CCM Adui Yenu si Ukawa. Ni Maisha Magumu ya Watanzania

amilyroley

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
621
1,199
CCM wanaweza kujidanganya kuwa adui yao ni Ukawa na Lowasa. Adui yenu ni mazingira magumu ya maisha ya wananchi ambayo mliyatengeneza nyie. Muda huu kila mtanzania Analia hali ngumu, mnajitahidi kuokoa jahazi kwa utafiti wa kuwahadaa ila hali halisi inayowafanya waamini mabadiliko ni hali ngumu ya maisha na sio Lowasa.

Wananchi wamepigika kweli na wamechoka sasa ndio maana hawasikii hawaelewi. Tafiti zenu zikitangazwa zinawafikia asilimia 12 tu ya watanzania na haziondoi hali halisi ya maisha magumu ndio maana hawaelewi hawasikii.

Hasira zao za maisha magumu watazionyesha kwenye sanduku la kura na sio kusikia tafiti mnazozigharimia.
 
Back
Top Bottom