CCM Acheni kuihodhi Tanzania

Dangote anataka kuwekeza anapelekwa Lumumba, anataka kufunga kiwanda, CCM wanasema aende, analeta magari 600 CCM wanasema "hii ni aibu kwa UKAWA" bila ya hawa watu kujua kwamba hata wanaowapinga ni watanzania kama wao walivyo watanzania, hii nchi haitaendelea abadani.

Mzee Mwenyewe aliwaita watu "malofa" na "wapumbavu" akatetewa weee mpaka mbingu ikashusha mvua. Na yule mwingine anamwita mtumishi wa Serikali kichaa na anaendelea kudunda kama kawaida. Kama neno "B.w.e.g.e" lilileta taharuki nchi nzima,inakuwaje mtu aitwe kichaa watu waone kawaida, Au kwa kuwa limetamkwa na mwana CCM?
 
Kwa kweli inauma sana ila naamini ipo siku Mungu atatengeneza njia
Yaani viwanja vilijengwa na watanzania wote wao wameviteka na kuvigeuza mali yao na wala nafsi zao haziwashitaki kuwa wamedhulumu jasho la watanzania wenzao. Hawa jamaa walitaifisha mali za TAPA na kuzigeuza zao. Ni kama sasa hivi wajimilikishe shule za kata.
 
Aliuawa Dr. Sengondo Mvungi,aliuawa Daudi Mwangosi alijeruhiwa Dr. Steven Ulimboka na hata Ben saanane hajulikani alipo ni kawaida na wala roho haziwastuki kwa kuwa si wana CCM wenzenu.
 
Chedema lazima wahojiwe aliko Ben saanane kwani wamekuwa wakituaminisha yuko salama.
 
Zitto Kabwe alikuwa mwanachama wa CHADEMA na bila shaka mpaka leo pengo lake linaonekana ndani ya chama vilevile Dr Slaa wanamchango mkubwa sana ndani ya historia ya CHADEMA mbona siku wameondoka hajawagawia Mali za chama ,hawana jasho lao humo, hiyo siyo dhuluma. Kama unashida na viwanja nenda CCM
 
Unajua hizo unazoziita za CCM zingine zilijengwa kwa mikopo ambayo mingine mpaka leo inalipwa kwa kodi za watanzania wote.
Viwanja vilijengwa na CCM au vilijengwa zama za chama kimoja kwa kutumia kodi za wananchi?
 
Mleta Uzi huu uko sahihi 100% !mmejifanya mungu mtu?mfalme nebkadreza alipotia unajisi hekalu la bwana mungu aliandika ukutani MENE MENE TEKERI NA PERESI utawala wenu umepimwa kwa mizani subirin kwenda kondeni mle majani Na kunyweshewa Na umamde!katu dhuluma hii haitawaacha salama,!!
 
Mungu siyo mjinga ndiyo maana anawafanya Watanzania waendelee kuiamini CCM kwa kuwa Hamna hoja za maana mnaishi kwa matukio kama sasa mnalaum Dangote kwenda Lumumba ni hoja nyepesi sana, Mzee Mkapa kusema marofa alikwambia ametumwa na CCM aseme na hii inaadhili VP utendaji wa selikari ya CCM kwa wananchi wake
 
Dangote anataka kuwekeza anapelekwa Lumumba, anataka kufunga kiwanda, CCM wanasema aende, analeta magari 600 CCM wanasema "hii ni aibu kwa UKAWA" bila ya hawa watu kujua kwamba hata wanaowapinga ni watanzania kama wao walivyo watanzania, hii nchi haitaendelea abadani.

Mzee Mwenyewe aliwaita watu "malofa" na "wapumbavu" akatetewa weee mpaka mbingu ikashusha mvua. Na yule mwingine anamwita mtumishi wa Serikali kichaa na anaendelea kudunda kama kawaida. Kama neno "B.w.e.g.e" lilileta taharuki nchi nzima,inakuwaje mtu aitwe kichaa watu waone kawaida, Au kwa kuwa limetamkwa na mwana CCM?
Umekata viroba sasa unashushsha na vipande vya nanasi unaongea kama mtu aliekata tamaa.Hata chadema wangekuwa madarakani wangeongea lugh hiyo hiyo
Kama mliweza kuchagua kambi rasmi ya upinzani bungeni bila ya kushirikisha wenzenu,mkichukua dola mtamsikiliza nani nyie wasanii?
 
Nikiyaangalia matukio yaliyotokea hivi karibuni na kukumbuka yale yaliyowahi kutokea hapa nchini mwetu kwa upande wa Siasa, nimefikia hitimisho kwamba ili nchi hii isonge mbele ni lazima CCM iache fikra na matendo ya kuhodhi nchi yetu ya Tanzania kama ni mali yao peke yao.
Mimi na mawazo tofauti, ni bora kwa CCM iendelee kuihodhi Tanzania inavyotaka kuliko kumkabidhi Bikira Maria kuwa Msimamizi wa Jamhuri ya Muungano wa,Tanzania. Nchi itaingia nuksi, kunakamizwa, kugharikishwa na kuangamizwa
 
Kwani hiyo CCM sasa hivi iko chini ya nani? Ukijua jibu lake hapo ndipo utajia kama tayari imeshatwaliwa na huyo unayemwogopa au la.
 
Zitto Kabwe alikuwa mwanachama wa CHADEMA na bila shaka mpaka leo pengo lake linaonekana ndani ya chama vilevile Dr Slaa wanamchango mkubwa sana ndani ya historia ya CHADEMA mbona siku wameondoka hajawagawia Mali za chama ,hawana jasho lao humo, hiyo siyo dhuluma. Kama unashida na viwanja nenda CCM

Unapoandika comment shirikisha viongo vyote vya mwili
 
Umekata viroba sasa unashushsha na vipande vya nanasi unaongea kama mtu aliekata tamaa.Hata chadema wangekuwa madarakani wangeongea lugh hiyo hiyo
Kama mliweza kuchagua kambi rasmi ya upinzani bungeni bila ya kushirikisha wenzenu,mkichukua dola mtamsikiliza nani nyie wasanii?

Mkuu hata kama ni usanii tusingefikia hatua ya kura rambirambi
 
Ni vizuri ukaelewa tu, siasa kuhodhiwa ni ulimwengu mzima. Pale US mnapopaangali daily viko republic na democratic tu ..unaelewa ni kwanini?
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom