Castle lite yadhamini mashindano ya mpira wa kikapu, 11-17 dec, 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Castle lite yadhamini mashindano ya mpira wa kikapu, 11-17 dec, 2011

Discussion in 'Sports' started by magesa, Dec 7, 2011.

 1. m

  magesa Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dar es Salaam, 07, DECEMBER 2011

  Kampuni ya BiaTanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Castle Lite, leo imetangaza udhamini wamashindano ya mpira wa kikapu yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanziatarehe 11/12/2011 hadi tarehe 17/12/2011.

  Akizungumziaudhamini huo Meneja wa Bia ya Castle Lite Bi. Pamela Kikuli alisema;"Tunafurahi sana kupata nafasi hii ya kudhamini mashindano haya muhimu,tumeamua kushirikiana na Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kuhakikisha mashindano haya yanafanyikakatika hali ya ufanisi mkubwa. Mchezo wa mpira wa kikapu umekuwa na mvutomkubwa na kuendelea kujizolea mashabiki wengi hapa nchini na Ulimwenguni kwaujumla. Zaidi ya kuwa chanzo kizuri cha ajira kwa vijana, mchezo huu pia unatoafursa kwa washiriki kufanya mazoezi ya kutosha na hivyo kuwa na afya borawakati wote".

  Bia ya Castlelite ambayo inawalenga na kuhamasisha zaidi watu wanaojali afya zao, imeamua kuoneshahayo kwa vitendo kwa kudhamini mashindano haya na kuhakikisha inashirikiana navyombo husika kuhakikisha kuwa mchezo wa mpira wa kikapu unakuwa hapa nchini.Aliongeza Bi. Pamela.Akizungumziathamani ya udhamini, Bi Pamela alisema; Castle Lite imetoa jumla ya shilingiMilioni Ishirini na Nane (28,000,000/-) ili kufanikisha mashindano haya. Tunaimani kuwa fedha hizi zitatumika vema katika maeneo yaliyokusudiwa ili kuletatija katika mchezo huu wa mpira wa kikapu na tutaendelea kuwa mstari wa mbelekuendeleza mchezo wa kikapu hapa nchini.

  Nae menejamahusiano na habari wa TBL Bi. Edith Mushi akitaja mikoa itakayoshiriki alisemamashindano hayo kwa mwaka huu yatashirikisha mikoa 19 ya Tanzania Bara naVisiwani, ambayo ni
  ILALA, KINONDONI, TEMEKE (IKIWA NI MIKOA MIPYA YAKIMICHEZO YA DAR-ES-SALAAM), ARUSHA, KILIMANJARO, TANGA, ZANZIBAR, PEMBA,LINDI, MTWARA, MBEYA, IRINGA, MOROGORO, MANYARA, MARA. MWANZA, SHINYANGA,TABORA NA RUKWA.
  Alisemamashindano hayo yatashirikisha timu za wanaume na wanawake na yanatarajiwa kuwana msisimko mkubwa miongoni mwa jamii ya wanamichezo kote nchini. Mashindanohaya pia yatakuwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kwaupande wa mpira wa kikapu.

  Kwa upande wake Makamuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania Bw. Phares Magesa, alitoashukurani na pongezi nyingi kwa Bia ya Castle Lite kwa ushirikiano mkubwawaliotoa kwa kudhamini mashindano haya ya mwaka 2011 yatakayoshirikisha timu 24kutoka mikoa 19 ya Tanzania. "Castle Lite imeonesha moyo wa Uzalendo kwa kuwamstari wa mbele kudhamini mashindano haya, kwa kushirikiana na mdhamini huyutuna imani kubwa kuwa mchezo wa mpira wa kikapu utapata msukumo mkubwautakaoleta maendeleo ya kweli katika mchezo huu hapa nchini; Alisema Magesa.

  Sisi viongozi wa shirikisho na wapenzi wa mpira wa kikapu hapa nchini, Tuna imani kubwa kuwaudhamini huu utaongeza chachu ya ushindani kwa timu zitakazoshiriki na hivyokuongeza tija katika mchezo huu hapa nchini. Tunawaomba wapenzi na mashabiki wampira wa kikapu kujitokeza kwa wingi katika viwanja viliyvotajwa ili kujakushuhudia na kushangilia timu zao wakati wote wa mashindano.

  Amesema udhamini waCastle Lite utalenga maeneo yafutayo - kwanza tumezipa kipaumbele sana timuzinazotoka nje ya Dar es salaam kwa kuzisaidia fedha kiasi za kujikimu ambapobajeti itagharimu kiasi cha Tzs milioni 22,400,000/ ikiwa ni kiasi cha TShs.900,000.00 kwa kila timu itakayoshiriki kutoka nje ya Dar-es-Salaam. Zawadiikiwa ni pamoja na fedha taslimu – TSh. 2,000,000.00; Vikombe kwa washindi wa kwanzana wa pili pamoja na mchezaji bora na medali kwa mshindi wa kwanza, vitagharimuTzs Milioni 1,200,000/. Gharama za kulipia viwanja zitakuwa ni Tzs 3,000,000/; Malipoya waamuzi ambayo imetengwa Tzs Milioni 2,100,000/; T-Shirts kwa washiriki woteTSh. 3,000,000.00. Jumla ya mchanganuo huu ni TShs. 33,700,000.00. Alisema TBFitachangia kiasi cha Shs. 5,700,000.00 za ziada toka katika vyanzo vingine.

  Tunaomba ielewekekuwa gharama hizi hazitoshi kukidhi mahitaji yote ya kuendesha mashindano laTaifa Cup lakini tunaishukuru TBL kupitia Bia ya Castle Lite kwa udhamini huuambao umeonesha njia, na tunawashukuru mikoa yote iliyokubali kushiriki katikamashindano haya kwa kujitolea kwao kutafuta vyanzo vingine vya pesa kukidhimahitaji ya ushiriki.

  Mwisho tunawashukuru sana Waandishi wa Habari wote kwa ushirikiano wenu toka tulipoanza mchakato wa Taifa Cup tunaomba tuendelea mpaka mwisho wa mashindano hayo.

  -MWISHO-

  Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
  Pamela Kikuli – Castle Lite BrandManager, +255767266415, pamela.kikuli@tz.sabmiller.com

  Editha Mushi, Communications &Media Manager, +255767266420, editha.mushi@tz.sabmiller.com

  Dorris Malulu, Public AffairsAdministrator,+255767266049, doris.malulu@tz.sabmiller.com

  Phares Magesa, Vice President,Tanzania Basketball Federation,
  +255 784 618320E-mail:
  magesa@magesa@hotmail.com,

  Michael Maluwe, Asst. Secretary General, Tanzania Basketball Federation,
  +255 717 053876 Email:
  michaelmaluwe@yahoo.com
   
Loading...