CCM Arusha imefanza nini???

CCM Arusha imefanza nini???

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
Kwa ufupi....
CCM watafakari sana hatima yao....
Kwanza tukio la Arusha sijui imewafunza nini... lakini mi naona la kwanza kuwa walikosea mahesabu... kama walimtumia aliyerusha bomu na risasi ili kuvuruga uchaguzi uliokuwa ufanyike 16/06, sasa ndo wamechemka mara kumi, kura ambazo wangepata 16/06 zimehamia tayari CHADEMA kwa uchaguzi wa 30/06.

Pili, sijui kama wamejifunza kitu kuwa wameishiwa sera hadi imefikia hatua ya kutishia na silaha.. mbaya zaidi kuhusiana na tuko hilo hilo bosi wao mmoja ameidhinisha piga, ua.... lakini hiyo kete ya piga ua sijui itawapeleka wapi????
 
Usihofu, hiyo ndiyo style ya CCM kukata roho! Wako hoi na mahututi! Dawa zote walizokuwa nazo za udini, ukanda, ukabila na ugaidi hazifanyi kazi tena! Wako ICU wakipumulia mashine ya polisi na mahakama!! Tumaini lao la mwisho sasa ni mabomu!! Lakini dawa hii nayo haitafanya kazi. Kaburi linawasubiri kwa hamu!!!
 
tutafakari kwa hesabu zao za ngumbaru hivi angakufa mwakilishi wa papa ni nini kingetokea kwa tanzania?
 
Nzuri zaidi ni kuwa hawajui kuwa wanazidi kushindwa kila wakitumia njia za kuwaogofya watu!!!!!!
 
Samahani tarehe 30/6 kwani nani kakuambia kuwa kutakuwa na uchaguzi? subiri uone kwani nijiavyo mimi hakutakuwa na uchaguzi mpaka 2015
 
Na hii mbinu yao ya Mabomu ndio mbaya zaidi kwao kwani inawaamsha wananchi waelewe Serikali yao ya CCM ni Dhaifu kiasi kwamba haiwezi kuwalinda kwa hiyo haina Uhalali wowote wa kuendelea kuongoza Nchi.
 
Kichapo chao kwenye sanduku la kura kpo pale pale
 
hv iliishia wp wale waliokuwa wanataka kuja kujiunga chadema waliokuwa wagombea wa ccm arusha ?
 
Back
Top Bottom