CCJ kumburuza kortini Msajili vyama vya siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCJ kumburuza kortini Msajili vyama vya siasa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 6, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Wabaini namba za wanachana kubadilishwa  [​IMG]
  Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa  Uongozi wa Chama Cha Jamii (CCJ), umeibuka na kutoa madai ya kufanyiwa hujuma baada ya kugundua namba za wanachama wake zilizokuwa ndani ya fomu za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini zimebadilishwa.
  Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi, alisema kutokana na kubainika kwa kasoro hiyo, wamepanga kumfikisha Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa mahakamani Jumatatu (kesho) ili asiendelee na zoezi la kuhakiki wanachama wao hadi hapo hali hiyo itakaporekebishwa.
  Muabhi alisema, baada ya kuvunjika kwa uhakiki wa wanachama wa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na watu wengi kuonekana sio halali, uongozi umegundua fomu alizokuwa nazo Tendwa nyingi zimebadilishwa namba pamoja na majina ili kuhakikisha kinashindwa kupata wanachama wa kutosha na kunyimwa usajili ya kudumu.
  "Kwa kweli tumebaini kuna njama zimefanyika kwa kubadilisha namba kwenye fomu alizokuwa nazo Msajili, lakini hilo litamalizwa kisheria kwa sababu tunatarajia kwenda mahakamani kupinga mchakato wote wa kuhakiki wanachama hadi hapo totakapokaa na kumaliza tatizo hili," alisema Muabhi.
  Katika zoezi hilo lililofanyika Jumatano iliyopita katika Viwanja vya Mwembeyanga, wanachama 40 waliofanikiwa kuhakikiwa kabla ya zoezi hilo kusitishwa, 27 walishindwa kutambuliwa na Msajili baada ya kuonekana sio halali na 13 pekee ndio waliotambuliwa.
  "Kitu hiki bado kinatuumiza kichwa sisi kama viongozi wa CCJ, haiingii akilini tuwe na wanachama 13 tu ikiwa tulikuwa na maandalizi ya kutosha kabisa, hili jambo lazima tutakwenda mahakamani ikiwa ni pamoja na kumzuia Tendwa asiendelee kuhakiki wanachama wetu bila ridhaa yetu," alisisitiza.
  Aidha, alisema ametoa agizo kwa viongozi wa mikoa yote itakayotembelewa na Msajili kutotoa ushirikiano wowote kwa sababu wao wamejitoa.
  Aliwataka wanachama wa chama hicho kutulia kwa kuwa ana matumaini makubwa suala hilo litatatuliwa haraka ili uhakiki huo urudiwe kwa mara ya pili.
  Hata hivyo, Tendwa alipozungumza wakati akiendelea na zoezi la uhakiki wa chama hicho Ifakara mkoani Morogoro, alisema fomu alizokuwa nazo ni halali kitu ambacho hata viongozi wa CCJ wanakitambua, bali kinachofanyika sasa ni kulidanganya taifa.
  Alisema, anachoendelea kukiona katika ziara yake hiyo ni kitu ambacho hakukitarajia, kwani kuanzia uhakiki wa Mkoa wa Pwani hadi alipofika Ifakara jana hakuweza kumpata hata mwanachama mmoja.
  "Nadhani CCJ wanaliongopea Taifa, hawa watu hawana wanachama kama wanavyodai, jambo hilo ndilo nakumbana nalo kwenye ziara yangu kuanzia jana (juzi) Kibaha na sasa Ifakara hali ni hiyo hiyo, japokuwa huku nimeona ofisi yao," alisema.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...