CCK imepata usajili, tuwape hongera!

Bado kuna Vacuum kubwa sana ki-itikadi ambayo ni opportunity kwa chama kingine chochote kipya au cha sasa kujiaza, hivyo kufanikiwa. Inabidi vyama vijenge core values zao based on itikadi, not based on mambo ya kupita kama katiba na ufisadi. Wananchi inabidi washibe itikadi za vyama, ili wananchi hawa wajenge imani za kudumu, na kupigania imani hizi huko makwao, hata kwa kujitolea, badala ya kushabikia mambo ya mpito.

Nilifanya kautafiti kidogo Arusha na Mbeya, nilikusanya vijana 20 randomly katika kila mikoa na kuwauliza, hivi nyinyi mnashabikia chama gani? Arusha, 16 of 20 said Chadema, Mbeya wote said Chadema. Nikawauliza, Chadema itikadi yake nini? Hawakunielewa, nikawauliza, kwanini mna imani na Chadema? hapo wakapata idea, na kusema kwamba wamechoka na Ufisadi wa CCM. Wengine pia walitaja suala la katiba. Nikawauliza, haya mawili yakipatiwa ufumbuzi je, mtakuwa wapenzi wa Chadema kwa sababu zipi? wakajibu kwamba Chadema wapo juu. Nikauliza, kivipi? Wakaanza kuzungumzia majina maarufu ya viongozi wa chadema kwamba wapo juu. Nikaondoka nikijiuliza, hivi kwa mfano ukiondoa viongozi wa chadema uwaweke pembeni, ukiondoa ufisadi, na ukiondoa suala la katiba, Chadema ina nguvu gani? Dont get me wrong, Chadema ina potential kubwa sana lakini bado sana kufikia mafanikio ya kudumu kwa sababa hawana core value iiliyokuwa unique na yenye mashiko ya kudumu kwa wananchi.

NCCR ilikumbwa na haya haya kwani kilipata mafanikio makubwa sana in the 1990s kutokana na sababu za mpito kama vile majina makubwa - Marando, Kaborou, Bagenda, Lamwai, Mrema, n.k, na pia kutokana na udhaifu wa uongozi wa Mwinyi uliozaa ufisadi mkubwa. Laiti NCCR wangewekeza kweney itikadi, leo tungekuwa tunaongea mengine, hata kama Nyerere alikuwepo. Otherwise, kampeni zikawa zaidi on personalities, Nyerere Versus Mrema and Crew. Chadema wakaze mwendo katika hili, kwani CCM sasa hivi kipo ICU, ila kinaweza kufufuka iwapo kitaliwahi suala la itikadi before Chadema. Otherwise tujiandae CCM kuanguka, Chadema kuchukua nchi, na baada ya miaka michache sana Chadema kupoteza nchi kutokana na wananchi kutoridhika na kasi ya Chadema kumaliza umaskini etc, kwani siasa za chadema za sasa zipo zaidi based on that, badala ya kuwa based on itikadi ambayo wananchi watakuwa tayari kuvumilia maendeleo ya kasi ya pole pole kwani vichwani watakuwa consumed zaidi na itikadi with hopes kwamba itikadi husika ndio njia sahihi kwa vizazi vyao vya baadae.

Kauli ya Dr. Slaa hivi karibuni kwamba "Kazi yetu ni kuikosoa serikali, ikirekebisha matatizo yote, tutaishiwa na hoja", inathibitisha mengi ambayo nimekuwa naimba kama mwendawazimu kuhusu umuhimu wa itikadi kwa chama. Ipo siku watanzania watakuja kulibaini hili, na hata humu JF, suala hili litakuja kuwa kubwa baada ya kutamkwa na watu wenye heshima au nafasi kubwa kwenye jamii yetu. Tuombe uzima.
 
hii ni ishara itakayo msaidia HR na wenzake wanapo anzisha chama chao hapo march waone jinsi CCK inavyo pokelewa
 
Chadema ina potential kubwa sana lakini bado sana kufikia mafanikio ya kudumu kwa sababa hawana core value iiliyokuwa unique na yenye mashiko ya kudumu kwa wananchi.

Hapa mkuu umenena, laiti kama viongozi wa CHADEMA wangekua wanapitia hapa, wangepata Challenge ya kujipanga vizuri
 
yaani mtu anakung'oa kwanza meno kisha anakupa mswaki hakuna cha kukipongeza cck hapo! majembe yote yameingia mitini hata wale ambao walikuwa nyuma ya pazia pale CCJ kushney. REST IN PEACE CCJ.
 
KWa kweli suala la itikadi, vyama vya upinzani hakuna kilichokuwa nayo, na wala hakuna chenye mpango wa kutengeneza itikadi na kuisimamia!!

Kama wenzangu walivyosema nashauri chadema kubadili mtazamo, la sivyo yatakuwa yale yale ya Zambia baada ya KK!!!
 
CCK,NCCR,CUF lao moja,chama cha upinzani Tanzania ni CDM
Zamani chama cha upinzani kilikuwa NCCR baadaye CUF kisha CHADEMA. Hivi mkuu unakumbuka CHADEMA mwanzoni haikupokelewa vizuri Watanzania. Wengine walisema ni cha Nyerere na wengine walikuwa wakisema Mtei katumwa! Kilionekana kama sehemu ya CCM lakini leo ndicho Chama Kikuu cha upinzani. Hivyo mkuu upinzani ni kupokezana vijiti
 
Vyama vyote vilianzishwa na uwt, jee CCK?

Wengine siasa ya Tanzania tunaichukulia kama Yanga na Simba. Hivi kuna mtu hapa haswa yuko serious kisiasa? Bado naona, na kama yuko asiyetakiwa basi ni Mtikila na yeye wamesha-mnyamazisha.

Haya tuone timu mpya iliyosajiliwa, itaweza ligi kuu au daraja la pili?
Mkuu heshima. Umesema kweli. Watu wengi hawajui historia ya vyama vingi. Mwanzoni hata mimi nilikuwa sijui basi kuna mwaka nikajitosa kwenye.maandamano kuelekea Bungeni kulikuwa na kikao cha Bunge. Basi kufika pale Ohio tukakutana na FFU tukapigwa mabomu. Cha kushangaza sikujua vionhozi wetu walivyotuacha tukikohoa na kutoa machozi. Walikuwepo Mtei (tulimpitia kisutu), Marando, Mzee Mapalala nk. Baada ya hayo mabomu ndio nikagundua kamchezo kachafu.
 
Ingekuwa busara kuimarisha vyama vilivyopo, otherwise itakuwa ni Miradi ya kutafuta ruzuku tu
 
Back
Top Bottom