CCM badilikeni nendeni kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM badilikeni nendeni kwa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Mar 6, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ningependa kuona viongozi wa CCM wakiandaa majukwaa ya siasa waliko wananchi na kuyatumia kuwaambia kuwa Chadema wanachosema ni uongo badala ya kukaa maofisini Dar na kuita waandishi wa habari ghorofani na kulalamika kwao.


  Kwa sababu Chadema ni waongo na wanataka wananchi waichukie serikali yao kwa mambo yasiyo na msingi, basi ningependa kusikia yafuatayo aidha yakitolewa na Makamba, Chiligati, Tambwe Hiza au Mwenyekiti wa CCM na si vitisho.
  1. Si kweli madai ya Chadema kuwa sukari imepanda.........hii imetokana na sababu zifuatazo 1,2,3......kwa misingi hiyo serikali inafanya juu chini kuboresha uzalishaji na wakati huo huo serikali imeagiza tani kadhaa kutoka nje.
  2. Si kweli tena kuwa bei ya umeme imepanda........hii inatokana na maji kupungua kwenye bwawa la Mtera na la Nyumba ya Mungu, lakini wakati huo huo serikali ya CCM imeagiza mitambo yake mipya ya kuzalisha umeme.
  3. Suala la Dowans liko mahakamani na litaamuliwa na mahakama ndiyo maana NEC-CCM imeamua walipwe kwa sababu 1,2,3......
  4. Kupanda kwa gharama za maisha ya mtanzania....ni kweli/si kweli... hii inatokana na hali halisi ya kupanda kwa bei ya mafuta duniani ambayo serikali ya CCM haina uwezo nayo na.........
  5. nk.nk.
  Haya ndiyo majibu ambayo tulitegemea sisi wananchi kusikia kutoka kwa chama kikongwe kilicho makini, lakini badala yake tumesikia vitisho vikitolewa kwa viongozi wa Chadema wanaofanya siasa kuikosoa serikali kwa mujibu wa katiba ya nchi.

  CCM isi-take for granted kwamba malalamiko yanayotolewa na Chadema majibu yake ni rahisi na yanafahamika kwa wananchi kama wao (viongozi) wanavyoyafahamu wanatakiwa waje watufafanulie kwanini hali iko hivi.

  Ushauri:

  Dunia inabadilika na mifumo yake yote ikiwemo ya kiutawala, mifumo ya kiutawala ya zamani (serikali imesema) imepitwa na wakati. Sasa tuko kwenye mfumo wa 'wananchi wanataka' si serikali inataka refer mabadiliko ya mashariki ya kati.

  Pamoja na CCM kuyaona hayo bado viongozi wake wanadhani serikali itaendelea kuwatawala wananchi kwa mfumo wa zamani, ndiyo maana badala ya CCM kama chama kinachotafuta ridhaa kwenda kwa wananchi na kuongea nao kinaitumia serikali kuwatisha wananchi.

  Matokeo yake ni nini, wananchi hawatatenganisha chama na serikali wanapoichukia serikali kutotenda haki (mfano polisi) chama kinapunguza mvuto kwa watu hasira yake inaishia kukiadhibu kwa kukinyima kura.

  Wito wangu kwa CCM ni kubadilika kwenda na wakati kuacha siasa za maofisini kwa kutegemea serikali itafanya kazi za chama, ingawa ni serikali ya CCM lakini kuna siku serikali nayo itachoka kama zilivyokuwa serikali za Misri na Libya. NENDENI KWA WANANCHI msitegemee mtaji wa kura za mwaka jana eleweni hata mtaji huwa unakua na kufa.

  Shukrani naomba kuwasilisha.
   
 2. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kaka umesema ndugu yangu
   
 3. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  duh! Kweli tupu! Kwa bahati 'think tank' ya chama chetu kipendwa is gone! They r there 2 loose......and I'm afraid it gonna be forever!
   
 4. ambili

  ambili JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mi naona badala ya kutumia kodi zetu kujisafisha kwa kufanya mikutano ni bora wangezitumia kujenga ward mpya na kununua vitanda vya hospitali za wilaya maana niliwahi kumpeleka mgonjwa m'nyamala hospitali juzi kati flani, cha kusikitisha alilazwa mzungu wa nne na ward zilikuwa zimejaa sana. kwa kweli iliniuma sana. Natamani hiki chama cha Chaka Chua Matokeo king'oke madarakani.
   
 5. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Luteni, hapo juu umewaeleza vizuri ccm nini cha kujitetea, je watasikia?
  Akina JeyKey hawawezi kusema lolote hapa.
   
 6. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakuna Mbunge wa CCM aliye msafi hata mmoja
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndiyo ambili nakubaliana na wewe kwenye bold lakini kwa chama cha siasa mikutano ndiyo roho yake kutokutana na wanachama kwa kuogopa gharama ni kuua chama.
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Waende kwa wananchi wakiwa na hoja gani?
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Bado kuna watu wenye mapenzi na CCM na wanaendelea kukishauri ingawa hawasikilizwi mfano kina Sumaye, Butiku nk kuna siku nao watachoka na kuanza kushauri vyama vingine kwa uwazi zaidi.
   
 10. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,726
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280
  Kweli waende kwa wananchi wakiwa na hoja gani? Wanachotakiwa kufanya ni kutekeleza mahitaji ya wananchi period. Chadema inatosha kuwaamsha wale waliolala usingizi kwamba ccm inafaa wakati bado wanalala njaa hakuna hospitali, barabara mbovu, shule hazina madawati huku wabunge waliowachagua wakijineemesha kuwa na wake watatu watatu waume wanne wanne magari matatu ya kifahari nyumba za kifahari etc. wajue ndio hao waliowapigia kura kwa kutokujua wanawapa kula. Watanzania tumechoka na upuuzi wa ccm
   
Loading...