VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Jana,kulifanyika kikao hapa Ofisi Ndogo za CCM-Lumumba cha kutathmini hali ya kisiasa hapa nchini kwa hivi sasa na kuandaa mwongozo wa kipi kifanywe na Wabunge wa CCM ilimkuhakikisha Bajeti ya Serikali inapita bila mawaa Bungeni Dodoma. Ikaundwa timu ya kishushushu kwenda Dodoma kufuatilia Wabunge wote wa CCM walio 'watukutu'. Nami nimo kwenye timu hiyo. Nitaelekea Dodoma baadaye kidogo ya leo.
Katika kikao cha jana,wajumbe wengi wa kikao walionesha kufurahishwa kwao na jinsi CHADEMA ilivyoelemewa na kesi ya ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA,Winfred Lwakatare. Wakadai kuwa sasa CCM inapumua na kufanya mambo yake kwa utulivu.
'Sasa tunapumua. Walizidi kutubanabana hawa CHADEMA.Kombora moja tu,chali!' alitamba mjumbe mmoja ambaye pia ni Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya CCM toka mkoa wa Dar es Salaam.
'Nasi tupate nafasi sasa ya kuelezea sera na miongozo ya chama kama itupasavyo. CHADEMA wakikukuruka,wapigwe kombora jingine' alishauri mjumbe huyo wa kikao aliyekuwa akishangiliwa kwa nguvu muda wote. ' CCM ni chama dume,hakiwezi kutishwa na chama cha 1992. Sasa wajitoe kwanza kwenye ugaidi ndipo warudi kwenye ulingo wa siasa.Hata Bungeni safari hii watakuwa wapole' alitamba mjumbe huyo wa kike
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (baadaye Dodoma 'kikazi')