CCJ wamefanya nini kustahili dhamana ya kuongoza nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCJ wamefanya nini kustahili dhamana ya kuongoza nchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bigirita, Jun 29, 2010.

 1. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Hili lilikuwa swali la MMKJJ kwa CHADEMA November 2009!!

  Naona MMKJJ mahesabu yake hayakuwa sawa!! kama anatumia kigezo cha KUFANYA NINI, Namuuliza, CCJ imefanya nini mpaka tuipe dhaman aya kuongoza nchi???
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Si hilo tu, Tungependa kujua kwanza ni akina nani hao waliounda CCJ. Tukishawafahamu na kufahamu ruuya yao kwa Tanzania tunaweza
  kuwaunga mkono.
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Ndiyo mkuu, maswali yajibiwe, tusisahau kuwa siasa na uwanaharakati sio sawa!! mtu akiamua kuwa mwanaharakati siku akigeuka kuwa mwanasiasa, ni sawa na kugeuka misingi uliyojiwekea!! MMMKJJ anageuka misingi aliyojiwekea, sasa moja na moja inakuwa 11 na anaona ni sawa tu!!
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kuongoza nchi si kazi ya wanasiasa. Hapo ndipo wadanganyika mnapoanzaga safari wrong-footed.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hili linajibu vipi swali la awali?
   
 6. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwasasa CCj haistahili kupewa uongozi wa taifa!

  Uzembe wa viongozi wao kwenye usahili unaongea mengi sana from management point of view.
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Naona napata swali lingine. CCM awamu ya nne wamefanya nini kustahili kuendelea na dhamana ya uongozi wa taifa? Is there anything they can show to intelligent men kuwa walifanya na watafanya nini wakipewa tena 2010.

  Mwanakijiji unaweza kutuma ka-inzi kako kwenye ofisi ya CUF, maana kwa uzoefu wangu wa siku za nyuma inaonekana kuwa mchezo unakuwa wa kawaida. CUF inashinda CCM itawala, CUF wanacharazwa bakora unaitishwa mwafaka, life goes on. Naona this time around kumekuwa kimya kiasi au ndio kuwa viongozi wachache wa CUF wamelambishwa asali, wanakaa kimya, halafu wataanza kulalama baada ya Oktoba? Huko Zanzibar nako kula swali kama hilo wamefanya nini kustahili tena dhama ya uongozi??
   
Loading...