CCM: Afadhali tunapumua sasa!

CCM: Afadhali tunapumua sasa!

Jana hukuona kadi za CCM,wanaloliondo wakizisigina chini ardhini?bajeti la govt ya ccm ni uozo mtupu kwani huishia kwenye karatasi bila kupeleka pesa inapohitajika
 
Juzi nilikuwa kijijini kwetu mkoani Tanga wilaya ya mkinga, nikiwa natekeleza kilimo kwanza kwa vitendo kwenye zoezi la kupanda mbegu. Nikawachokoza vibarua niliowapa kazi wanawake kwa wanaume, kwamba inasemekana watu wa vijini ndio mtaji wa CCM, almanusura waniachie zoezi la kuotesha kuliko kuwasingizia kwamba ndio wanaoichagua CCM. Sasa najiuliza hawa CCM wanashindaje? Ila huo wizi wenu ndio mwisho wenu 2015 kwa elimu ya uraia niliyoitoa kwa vijana hao wa kijijini kwetu.
 
Mkuu jana si ndio nusura ngumi zichapwe UVCCM na mwenyekiti kutimkia kwa Nape Kwa ulinzi zaidi hebu tujuze.
 
Kweli mnapumua maana naona mmeishatoa leseni ya uchimbaji wa Uranium...

Endeleeni kupumua maana kupumua kwenu ndio maafa kwa wanyamapori wetu toka kwa Mzee wa Maangamizi Kinana
 
Pro CHADEMA wanavyopenda kulishwa ujinga! Utawaona watakavyojazana hapa!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Kweli Viroba ni Sumu.Saa hizi uko wapi?
 
Mungu aliwaumbua hadi watumishi wake aliowapenda. Mfano Mfalme Daudi alizini na mke wa mtu (mwananch wake mwanajesh), akampa mimba, mfalme kuona vile akamwita mwenye mke toka vitani aje nyumban akiamini ata DO na mkewe ili ampakazie mimba, jamaa alipokuja hakwenda kulala kwa mkewe, dili likabumbuluka. Kete ya mwisho ilikuwa ni kumuua jamaa ili mfalme ajihalalishie kwamba ameoa mjane, kumbe alishamjaza mimba. Mfalme akaua kweli. ADHABU TOKA KWA MUNGU: Yule mtoto akafa na Mfalme alipinduliwa. CCM ilipendwa na MUNGU ila kwa madudu haya. Wallahi HAIPONI
 
Jana,kulifanyika kikao hapa Ofisi Ndogo za CCM-Lumumba cha kutathmini hali ya kisiasa hapa nchini kwa hivi sasa na kuandaa mwongozo wa kipi kifanywe na Wabunge wa CCM ilimkuhakikisha Bajeti ya Serikali inapita bila mawaa Bungeni Dodoma. Ikaundwa timu ya kishushushu kwenda Dodoma kufuatilia Wabunge wote wa CCM walio 'watukutu'. Nami nimo kwenye timu hiyo. Nitaelekea Dodoma baadaye kidogo ya leo.

Katika kikao cha jana,wajumbe wengi wa kikao walionesha kufurahishwa kwao na jinsi CHADEMA ilivyoelemewa na kesi ya ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA,Winfred Lwakatare. Wakadai kuwa sasa CCM inapumua na kufanya mambo yake kwa utulivu.

'Sasa tunapumua. Walizidi kutubanabana hawa CHADEMA.Kombora moja tu,chali!' alitamba mjumbe mmoja ambaye pia ni Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya CCM toka mkoa wa Dar es Salaam.

'Nasi tupate nafasi sasa ya kuelezea sera na miongozo ya chama kama itupasavyo. CHADEMA wakikukuruka,wapigwe kombora jingine' alishauri mjumbe huyo wa kikao aliyekuwa akishangiliwa kwa nguvu muda wote. ' CCM ni chama dume,hakiwezi kutishwa na chama cha 1992. Sasa wajitoe kwanza kwenye ugaidi ndipo warudi kwenye ulingo wa siasa.Hata Bungeni safari hii watakuwa wapole' alitamba mjumbe huyo wa kike

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (baadaye Dodoma 'kikazi')
Wanapumua au WANAPUMUWA?? Maana nijuavyo mimi kupumuwa ni kutoa hewa chafu kupitia njia ya haja kubwa.
 
Ahueni ya haya mambo ni kuhakikisha yafuatayo:

1. Spika na Naibu spika, Mawaziri na manaibu wao wasitokane na wabunge.

2. Kuondoa ubunge viti maalum .
 
Tunakuaminia sana mkuu.Unapoteaga saaana lakini ukiibuka huko ni kama kombora. Asante kwa tahadhari.
 
Back
Top Bottom