Ndugu yetu, Daktari wa Filosofia uliyetumainiwa na wenazako hata ukasimamia Chama cha Magwiji wasomi UDSM (UDASA), yaani ndani ya viatu vya kina Prof Chachage, Leo hii bila hiana, unakacha misimamo wako Wote, unakumbatia misimamo wa watu wengine na kutumia hoja dhaifu kuutetea! Umenishtua sana!
Inakuwaje licha ya kushiriki kikamilifu mijadala yote rasimu ya kwanza na rasimu ya pili, kushiriki na kuandika mawazo ya kitaaluma, yaliyowakilishwa kwenye Tume, Leo hii unayakimbia! Wewe na wenzako mmedanaganya Tume, mlijenga hoja nzito mkaziweka kwenye kijarida na kuwakabidhi Tume, sio Mara moja Bali Mara mbili, Tume ikazikubali, Leo unawajeuka? Leo unahoji dhana iliyotumika katika utafiti, eti 'sampling'? Mbona hata Mara Mmoja hukusita wala kuhoji Tume ilitumia dhana gain katika utafiti wake? Kweli Michael, umepewa nini Hadi ukubali kuonyesha na kujidhihirisha mbele y kadamnasi yote kuwa unaweza ukawa msaliti kiasi hicho?
Wana Jamvi namhoji Huyu Ndugu yangu maana yeye huko nyuma wakati wa kukusanya Maoni Alikuwa mbele sana na hata kuonekana Kama shabiki wa Tume, na hoja nyingi zilizoko kwenye rasimu zinatokan na mawazo ya Wanataaluma wa Vyuo Vikuu vya Umma, Michael akiwa mojawapo wa viongozi Hao! Je tuwavumilie wakahaba wa hoja/taaluma? Je Kwa nini tusiamini kunmekuwepo na rushwa kubwa iliyoweza kuwashawishi wasomi wa aina ya Dr Francis na kina Prof Malymkono hata wasione Aibu mbele ya jamii Kwa kushabikia hoja wasioiweza kuiwekea mishiko?
kwa nini tusiibue hoja kuna rushwa inatembezwa ili kupata katiba? Je katiba itokanayo na rushwa sio rushwa Mara Mia zaidi. Ni nani atamjibia Dr Francis? Hivi atuthubutu kurudi na kusimama darasani anafundisha? Nchi yangu Tanzania inakwenda wapi?