CCJ wamvutia pumzi Tendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCJ wamvutia pumzi Tendwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa


  Kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa ya kutangaza kuipa kipaumbele Sheria ya Gharama za Uchaguzi katika shughuli za ofisi yake kipindi hiki dhidi ya mambo mengine, ikiwamo uhakiki wa wanachama wa Chama Cha Jamii (CCJ) kwa ajili ya kupatiwa usajili wa kudumu, imezua mkanganyiko mkubwa miongoni mwa viongozi wa chama hicho.

  Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mwenezi wa CCJ, Costantine Akitanda, alisema wameipokea kauli ya Tendwa kwa uzito mkubwa, hivyo wamelazimika kukutana ili kuitafakari kwa kina.

  "Ni kauli nzito sana aliyoitoa. Inahitaji kuitafakari kwa kina. Hivyo, viongozi wanakutana, na tutatoa tamko letu baadaye," alisema Akitanda.

  Awali, Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi, alisema pamoja na kauli hiyo ya Tendwa, wanachoamini wao ni kwamba, wamekamilisha yote yaliyohitajiwa katika nyaraka za maombi ya kupatiwa usajili wa kudumu waliyoyawasilisha ofisini kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Ijumaa wiki iliyopita.

  "Hayo mambo kwamba hana pesa, anaipa kipaumbele Sheria ya Gharama za Uchaguzi, sisi hayo hayatuhusu. Tunachokijua sisi ni kwamba, tumekamilisha kila kitu. Hivyo, tunakutana na baadaye tutatoa taarifa yetu," alisema Muabhi.

  uzi Tendwa aliitisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake na katika jumla ya mazungumzo yake, alieleza bayana kwamba, suala linalopewa kipaumbele na ofisi yake katika kipindi hiki, ni kushughulikia Sheria mpya ya Gharama za Uchaguzi.

  Tendwa alitoa kauli hiyo zikiwa zimepita siku tano tangu viongozi wa CCJ, wawasilishe ofisini kwake maombi ya usajili wa kudumu, huku wakielezea matumaini yao ya kupatiwa usajili huo katika muda mwafaka ili waweze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

  Mkutano huo uliitishwa na Tendwa kwa lengo la kuwaomba waandishi wa habari waisadie ofisi yake kuielimisha jamii kuifahamu vyema Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambayo alisema kuwa ni "ngumu".

  Alisema anazo taarifa za CCJ kuwasilisha katika ofisi yake nyaraka za maombi ya kupatiwa usajili wa kudumu zenye orodha ya wanachama wao kutoka mikoa 10 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

  Hata hivyo, alisema nyaraka hizo ziliwasilishwa katika ofisi yake Ijumaa wiki iliyopita, lakini hadi kufikia juzi, zilikuwa hazijafika mezani kwake.

  Alisema kwa sasa ofisi yake haina fedha za kufanya uhakiki ili kujiridhisha kama wanachama walioorodheshwa kwenye nyaraka zilizowasilishwa na CCJ katika ofisi yake, hawana utata wowote wa kisheria.

  Alisema hata ofisi yake kama itakuwa na fedha, itabidi akutane kwanza na uongozi wa CCJ kupanga lini waanze safari ya kwenda mikoani na waanzie mkoa gani kufanya uhakiki wa wanachama wao.

  Hata hivyo, Tendwa alisema: "Priorities (vipaumbele) kipindi hiki ni Sheria ya Gharama za Uchaguzi." na kuhitimisha kwa kusema: "Agosti 19 ni tarehe ya mwisho kwa vyama kuwasilisha majina ya wagombea wao. Sasa kama kufikia tarehe hiyo CCJ watakuwa wamekamilisha taratibu za usajili (wa kudumu), watashiriki uchaguzi."

  Aidha, alisema watahakikisha wanafuata taratibu na sheria na kwamba, wataiendea haki CCJ.

  CHANZO:
  NIPASHE
   
 2. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Katika mazingira kama haya hiyo haki itatoka wapi? Ili kumkomoa na asipate visingizio CCJ wajitolee kumlipa posho na nauli ya kuzunguka mikoani!
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  pisha njia weee pisha njia weee

  hao ndio chama tawala, wako kila eneo. sasa nguvu zao na za shetani kubwa zipi?
   
 4. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ??//////????????
   
Loading...