .
  Chitanda.
  -hatuhitaji kiongozi kutoka kundi lolote ila watunataka raisi ambae ni mzalendo kweli kweli mwenye kuonekana kwa watu wote kwamba ni mchapakazi na mwenye kuchukia rushwa.
  .
  E. Sanda.
  -sitatofautiana sana na chitanda. Tungependa rais awe na kama umri wa miaka 41. Itapendeza kama atakuwa na umri mdogo kuliko huyu tulie nae. Kwa upande wa jinsia awe ni kutoka kokote.
  -tumetoka tu kwenye uchaguzi tuyaache kwanza haya ya urais.
   
 17. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  muache atujuze-maana kuna wengine hio redio haitufikii tulipo
   
 18. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Babu wa cuf anajikomba kote kote................ccm na chadema..........mtaka yote kwa pupa km cuf mwishowe hukosa yote..........washike sana walichonacho yaani ccm waishikirie ili wasijekosa vyeo
  \
   
 19. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Sanda-ccm.
  -maamuzi mengi yanayotekelezwa na chama yana mkono wetu sisi kama vijana.
  -sii rahisi kutaja moja moja kwani tunapokuwa kwenye kikao cha maamuzi tunakuwepo wawakilishi wa vyama vyote na hatusemi ni maamuzi ya jumuia fulani bali ya chama.

  .
  Babu -cuf.
  -chama kinataka kufanya marekebidho ya katiba ili kuongeza uwakilishi wa vijana katika vikao vya maamuzi.
  - hili limetokana na enfluence ya vijana.
  -naona niishie hapo maana yapo mengi tuliofanya kama vijana ila sitaki nionekane najivuna.
  .
  Chitanda-chadema
  -tunaweza kupeleka hoja kama vijana katika vikao vya maamuzi lakina likishapita haliwi ni la vijana bali maamuzi ya chama.
  -vijana kwenye vyama vyetu tunamichango na tunathaminiwa.
  .
  Chitanda-chadema.
  -umefika wakati ccm wakae pembeni. Wamekosa uadilifu.
  -chadema tulilalamika kuhusu kodi za manyanyaso, ilifikia mahali serikali ikasalimu amri.
  -ada ya shele kuondolewa na inawezekana kusoma bure, sasa wameondoa angalau watoto wa shule za msingi wanaruhusika kwenda shule hata kama hawana hela.
  -ndio maana tunasema ccm watupishe ili tuwaganyie mambo watanzania ambayo ccm imeshindwa kuwafanyia kwa miaka itapendeka 50.
  -ccm hawawajibiki na tuna tofauti katika sera, mipango na mitizamo.
  .
  Babu cuf.
  -cuf ndio chama peke yake makini Tz.
  -mkapa alisema hakuna chama chochote kufanya siasa. Kafu tukaandamana na kufanya siada, na baada ya hayo benjamin kasalimu amri na kuruhusu vyama kufanya siasa.
  -viongozi wa cuf ndio pekee waliofungwa gerezani na hii ni kuonyesha ni chama gani kinasumbuliwa na serikali na ni kwa sababu ya umakini wao.
  -viongozi kutoka ccm hawawezi kukimbilia cuf ila watakimbilia vyama vingine maana wanafahamu ukali wa cuf kuhusu fisadi.
  -cuf hatujapatakusaidiwa na mwanachama wala kiongozi yeyote wa ccm.
  -kuunda serikali na ccm sii hiari ya cuf bali kura za wananchi kuwataka waunde mashirikiano.
  -katika kushirikiana kuiondoa serikali sii tu kwa cuf bali hata kwa wenzetu.
  -chedema walishirikiana na ccm huko kigoma na huu ni kushirikiana pia. Maana niyake ushirika sii sisi tu cuf tumeanza.
  .
  sanda-ccm.
  -tuliona wanaoumia ni wananchi na tukafikia kwamba tuwaendee wananchi na tuone namna ya kuondoa hali hiyo.
  -hali ya sisa ya sasa ya zanz ni nzuri zaidi na hili lisingekuwa hivi kama kusingekuwa na ushirikiano.
  .
  Chitanda chadema.
  -hatubezi ushirikiani ila tunasema baada ya masuguano mmekubali ili tu yaishe.
  -kuhusu Kigoma.
  -kuna sheria za halmashauri na hivyo kama imeshindikana ndipo tulipofikia uamuzi wa kuongoza 1/2
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Ccm na cuf wanasisitiza kuwa chaguzi zote wamekuwa wakishinda.
  -cuf anasema wameshinda chaguzi zote kuanzia 1995 hadi uchaguzi wa mwaka jana pia walishinda.
  .
  Sanda-ccm.
  -ccm inakubali kuwa kuna haja ya kuwa na elimu ya msingi kabla ya kujiunga na chama.
  -kwetu tulipitia chipukizi na pia jkt na kwa sasa tuna mikakati ambayo tunayo ya ss ambayo sotayasema.
  .
  Babu-cuf
  -sisi ni chama cha siasa ambao tunataka kuingiza wanachama na wanachama hawapewi cadi ila wananunua.
  - wakiisha kufanya hivyo basi sis kama chama tunawataka wanachama waende kwenye matawi yao wakajiandikishe na hivyo imetufanya cuf kuwa na nguvu.
  .
  Chitanda-chadema
  -kadi zetu kwa nyuma zina maelekezo ya kuwaelimisha ni nini cha kufanya baada ya kujiunga na chedema.
  -chedema hatusemi watu wakasome kwanza kabla ya kujiunga na chama kwani wananchi wana uelewa na wanazifahamu haki zao kwa kiwango kikubwa..
  .
  Mwsho.
  Wajumbe wanatoa shukrani zao na wanawaomba watu wajitokeze kujiunga na vyama vyao ili kupata fursa ya kugombea uongozi wa sehemu mbali mbali.
  .
   
Loading...