CCJ yadai kuhujumiwa Pemba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Kiyabo.jpg

Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo.



Daftari lenye orodha ya majina ya wanachama wapya 450 wa Chama Cha Jamii (CCJ) Mkoa wa Kaskazini Pemba, linadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha kisiwani humo, huku uongozi wa taifa wa chama hicho ukiita tukio hilo kuwa ni hujuma.
Katibu Mwenezi wa CCJ, Dickson Amos, alisema jana kuwa orodha ya majina iliyokuwamo kwenye daftari hilo ni ya wanachama ambao walikusudiwa kufanyiwa uhakiki ili kupata usajili wa kudumu.
“Kuna hujuma zinafanywa dhidi yetu. Leo (jana) tumepigiwa simu kutoka Pemba. Daftari lenye orodha ya majina ya wanachama, ambao walitakiwa wafanyiwe uhakiki limepotea Mkoa wa Kaskazini Pemba katika mazingira ya kutatanisha,” alisema Amos.
Alisema kabla ya hujuma hiyo kufanyika, walipanga uhakiki wa wanachama uanzie kufanyika katika Mkoa wa Kaskazini Pemba na kisha uendelee katika mikoa mingine ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Taarifa za tukio hilo zimetolewa siku moja baada ya chama hicho juzi kushindwa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini maombi ya kupatiwa usajili wa kudumu kama kilivyokuwa kimetangaza awali.
Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo, alikaririwa akisema jana kuwa hali hiyo ilitokana na hitilafu zilizotokea katika fomu za majina ya wanachama 2,000 ‘waliovunwa’ katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo mtu aliyepewa jukumu la kuzikusanya kutoka mikoa hiyo, alichukua fomu zilizorudufiwa badala ya halisi.
Wakati hayo yakijiri, baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanadaiwa kukutana juzi katika moja ya ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam na kujadili namna ya kufanya ili kukwamisha CCJ isipate usajili wa kudumu.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom